SoC03 Somo la uadilifu na Utawala Bora lianzishwe na liwe somo la lazima kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu. Taasisi za Dini, na Familia zihusike pia

Stories of Change - 2023 Competition

Fannjosh

Member
Joined
May 28, 2016
Posts
35
Reaction score
46
UTANGULIZI

Uadilifu ni hali ya kuwa mwaminifu na kuzingatia kanuni zote za kimaadili katika jamii inayokuzunguka.
Kwa upande mwingine, utawala bora lazima uwe na uadilifu ndani yake.
Jamii haiwezi kuwa na watawala walio bora ikiwa hawana uadilifu.

UMUHIMU WA UADILIFU KATIKA JAMII
  • Uadilifu huchochea uwajibikaji. Kiongozi yeyote aliye mwadilifu lazima awajibike katika nafasi yoyote atakayopewa kuisimamia.
  • Uadilifu hujenga utawala bora. Utawala wenye kuheshimu haki za raia, kujali mahitaji ya watu na kufuata sheria huchangiwa kwa kiasi kikubwa na uadilifu.

Ili nchi yoyote iwe na viongozi imara na wenye kujali maslahi mapana ya watu, lazima viongozi hao wawe waadilifu. Uadilifu hauwezi kujengwa kwa mtu kipitia sheria, bali unaweza kujengwa kwa mtu tangu utotoni.
Kama taifa, tunaweza kutumia vyema rasilimali tulizonazo na kupata maendeleo makubwa ikiwa wanaoongoza watu watakuwa waadilifu katika nyanja zote za kimaisha.

MATOKEO YA KUWA NA VIONGOZI WASIO WAADILIFU

  • Rushwa huongezeka. Kiongozi huweza kupindisha haki ya mtu na kufanya maamuzi yasiyo sahihi kwa kupokea rushwa ikiwa tu si mwadilifu.
  • Matumizi mabaya ya madaraka
  • Kupindisha sheria
  • Kufanya ufisadi nk.

NINI KIFANYIKE ILI KUJENGA KIZAZI CHENYE UADILIFU NA UTAWALA BORA

Kubadili mtu mzima asiye mwadilifu ni kazi kubwa sana. Hata sheria inaweza isifanikiwe kumbadili mtu huyo.
Hivyo basi, ili kuwa na kizazi chenye uadilifu, lazima watoto wadogo waanze kufundishwa uzuri na ubaya wa kukosa uadilifu katika shule ngazi zote, taasisi za kidini, jamii na familiya kwa ujumla.
Kufundisha watoto kuhusu utawala bora na uadilifu kutajenga viongozi wazuri watakaoweza kulifikisha taifa mahali pazuri hapo baadaye.

Hivyo basi, Serikali ianzishe somo maalumu la uadilifu na utawala bora katika ngazi zote za elimu, na iwe lazima kufundisha somo hili kwa yeyote anayeitwa mwanafunzi bila kujali anasomea nini hata ngazi za vyuo.

Pia, taasisi za kidini, wazee katika jamii pamoja na Familiya, kila mmoja aone tatizo la kukosa uadilifu kwa viongozi na tuimbe wimbo wa uadilifu kila siku ili kuamsha hali ya uadilifu katika jamii.

Pia zianzishwe clubs mbali mbali mashuleni kama ilivyo clubs za Rushwa ili kuongeza uzito kwa wanafunzi juu ya umuhimu wa uadilifu na utawala bora katika jamii.

Tafadhari bonyeza Vote hapo chini kama umependa chapisho hili. Asante sana.
 
Upvote 8

Vzuri
 
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom