Songea: Waumini wachoma Kanisa kwa hasira baada ya Padre kukataa kwenda kumzika muumini

Songea: Waumini wachoma Kanisa kwa hasira baada ya Padre kukataa kwenda kumzika muumini

Faida ya kuchoma Kanisa ni kubwa kuliko Kumchoma/kumwadhibu Padre au kususia kwenda Kusali!

Kanisa Katoliki Lina Changamoto ya kuwabagua Masikini huku likitoa Upendeleo kwa Matajiri kwenye shughuri za Maziko.

Sasa message sent, Paroko ataondoshwa, atakayekuja atajua kabisa nikiyakoroga, mnaweza kuchomwa nikiwa hai.....!
 
Mwaka Jana hapo hapo Songea Mjini Paroko kapewa maneno kuwa akagoma kumzika baba mdogo, akaja katekista kutoa huduma. Jioni baada ya kuzika Babu na Ndugu wakawa wameenda kupoza Koo wakakutana nae sehemu Moja nae anapoza koo, Babu ilibidi amwambie unachofanya sio sahihi usicheke hapa wakati unakuwa na visasi.
Yeah thats how they operate! Yani kanisa limeajiri chawa kwa ajili ya kupeleka maneno ya umbea wa waumini kwa mapadre, huku nilipo kuna jamaa alikua muumini mzuri tu na michango anatoa , ila alipata bahati mbaya ya kufiwa na mke wake , huku na kule akaamua kuvuta mke mpya wa kiislam , umbea ukafika kwa baba paroko, siku alipofariki kanisa halikujigusa
 
Viongozi wa Juu wa KANISA wanapaswa watoe TAMKO KALI kulaqni na kukemea kitendo hicho kilicho fanywa na waumini wa kanisa hilo ili vitendo kama hivyo visijirudie tena.
 
Hao waumini huenda wana matatizo ya akili; kosa la padre kwanini uchome kanisa. Kesho watasali wapi? Kwa hiyo kesho wachangishane tena fedha kukarabati kanisa?
'Excommunication' siyo tatizo la Padre, ni tatizo la kanisa.
 
wamekosea sana kuchoma nyumba ya ibada.
maana hiyo sio nyumba ya Padre.
Ni kosa kujichukulia sheria mkononi.
ni bora wangemtenga Padre kwa kususia kwenda kanisani badala ya kuchoma.
Kichwa cha binadamu kikishazidiwa na maswaibu hasa njaa ndio kinafanya maamuzi ya ajabu kama haya.

Sema hii inatokea kwenye nchi ya 'amani na utulivu', sasa kama waumini wanaweza kchoma kanisa lao wenyewe itakuwaje kwa lile ambao sio lao au kwa wapiga kelele za siasa na hadithi za ng'ombe kunywa lita 40 kwa siku? Tukijitafakari ni bora zaidi lakini nchi ilishakuwa ngumu tayari labda kuwazidi hata hao tunaowachekaga
 
Kondoo wamestuka, Wamegeuka kuwa mbuzi

Baphomets kabisa
download.jpeg
 
Unataka nithibitishe nini kwanza ?nikutajie jina langu , parokia nilipo na hadi jumuiya yangu, na michango ninayodaiwa ? Au we ni padre mkuu!! , Uandishi wako una reflect mtu mwenye ku support, hizo sheria za kibabe za Rc. Na kwa michango ninayodaiwa si rahisi kuzikwa na padri!! Haha , but i dont even care
Kwahiyo shida ni kutokuwa tayari kwako kuwajibika!!?

Ili uzikwe Kikatoliki kuna vigezo na masharti ya kuzingatia. Unaposhindwa it means haustahili.

Kama ambavyo wao hawakulazimishi kufuata sheria zao, na wewe usiwalazimishe wakuzike.

Kila mmoja ashinde mechi zake.
 
▪︎ Mnajua sababu zilizofanya Padri akatae kwenda kuzika?

▪︎ Mnafikiri huyu ni wa kwanza kukataliwa mazishi ya Kikristu?

▪︎ Mnafahamu sababu au vigezo vya kumkqtalia mtu mazishi?

▪︎ Je, mna uhakika mhusika alitimiza vigezo na hivyo kustahili maziko ya Kikanisa?
Ujinga huu unapaswa kukomeshwa na ndio chanzo cha kanisa kugawanjika na kuzaliwa Protestant.

Hata Dr Luther alijiondowa Vaticano kwa mambo ya kipumbavu kama haya uliyoandika wewe.

Waislamu hawana upumbavu kama huu ulioandika, anayekufa astiriwe.
 
Unataka nithibitishe nini kwanza ?nikutajie jina langu , parokia nilipo na hadi jumuiya yangu, na michango ninayodaiwa ? Au we ni padre mkuu!! , Uandishi wako una reflect mtu mwenye ku support, hizo sheria za kibabe za Rc. Na kwa michango ninayodaiwa si rahisi kuzikwa na padri!! Haha , but i dont even care
Kikubwa mkuu ishike ile amri ya mapendo.......
 
Kwahiyo shida ni kutokuwa tayari kwako kuwajibika!!?

Ili uzikwe Kikatoliki kuna vigezo na masharti ya kuzingatia. Unaposhindwa it means haustahili.

Kama ambavyo wao hawakulazimishi kufuata sheria zao, na wewe usiwalazimishe wakuzike.

Kila mmoja ashinde mechi zake.
Msingi wa Ukristo ni Biblia na siyo mawazo ya watu, tena watu wajinga kabisa.

Amri kuu aliyotuachia Kristo ni amri ya upendo.

Huwezi kufanya mambo ya kihuni kama haya kwa kisingizio chochote kile.
 
Hii taarifa nafikiri ipo nusu nusu ila pia mpaka raia kufikia walichokifanya kimechagizwa na chuki iliota kwa muda mrefu baina ya viongoz wa kiroho na watu wa kawaida.

Kuna muda baadhi ya mapadri/viongozi wa kiroho wamekuwa wakijisahau na kuonyesha madhaifu yao wazi wazi.

Kanisa lijifunze kwa tukio hili dogo ilikuendelea kuleta umoja lasivyo mambo yatakuwa magumu sana mbeleni
 
Ujinga huu unapaswa kukomeshwa na ndio chanzo cha kanisa kugawanjika na kuzaliwa Protestant.

Hata Dr Luther alijiondowa Vaticano kwa mambo ya kipumbavu kama haya uliyoandika wewe.

Waislamu hawana upumbavu kama huu ulioandika, anayekufa astiriwe.
Haulazimishwi kuwa Mkatoliki, na unaruhusiwa kuondoka muda wowote unapoona imani yako haifungamani na imani yetu.
 
Msingi wa Ukristo ni Biblia na siyo mawazo ya watu, tena watu wajinga kabisa.

Amri kuu aliyotuachia Kristo ni amri ya upendo.

Huwezi kufanya mambo ya kihuni kama haya kwa kisingizio chochote kile.
Msingi wa Ukristo ni Kristu.
 
Msingi wa Ukristo ni Biblia na siyo mawazo ya watu, tena watu wajinga kabisa.

Amri kuu aliyotuachia Kristo ni amri ya upendo.

Huwezi kufanya mambo ya kihuni kama haya kwa kisingizio chochote kile.
Marehemu alionyesha upendo?
 
Back
Top Bottom