DOKEZO Songoro, Meru kuna matukio ya Watu kutoweka kiajabu, Serikali ifanye uchunguzi

DOKEZO Songoro, Meru kuna matukio ya Watu kutoweka kiajabu, Serikali ifanye uchunguzi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Kijiji cha Songoro, Wilaya ya Meru, Mkoa wa Arusha, wameeleza wasiwasi mkubwa kufuatia kutoweka kwa wananchi wawili ambao hadi sasa hawajulikani walipo, licha ya jitihada mbalimbali za kuwatafuta.

Watu waliotoweka ni Philemoni Nasari (60) na Gamalelu Sethi Nnko (45), wote wakazi wa Kijiji cha Songoro. Kwa mujibu wa ndugu na wananchi wa eneo hilo, wawili hao walipotea tangu tarehe 6 Juni, na hadi sasa hawajapatikana wakiwa hai wala miili yao.

Inadaiwa kuwa baada ya taarifa ya kutoweka kwao kutolewa, Jeshi la Polisi katika Kituo cha Usa River lilitoa kibali kwa wananchi kufanya msako katika eneo la hifadhi wakiamini huenda wangepatikana huko. Mnamo Alhamisi, tarehe 11 Juni, wananchi waliinua msako huo ndani ya hifadhi, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwani hawakuwapata wala kuona dalili zozote za walipo.

Wananchi wa Songoro wanasema matukio ya watu kutoweka yamekuwa yakijitokeza katika eneo hilo, jambo linalozua hofu na taharuki miongoni mwa wakazi. Wanaomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kilichowapata wananchi hao na kuhakikisha wahusika, endapo wapo, wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Aidha, familia za waliopotea zipo tayari kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zaidi zitakazosaidia uchunguzi.

Wananchi wanaomba serikali na vyombo vya ulinzi na usalama kulipa uzito suala hili ili ukweli ubainike na familia za waliopotea zipate majibu kuhusu hatima ya ndugu zao.
 
Back
Top Bottom