Somo la uchumi (Economics) linapaswa kufundishwa kuanzia kidato cha kwanza kwa wanafunzi wa mchepuo wa biashara (Bookkeeping/Commerce)

Somo la uchumi (Economics) linapaswa kufundishwa kuanzia kidato cha kwanza kwa wanafunzi wa mchepuo wa biashara (Bookkeeping/Commerce)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari zenu ndugu wa Jamii Forums.

Kama ni kweli Tanzania inataka kuandaa wachumi na wataalam wazuri wa kutunza hesabu, sasa wakati umefika kwa wataalam wa elimu kuruhusu wadogo zetu wanaochukua mchepuo wa biashara (ECA) kuanza kusoma somo la uchumi (Economics) kuanzia kidato cha kwanza kama ilivyo kwa wale wa PCM, PCB, HGL, CBG na HGK. Tanzania ya mwaka 2011 sio hii ya sasa ya mwaka 2021. We need to change folks.

Guys let me tell you one thing here. Hakuna level nzuri ya kuandaa wataalam kama kidato cha kwanza mpaka cha nne. Unajua kwanini? Sababu kuu ni hii. Mwanafunzi wa kidato cha pili anapojiandaa na mitihani, huwa analazimika kusoma mpaka yale ya kidato cha kwanza.

Yule wa kidato cha tatu akisikia papers zimekaribia anasoma kuanzia yale ya form one, two pamoja na three. Kidato cha nne kikifia ambao ndio mwaka wa mwisho mwanafunzi anajikuta anasoma yoooote ya kidato cha kwaza, cha pili, cha tatu na kile alichopo cha nne, hivyo kumuwezesha kujua masuala mengi madogo madogo katika taaluma yake ile.

Elimu ya chuo mtu akisoma semester moja akafanya papers kisha akafaulu, ndio basi tena hiyo hata akifika semester ya mwisho ya mwaka wa tatu halazimiki tena kusoma masula ya mwaka wa kwanza kwa maana haji kuulizwa katika mtihani wake wa mwisho.

Sasa utaniambia mhasibu aliyesoma Bookkeeping tangia form one, form six hadi chuo anaweza kulingana na yule aliteyetoka PCM Ilboru kisha wote wakaenda kusoma Accountancy UDSM au Mzumbe? Hapana hawawezi kufanana kwa maana huyu mmoja wa ECA alianza nayo tangia akili ikiwa bado haina mambo mengi.

Mbona wanaosoma PCM, HKL na HGL wanaanza na hayo masomo ya Physics, History, Language (English) pamoja na Kiswahili tangia wakiwa kidato cha kwanza? Kwanini Economics ianzie kidato cha tano na sio cha kwanza? Hivi tupo serious kweli katika kuandaa wachumi bora kwa manufaa ya baadae ya Tanzania?

Kama Kiswahili ndio lugha mama ambayo watoto wetu wanaielewa vema na ndio iliyotumika kuwafundisha masuala ya afya na mfumo mzima wa umeng'enyaji wa chakula kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba, kwanini tena mwanafunzi anayeandaliwa kuja kuwa mchumi bora asome tena biology kwa kiingereza kwa muda wa miaka 4, somo ambalo hawezi kulitumia katika kuunda combination ya kumpeleka kidato cha tano?

Hii ni nini kama sio kupoteza muda wa mtoto? Kwani kuna combination ya biology na bookkeeping? Kuna mchepuo gani wa Biology na commerec?

Wanaochukua mchepuo wa sayansi waendelee na hiyo biology yao kwa maana wanaweza kuunda combination kwa masomo mengine kama Physics na Chemistry, lakini mwanafunzi anayesoma Commerce na Bookkeeping mnamfundisha biology ya nini? Kwanini msitoe hiyo biology mkaweka Economics?

Katika masomo yoooote ya A level, ni economics pekee ndio halianzii kidato cha kwanza. Kwanini? Mfumo wetu wa elimu unahitaji mabadiliko makubwa sana kwa maana Tanzania ya 2001 sio sawa na hii ya 2021.

Maoni ya wadau;
==========
Hata mimi nakubaliana na mtoa mada ni afadhari somo la uchumi per say sio hayo yenye mlengo wa biashara liwe somo la lazima Ili kuwasidia watu wanapokuwa viongozi kufanya maamuzi sahihi ya matumizi ya rasilimali badala ya kuamua ki layman afu mwisho wa siku kila kitu kinaishia kuharibika na kupoteza rasilimali za watu.

Somo la Uchumi lime address vizuri dhana ya serikali kutoa huduma na kutoa miongozo inayojaribu kudhibiti matumizi ya hisia binafsi au matumizi mabaya ya rasilimali.kozi za welfare economics, choices and public finance, inequality, poverty and Discrimination nk nk.

