Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili tangazo umelipia sh ngap? Nimependa Jinsi ulivyojitangaza, hongera sana😊Ningependa kutoa somo la bure kwa wale ambao wanawaza jinsi gani wanaweza kuanza kuagiza bidhaa kutoka china.
Bidhaa hizi ni za jumla kwa ajili ya biashara.
Utaagiza moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji.
Kupitia uzi huu utaweza kuona bei halisi za bidhaa pamoja na kujua ni jinsi gani utasafirisha mpaka mzigo unakufikia ulipo.
Pia utafahamu ni kwa namna gani utamtambua mzalishaji gani wa bidhaa utaweza kumtumia na yupi sio salama kumtumia.kuokoa pesa zako zisipotee.
Haya yote utaweza kuyafanya kupitia simu yako ya mkononi.
Niamini mimi haya mambo yanawezekana huhitaji mtu wa kukushika mkono zaidi ya huu mwongozo.
Watu wanapiga pesa kwa kuagiza bidhaa kupitia mtandaoni tu bila hata ya kukanyaga china.
Bidhaa utakayouziwa bongo 80,000 - 100,000.Jua mfanyabiashara huyo kainunua china 20,000 - 30,000.
View attachment 2945112
Bei ya china
View attachment 2945113
Bei ya Kuuzia Tanzania
Ijapokuwa kuna gharama za usafiri ila haiwezi zidi 15,000 mpaka 20,000 kwa kila blender.. hapo utaona gharama mpaka inamfikia mkononi mfanyabiashara ni 35,000 mpaka 40,000.
Ingia alibaba fanya utafiti wa bidhaa mbalimbali naamini huwezi kosa idea ya nini utaweza kuagiza na kuanza kuuza kwa faida nzuri.
Hata kama huhitaji kwa sasa embu download hii application, ufanye japo research ya kujua bei za bidhaa zipo vipi huko viwandani na huku masokoni wanauzaje.
Chunguza bidhaa zinazouzika mtandoni au madukani kisha jaribu kuja kuangalia viwandani china wanauzaje..kisha ujionee ni kwa jinsi gani watu wanapiga faida ndefu.
Tena kwa mikoani ndio usiseme.Kama mtu akinunua mzigo kariakoo anapata faida jee akiagiza kutoka china moja kwa moja itakuwaje?
HATUA YA KWANZA
1.Download application ya alibaba kupitia playstore au appstore.
Hiki ni zoezi rahisi tu.Ingia play store kwa wale wa android na appstore kwa wale wa iphone.
Application inaitwa alibaba
View attachment 2945124
Kisha idownload hakikisha unajisajili kupitia email ambyo ipo active kwenye simu yako na pia utakapohitajika kuweka namba ya simu weka namba ambayo ipo active kwenye simu yako.
ili watakapohitaji kufanya verification email na simu yako ziwe active kwa zoezi hilo.
Hatua hii ni fupi sana. Achana na taarifa za biashara wewe weka tu taarifa zako binafsi kisha anza kuperuzi..
Baada ya kujisajili unaweza kuamua kubadili fedha itakayoonekana kweny bidhaa ili uweze kupata picha ya bei kwa pesa yetu ya Tanzania.
Chini kulia kuna neno alibaba bonyezahl hapo kisha juu kulia utaona USD sasa ibonyeze kisha tafuta pesa ya tanzania TZS ili bidhaa zote zionekane kwa bei ya tzs
View attachment 2945131
Baada ya hapo unaweza sasa kuanza kutafuta bidhaa.
Kuna aina kuu mbili za utafutaji ningekushauri uanze nazo
.Kutafuta bidhaa (product)
.Kutafuta mzalishaji wa hiyo bidhaa (Supplier/manufacturer)
View attachment 2945132
Hapo juu utaona nimeandika hand bags halafu juu yake kuna maneno mawili products na manufacturers
Hapo juu nimechagua products ndii maana unaziona bidhaw mbalimbali na bei zake.
Ukichagua products wanakuletea bidhaa tu na ukichagua manufacturers wanakuletea viwanda/wauzaji wa hizo bidhaa tu.
Ili kama utataka kuona wauzaji uweze kuangalia bidhaa zao mbalimbali zinazohusiana na bidhaa uliyochagua.
Hapa chini nimechagua manufacturers/supplier utaona wananiletea majina ya viwanda au wauzaji wa aina hizo za bidhaa
View attachment 2945137
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA KUMCHAGUA SUPPLIER MZURI
1.Hakikisha ana alama ya verified (angalia picha hapo juu)
2.Mbele ya neno verified kuna miaka ambayo yupo katika mtandao wa alibaba.Kuanzia miaka 2 na kuendelea si mbaya ila angalia sifa ya 3 kujiridhisha zaidi
3.Angalia review (wanunuzi wanamzungumziaje huyu muuzaji)
hili ni muhimu pia.
