Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ameonesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa masoko ya Manzese A na B pamoja na mazingira yasiyoridhisha ya Soko la Bombambili.
Brigedia Jenerali Abbas amesema ujenzi wa masoko ya Manzese A na B haujaanza licha ya mkandarasi kulipwa Shilingi bilioni 3 kama malipo ya awali, huku mradi huo ukipangwa kuanza Julai 15, 2025 na kukamilika Julai 12, 2026.
Amesema amebaini ujenzi haujaanza na kilichofanyika ni ujenzi wa uzio, kuchelewa kwa kazi kuna mambo yatajitokeza ikiwemo mipango ya Manispaa kutofikiwa na hivyo mapato kupungua mwakani, changamoto ya Wananchi kutopata mahitaji yao, Wafanyabiashara kufanya biashara katika mazingira mabovu.
Kutokana na hali hiyo, amemuagiza mkandarasi kuwasilisha maelezo rasmi kuhusu kuchelewa kwa mradi huo na hatua atakazochukua kuharakisha ujenzi.
Pia soma:
~ Songea: Hali ya Soko la Bombambili si salama, wakati wa mvua hali ni mbaya
~ Mkurugenzi Manispaa ya Songea akabidhi eneo la Mradi wa Ujenzi wa Soko la Sh Bilioni 22.9 - Manzese A na B
Upande wa Soko la Bombambili ameelekeza barabara zinazoingia sokoni zirekebishwe, taka ziondolewe mara moja na usimamizi wa malori uimarishwe ili kulinda miundombinu.
Amesisitiza maagizo hayo yatekelezwe ndani ya wiki moja, akionya kuwa mazingira duni wakati wa mvua yanaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa na kuhatarisha afya za Wananchi.