Songea to Mwanza: Mwamba katoa chuma na kaanzisha hii route

Hiyo route inahitaji a special luxury bus, na kwa advancement hii, tuishauri serikali iondoe matuta yote barabara kuu kama ilivyo kwa kipande cha barabara cha Dodoma Kondoa
Dodoma-Kondoa magari machache. Songea-Njombe magari machache, Njombe-Iringa magari mengi. Iringa-Dodoma magari machache. Dodoma-Mwanza magari nyomi.

Kwa hiyo, matuta ni muhimu kwa ruti hiyo dume ili kupunguza ajali za barabarani.

Njoo ofisi za TANROAD Songea zilizopo karibu na SAMCO tukupe shule kuhusu umuhimu na hasara ya matuta barabarani.

Sawa we Mndendeure wa Mkongo- Namtumbo? [emoji2][emoji2]
 
Hongera kwa kwake

Na tuendelee kumshukuru Mungu kwaajili ya uhai wa John Pombe Joseph Magufuli kwa taifa letu

Tuliowahi kusafiri Dar Songea zamani, Songea Masasi na Dar Mwanza kupitia Nairobi tunajua Shujaa metuachia miundombinu ya kututosha na katurahisishia maisha mnoooo

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote

Aendelee kupumzika kwa amani kipenzi chetu JPM😍🇹🇿🙏
Hizo njia ulizozitaja zilifunguka kabla huyo uliemtaja kwa sifa hajaingia madarakani
 
Kama ni Scania atafanya vema lakini kama ni Yotong atapotea mapema, Nasubiria wababe waanzishe Route ya Arusha-Mtwara, Arusha- Songea, Mtwara-Mwanza
Kapeleka mchina na yawezekana kuna utafiti anaufanya kwanza.

Yule ni mfanyabiashara atakuwa anafahamu japo jambo la ukweli kuna gari/basi za kichina zinakata upepo kuliko scania ila kwenye kudumu in one or two years ndiyo tatizo.
 
Kuna route ina abilia wa kutosha ila baadhi wanaiogopa sijui kwa nini, Dar to Musoma, now nadhani kuna kampuni mbili as JM Luxury na CAPRICON.
Musoma
JM
Osaka
Kapricon
Falcon
 
Hizo njia ulizozitaja zilifunga kabla huyo uliemtaja kwa sifa hajaingia madarakani

Zilifunga nini?

Dr JPM 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato alishinda na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi.

Mwaka 2000 Dkt. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.

Mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi hadi 2015 alipogombea urais na kushinda

2015 hadi 2021 alikua Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiweka kipaumbele kwenye miundombinu ya usafiri wa barabara, majini, reli na anga

Huo ndio mchango wake kwenye sekta ya usafiri katika nchi hii

Umeelewa mtanzania mwenzangu?

Au unataka nikupe historia ya barabara za Tanzania pia kuanzia 1995 hadi alipoondoka?

Masasi Songea kulikua hakupitiki, mara ya mwisho mimi binafsi ilibidi nitoke mtwara kuja Dar ndio niende songea 2003. Hivyohivyo kwa Dar Mwanza na barabara nyingine nyingi nchini

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote😍🇹🇿🙏

KAZI IENDELEE 👍
 
Kapeleka mchina na yawezekana kuna utafiti anaufanya kwanza.

Yule ni mfanyabiashara atakuwa anafahamu japo jambo la ukweli kuna gari/basi za kichina zinakata upepo kuliko scania ila kwenye kudumu in one or two years ndiyo tatizo.
Mchina Route ndefu huwa hadumu
 
Mbamba bay to dar

Mbamba bay to kyela

Songea to mwanza

Mambo ni moto
Hii route sijaielewa mbamba bay to kyela kupitia mbeya?ni kukosa usafiri wa uhakika ziwani au ni kutalii maana ukiwa mwambaoni mbamba bay kyela unaweza kuiona!
 
Nafikiri zaidi ni kuwahudumia watu wa Tukuyu japo usafiri wa ziwani pia ni changamoto maana chombo kikitoa nanga pale Ipiyana kufika mbaba bay kuchukua zaidi ya siku nzima
 
Shida kwangu ni pale ulipoingiza ushabiki na kuuacha uhalisia
Zilifunga nini?

Dr JPM 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato alishinda na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi.

Mwaka 2000 Dkt. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.

Mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi hadi 2015 alipogombea urais na kushinda

2015 hadi 2021 alikua Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiweka kipaumbele kwenye miundombinu ya usafiri wa barabara, majini, reli na anga

Huo ndio mchango wake kwenye sekta ya usafiri katika nchi hii

Umeelewa mtanzania mwenzangu?

Au unataka nikupe historia ya barabara za Tanzania pia kuanzia 1995 hadi alipoondoka?

Masasi Songea kulikua hakupitiki, mara ya mwisho mimi binafsi ilibidi nitoke mtwara kuja Dar ndio niende songea 2003. Hivyohivyo kwa Dar Mwanza na barabara nyingine nyingi nchini

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote😍🇹🇿🙏

KAZI IENDELEE 👍
 
Nafikiri zaidi ni kuwahudumia watu wa Tukuyu japo usafiri wa ziwani pia ni changamoto maana chombo kikitoa nanga pale Ipiyana kufika mbaba bay kuchukua zaidi ya siku nzima
Ipiyana=Itungi au kiwira port
 
Back
Top Bottom