PreGE2025 Songea: Viongozi watatu CHADEMA, Mwimbaji nyimbo za chama na Wanachama wawili wakamatwa na Jeshi la Polisi

PreGE2025 Songea: Viongozi watatu CHADEMA, Mwimbaji nyimbo za chama na Wanachama wawili wakamatwa na Jeshi la Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wajifunze kwa mahita sasa hivi yuko wapi,
Na miongoni mwa taasisi zinazoishi maisha ya hovyo na magumu baada ya kustaafu ni hao hao.
Mzee malechela aliwahi kusema yeye sio katapila, alijitambua. Sasa wengine sio tu makatapila bali T= Shirt
Mahita ana shida gani uzee ht we utazeeka
 
Tuna polisi hayawani kabisa, wasio na uelewa wowote, wanashindana kuwafanyia uovu CHADEMA wakiamini wakifanya hivyo, watapanda vyeo.

Yalaaniwe haya mapolisi hayawani, na vizazi vyao vyote kwani hawana faida kwa Taifa. Ni aheri haya mahayawani yasingelizaliwa.
Hayawani wazazi wako we mbwa koko, wahalifu lazima washughulikiwe, mnajificha kwenye mavazi ya chama? Mtajua hamjui intelejensia ya jeshi letu ni ya kupongezwa.
 
Nilichokimaanisha kwa mahita ni kwamba utafika wakati hizo kazi wataziacha, watakua wageni wa nani.
UKIAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO BABA
Sheria ziko wazi kwa jeshi kwamba unatakiwa kutii amri lkn iliyopo kisheria. sasa wewe baba ndio mtuhumiwa wa kosa la jinai, mke anachukuliwa wa nini? Ndio PGO mpya zinasema hivyo.
 
Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Marco Chilya alipoulizwa amesema: “Nachojua tumeshikilia waalifu si wanachama. Nitafute baada ya saa mbili nitakuwa na ufafanuzi zaidi,

Ndiyo kisingizio kikubwa cha vyombo vya dola baada ya kutumwa na chama dola kongwe tawala CCM kuonea wapinzani.

TOKA MAKTABA :


View: https://m.youtube.com/watch?v=8QDIWdDSfCY
Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Marco Chilya alipooneshwa kukerwa na No Reforms No Election akapiga marufuku isionekane wala maneno hayo kusikika mkoani Ruvuma
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Kusini kimesemea viongozi wake watatu, mwimbaji nyimbo za chama na wanachama wawili wameshikiliwa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Songea Mjini.

Taarifa ya awali iliyotolewa leo Aprili 21,2025 na CHADEMA makao makuu, imewataja viongozi hao kuwa ni Christian Komba, Mwenyekit wa Jimbo la Songea, Esau Chiza Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Songea, Zubery Tindwa Mjumbe wa Kamati Tendaji Jimbo la Songea, George Mwingira mwimbaji wa nyimbo za Chama,Abubakar Swalehe na Erick Wolfrem.

Akizungumza na Nipashe Digital, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kusini, Masoud Malimusi, amesema viongozi hao walikamatwa kwa nyakati tofauti na wapo katika Kituo cha Polisi Songea Mjini, ikiwamo wanne waliokuwa wamekutana Baa kujadili mambo yao wakiwa na sare za chama zenye maneno ya ‘No Reforms No Election”

Amesema Mwenyekiti alikamatwa baada ya mkewe na mtoto wake kuchukuliwa na polisi ambao walikwenda dukani na kukuta limefungwa kwa kuwa alikwenda kituo cha polisi kuwapelekea chakula wenzake waliokamatwa.

Malimusi amesema akiwa kituoni alipigiwa simu na mkewe ambaye alimtaka kwenda dukani na alipofika aliwakuta polisi ambao walimkamata na kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake.
George Mwingira

Amesema viongozi na wanachama hao wamepekuliwa kila mmoja nyumbani kwake na kurudishwa kituoni humo na kwamba wamejulishwa kuwa wanashitakiwa kwa sababu walikuwa wanaandaa ajenda ya kufanya maandamano kupinga kushikiliwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.

“Tulichoelekwa ni kuwa walifanya mkusanyiko usio halali, tusichoelewa hawa watu walikuwa wamekaa watatu wanaongea, sasa sijui ni kwasababu wamevaa sare za chama za ‘No Reforms No Election’ au vipi, tumeambiwa tutafute barua za kuwadhamini, na wamehojiwa asubuhi hii. Tukirudi kituoni tutajua nini kinaendelea,”amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Marco Chilya alipoulizwa amesema: “Nachojua tumeshikilia waalifu si wanachama. Nitafute baada ya saa mbili nitakuwa na ufafanuzi zaidi,”Si kila anayeshikiliwa ni mwanachama sisi tunashikilia waalifu.
Eti tumeshikilia wahalifu,pumbavu kabisa huyo askari ,watu kuvaa sare za chama ni uhalifu?
 
Christian ni jirani angu kabisa hapa Msamala Miembeni, na aliwahi kuwa mwenyekiti wa mtaa wetu kwa miaka 5, na maendeleo tuliyaona.

Toka aondoke madarakani, msamala imekua ya hovyo kabisa, uzuri wananchi wake wengi wanajiweza ndo inabeba mtaa, wananchi tunampenda had kesho. Na iliwahi sikika Ccm Wanamtaka na angepewa udiwani wa kata, ila alikataa katu katu, ni mwana chadema kindaki ndaki na anakipenda chama chake.

Naombea atoke huko polisi akiwa salama, salimini.
Aiseee sasa kama wananchi wake wengi wanampenda si ndiyo wangeenda polisi kwa uwingi wao kumsaidia?
 
Back
Top Bottom