View attachment 2945145
View attachment 2945146
Review itakusaidia kupata picha ya jinsi mzalishaji huyo au msambazaji anavyohudumia wateja wengine au ubora wa bidhaa yake..
Kitu kingine ni Trade Assuarance. Hii ni huduma ya alibaba ambayo pesa yako inakuwa haiend moja kwa moja kwa muuzaji mpaka alibaba watakapo kuridhisha kuwa hauna malalamiko yoyote juu ya muuzaji huyo.
View attachment 2945148
Unaweza muuliza huyo muuza kupitia chat now hapo kama ana support trade Assuarance.
Kitu unachotakiwa kufanya utakapo jiridhisha na bidhaa husika ni kubonyeza hiyo chat now ili uweze kuchat na muuzaji kabla hamjakubaliana kufanya malipo.
Unaweza muuliza wanaweza kuuuzia bidhaa ngapi kama MOQ (minimum order quantity) yaan idadi ndogo wanazoruhusu mtu kununua kutoka kwao.
Wapo wafanyabiashara wanaruhusu bidhaa kuanzia 10 wengine kuanzi 100 wengine 5 au hata 1.
Sasa ipo hivi ikiwa unataka ujihakikishie ubora wa bidhaa yaan uipate kwanza 1 ujiridhishe zaidi ongea na huyo suppier akutumie sample 1 ya bidhaa yao kwa njia ya ndege ili ukiipata hiyo bidhaa utajiri dhisha na kuamua kununua bidhaa nyingi zaidi kwa ajili ya biashara.
Hii itakusaidia kujiondoa katika riski ya kuagiza mzigo mkubwa ambao ukifika utajutia kwa kuwa haukidhi vigezo vyako.
Japo bei ya bidhaa ya sample 1 huwa kubwa kidogo ila ni bora zaidi kwa kuwa unajiridhisha kwa mara ya kwanza kujua ubora wa bidhaa.View attachment 2945152
Ukisha fanya resarch yako ya kutosha na ukaona umejiridhisha na bidhaa na bei na idadi ya bidhaa unazohitaji.
Mambo ya muhimu ya kuzingatia maana hapo ni bei ya bidhaa huko china.
unatakiwa ujue huu mzigo kuusafirisha mpaka unakufikia gharama yake ni kiasi gani na utatumia muda gani mpaka kukufikia?
Kuna mizigo unaweza safirisha kwa ndege hiu unawahi kufika inaweza chukua siku 7 tu kulingana na ratiba za ndege.
mizigo hii hupimwa kwa uzito kgs.
Ukishajua uzito wa bidhaa zako unawasiliana na agent wa kukusafirishia mzigo na kumueleza uzito na aina ya mzigo wako ili akupe bei kwa kilogram 1 ni kiasi gani.
Kuna mzigo inabidi uusafirishe kwa meli hii mizigo hupimwa mwa ujazo wa mita CBM (Cubic Metres) yaani urefu * upana * kimo vyotr katika metres.
Hapo unaweza muuliza muuzaji wako huu mzigo una CBM ngapi ukiufunga pamoja.
Muuzaji akikupa CBM nenda kwa agent wako wa kusafirsha mzigo akupe gharama kulingana CBM ya mzigo wako.
Baada ya kuona gharama za mzigo pamoja gharama za usafirishaji unazimudu.
Ndio unaweza kumwambia akuandalie payment link.
Hii ni link maalum ambayo ukiibonyeza inakuletea gharama za kulipia oda yako.
View attachment 2945166
Utaona hapo baada ya kukubaliana na supplier gharama akanipa hiyo link ya kulipia.
Ambayo inahitaji nilipe initial deposit 50% kisha wakimaliza kuandaa mzigo wangu nawamalizia 50% kisha wanatuma.
Hiyo link ukiibonyeza inakupeleka kwenye aina za malipo uchague
Mimi nachaguaga paypal kwakuwa nimeiunga na bank account yangu.
yaan haina longolongo zaidi ya verification ya simu yangu tu.
paypal itanionesha kiasi nacholipia katika usd na kiasi kinachokatwa katika account yangu ya TZS.
View attachment 2945170
Ukibonyeza agree & pay now hakikisha kiasi hicho kipo kwenye account yako.
Hapo malipo yataenda alibaba na supplier atapata taarifa na kuanza kushughulikia oda yako kulingana na makubaliano.
Hakikisha umempa supplier wako address ya agent ambaye atakusafirishia mzigo.
Supplier atapeleka mzigo kwa agent na baada ya hapo ni kazi ya agent kukuletea mzigo wako hapa Tanzania.
Maagent wapo wengi kuna silent ocean, mapembelo cargo, tosh cargo kuna shamwaa n.k.
watafute maagent hawa kisha wakupe address zao za huko china ili supplier apelek mzigo wako kwao.
View attachment 2945177
Hizo ndio hatua utakazohitajika kufuata ili kuweza kuagiza mzigo wako kutoka kwa wazalishaji china mpaka kukufikia Tanzania.
Ikiwa utahitaji msaada zaidi wa namna ya kuagiza bidhaa kutoka china.
Napatikana whatsapp tu +255677818283
Madini mazuri sana mkuu,tunashukuru VP pia kuhusu kuagiza bidhaa nchi kama Korea,uturuki,Dubai waweza tupa machimbo ya sites kama wafahamuNingependa kutoa somo la bure kwa wale ambao wanawaza jinsi gani wanaweza kuanza kuagiza bidhaa kutoka china.

Alibaba ni kwa ajili ya wauzaji wa jumla hasahasa na AliExpress ni kwa ajili ya reja rejaNataka nijue hii kwanini usafiri Alibaba ni ghali mno ? Yani ukitaka sample ata saa ya $2 pc 1 seler atakwambia kuhusu agent wa usafiri
akifanya calculation zake ajabu inakuja samp $2 usafiri $50
Tofauti na Ali express unachukua mzigo labda flash ya $2 pc1 na unakuta usafir labda 800 na unalipa chap Kwa Kesho Tu email hii mzgo upo njiani
lakini hizi zote ni za China Ali express na Ali Baba
lakini
Ukitaka simu ya $100 pc1 Alibaba usafiri inakuja mpaka $150
Lakini Ali express hii ya $100 unakuta usafir labda $10 or 15 kwanin inakua hivi ?
campuscitymall.com
nzuriChukua machimbo ya biashara ukafanye biashara (Namba za simu 600 za machimbo na location zake)!
KINAUZWA
Kitabu cha Machimbo ya Biashara
Kitabu chenye machimbo 600 ya biashara kwa TSH 15,000 tu!
Kitabu hiki kina namba za simu 600 za wauzaji wa bidhaa kwa bei nafuu, jumla na rejareja.
Jinsi ya kukipata WHATSAPP: 0612607426
CALL: 0687746471
Unaweza kupakua kitabu hiki kupitia link hii:
![]()
Kitabu cha Machimbo ya Biashara Kariakoo bidhaa za jumla na rejareja bei nafuu
Ni kitabu kizuri sana kwa wafanya biashara. Kina namba za suppliers 600 wa jumla na rejareja. Kina maduka ya wachina yanayo patikana Kariakoo. Whatsapp: 0612607426 Email: bandg.editors@gmail.comcampuscitymall.com
Kwa msaada wa kupakua, wasiliana kupitia:
WhatsApp: 0612607426
Call: 0687746471
Kitabu kina sura 68 kama ifuatavyo:
Sura ya 1 hadi 5: Machimbo ya nguo za watoto, vifaa vya ofisini (stationery), vifaa vya ujenzi (hardware), dawa (pharmacy), na vinywaji.
Sura ya 6 hadi 10: Kahawa, maremba, vifaa vya mazoezi, miwani, na nywele bandia kama rasta na wigs.
Sura ya 11 hadi 20: Shati za shifoni, viatu, kofia, gauni za usiku, vitambaa vya masofa, hereni na cheni, vyombo vya jikoni, na vifaa vya michezo.
Sura ya 21 hadi 30: Pajamas, balo za mitumba, masweta, maturubai, pipi, jeans, jezi, na vifaa vya kufungashia.
Sura ya 31 hadi 40: Toys, T-shirts, diaper, bidhaa za supermarket, manukato, madera, mitandio, abaya, hijabu, na vitenge.
Sura ya 41 hadi 50: Khanga, vitambaa vya kushona, vipodozi, nguo za watoto, pochi, vifaa vya simu, mikeka, bidhaa za wachina, na sufuria sets.
Sura ya 51 hadi 60: Chupa za maji, midoli, lubricants za magari, maduvets, mashuka, mapazia, majora ya mapazia, T-shirts zinazotrend, na bidhaa za ubuyu wa Zanzibar.
Sura ya 61 hadi 68: Maua artificial, pipi, vifaa vya masofa, bidhaa za mitumba, vifaa vya kuandaa keki, na bidhaa kutoka kwa wachina moja kwa moja.
Mkuu custom clearance ndio kitu gani sorryUnafuu upo mkubwa sana rejea uzi kwa utaratibu ...ingia alibaba tafuta bidhaa utaona tu unafuu
Ko ukiagiza mzigo ushuru unalipia mwenyewe nimejaribu item moja wameniambia nifanye custom clearanceMasuala ya upitishaji mizigo inayoingia nchini...hapo inahusisha mambo ya ushuru na kodi za kutoa mizigo
Kipi bora sasaUkiagiza kupitia agent yeye ndio ataclear kila kitu lakin ukiagiza mwenyewe na uka upokea wewe mwenyewe utalipia
Mfano agent wa hii kitu nampatajeTumia agent...
kwakuwa hata kabla mzigo haujafuka anakupa bei ya kusafirisha mpka mzigo unautoa unakabidhiwa ina maana utajua huu mzigo una faida au hasara kabla hata kujanunua