Unashangaa hadi leo hii serikali haijui ifanyaje Ili kukabiliana na umaskini yaani imesalia kufanya mambo ya bora liende utadhani haina watu waliosomea Uchumi kushauri sera rafiki kulingana na mazingira.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Bora hilo wazo lakujenga na kutaka kumkomboa mwanachi..ila lile wazo la mwendazake la kusomeshana historia na uzalendo wakati watu uchumi mbovu..sijui alitaka iweje.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna baadhi ya masomo ni delicate.ndomaana hakuna diploma ya economics tz. Mi nafikiri tuwapunguzie watoto mizigo.mtoto ana masomo 9 na bado umpe na economics inakuwa mzigo sana.
Tunamuondolea biology kisha tunampa economics kwa maana masuala ya msingi ya afya aliyasoma shule ya msingi, tena kwa Kiswahili lugha mama akayaelewa vizuri mkuu.
 
Wacha waikute advance.mwisho basic knowledge ya uchumi ipo kwenye commerce.
Ndani ya somo la commerece hakuna chochote kinachohusiana na Economics mkuu. Kwa hiyo unataka kusema ndani ya physics kuna chemistry kwa sababu wanafunzi wanafanya litmus test?

Kama ndani ya commerce kuna economics kwanini combination isiwe Commerce na Accountancy peke yake?
 
Ni sahihi lakini itakua ni kuwaongezea mzigo watoto wa form 1. Umeongelea kuhusu kuitoa Biology lakini ina umuhimu wake mkuu tena mkubwa tu kuna mambo kibao primary huyasomi lakini sekondari utayasoma.

Achilia mbali hilo lakini pia mtoto wa form one unaemuondolea hiyo Biology na kumuwekea economics hajui kesho atakua nani , wengi wao akimaliza form four haijalishi alisoma masomo gani lakini akiona marks zake ni hafifu anakimbilia nursing ambako huko Biology aliyosoma o'level itambeba.

Economics ina umuhimu lakini si sahihi kutoa somo fulani kwa ajili ya hilo, labda pale kidato cha tatu wawawekee hao wa mchepuo wa biashara.
 
Achilia mbali hilo lakini pia mtoto wa form one unaemuondolea hiyo Biology na kumuwekea economics hajui kesho atakua nani , wengi wao akimaliza form four haijalishi alisoma masomo gani lakini akiona marks zake ni hafifu anakimbilia nursing ambako huko Biology aliyosoma o'level itambeba.
Mkuu, unaweza kusoma bookkeeping na commerce kisha ukaenda nursing bila kuwa na chemistry? Mimi ninaongelea wale wa mchepuo wa biashara tu.
 
Ni sahihi lakini itakua ni kuwaongezea mzigo watoto wa form 1. Umeongelea kuhusu kuitoa Biology lakini ina umuhimu wake mkuu tena mkubwa tu kuna mambo kibao primary huyasomi lakini sekondari utayasoma.
Mkuu, biology ni pana sana sana tena saaana na kuna mambo ya muhimu yapo kidato cha tano lakini form four hakuna. Mbona sio compulsory kwa wanafunzi wote wa advanced level?

Biology ya msingi ifundishwe kwa nguvu primary school kwa maana huku inatumika lugha mama ambayo ndio rahisi kwa mtoto kuelewa kuliko huko juu.
 
Economics ina umuhimu lakini si sahihi kutoa somo fulani kwa ajili ya hilo, labda pale kidato cha tatu wawawekee hao wa mchepuo wa biashara.
Hata wakianza na economics form three sio mbaya sana, lakini swali la msingi ni kwamba, kwanini mwanafunzi asome bilogy primary na secondary ilhali yeye ni mchumi mtarajiwa na hilo somo hawezi kuliundia combination A level?
 
Kwani Demand Schedule ya form one ya Commerce na ile ya kwenye Economics zipo tofauti!?
Kwani litmus test ya kwenye chemistry na food testing ya kwenye biology zipo tofauti mkuu? Ndio maana somo moja likaitwa commerce na lingine economics.
 
Hata wakianza na economics form three sio mbaya sana, lakini swali la msingi ni kwamba, kwanini mwanafunzi asome bilogy primary na secondary ilhali yeye ni mchumi mtarajiwa na hilo somo hawezi kuliundia combination A level?
Mkuu kimsingi mwanafunzi anayesoma commerce kuanzia form one mpk form four inatosha kabisa kumuandaa kusoma Economics kwasababu hayo masomo yana uhusiano mkubwa tu, ni km mwanafunzi anayesoma basic math o level zen akaja kusoma pure math advance, basic inampa msingi wa kuja kusoma pure na ndivyo ilivyo kwa commerce inampa msingi wa kusoma Economics japo commerce km commerce nayo ina mapana but mwanafunzi aliyesoma commerce o level anakuwa tayari na knowledge ya Economics at some points, pitia hapa [emoji116][emoji116]

Screenshot_20210520-201319.jpg
 
Mkuu kimsingi mwanafunzi anayesoma commerce kuanzia form one mpk form four inatosha kabisa kumuandaa kusoma Economics kwasababu hayo masomo yana uhusiano mkubwa tu, ni km mwanafunzi anayesoma basic math o level zen akaja kusoma pure math advance
Huu ni uongo mkuu kwa maana anayesoma basic o level akifika advance anasoma pure na kuachana na ile basic.

Anayesoma commerce o level ambayo nyie mnadai ni basic ya economics, akifika advance haachani na hiyo commerce ili asome economics bali anayasoma yote.

Umepata logic yangu mkuu? Kwa hiyo economics sio sehemu ya commerce.
 
Back
Top Bottom