Hizo njia ulizozitaja zilifunga kabla huyo uliemtaja kwa sifa hajaingia madarakani
Zilifunga nini?
Dr JPM 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato alishinda na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi.
Mwaka 2000 Dkt. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.
Mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010.
Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi hadi 2015 alipogombea urais na kushinda
2015 hadi 2021 alikua Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiweka kipaumbele kwenye miundombinu ya usafiri wa barabara, majini, reli na anga
Huo ndio mchango wake kwenye sekta ya usafiri katika nchi hii
Umeelewa mtanzania mwenzangu?
Au unataka nikupe historia ya barabara za Tanzania pia kuanzia 1995 hadi alipoondoka?
Masasi Songea kulikua hakupitiki, mara ya mwisho mimi binafsi ilibidi nitoke mtwara kuja Dar ndio niende songea 2003. Hivyohivyo kwa Dar Mwanza na barabara nyingine nyingi nchini
Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote😍🇹🇿🙏
KAZI IENDELEE 👍