Songwe: Baba amchoma mtoto wa miezi sita akidai amesingiziwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia mkazi wa mtaa wa Ilembo wilayani Mbozi, Mariko Kahinga kwa tuhuma za kumuunguza mtoto wake wa miezi sita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe (RPC), Janeth Magomi amesema Jeshi hilo limebaini kuwa Kahinga alimchoma mtoto huyo kwa madai kuwa sio wake huku amtuhumu mkewe kuwa alipewa mimba na mwanaume mwingine.

Kamanda Magomi amekemea kitendo hicho na kuahidi kumfikisha mtuhumiwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Awali mama wa mtoto hiyo, Patricia Mwilenga aliwaambia waandishi wa habari kuwa kabla ya tukio hilo mumewe alikuwa akitamka kauli mbaya dhidi ya mtoto akidai siyo wake.

Amesema siku ya tukio yeye alikuwa akifua nguo nje ya nyumba huku mumewe akiwa ndani na baadaye mumewe alitoka nje.

"Aliponiona aliambia amemchoma mtoto ndipo nilipoingia ndani na kumkuta mtoto akilia sana", amesema .

Amesema mtoto ameunguzwa usoni, shingoni kwenye makalio hadi mguuni.

Ofisa Muuguzi Mfawidhi msaidizi wa Hospitali ya Mkoa wa Songwe, Wilson Kasanga amekiri kumpokea mtoto huyo Januari 1, 2022 akiwa na majeraha ya kuungua na kwa sasa yupo hospitali hapo kwa matibabu zaidi.

MWANANCHI
 
Wanawake muwape watoto baba zao muache kubandikiza Wanaume watoto ambao sio damu yao kenge nyie ...

inauma sana ujue ?
 
Hii ndio shida ya baadhi ya Wanaume (kukaa na vitu rohoni) utakuta hilo jambo lilikuwa linamuumiza kitambo tu lakini kulitowa kwa hata watu wazima wamsaidie kumshauri nini cha kufanya alishindwa mwishowe ndo akajikuta anafanya maamuzi ambayo kiukweli hayana afya.

Wacha aende akapambane na mkono wa sheria.
 
Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia mkazi wa mtaa wa Ilembo wilayani Mbozi, Mariko Kahinga kwa tuhuma za kumuunguza mtoto wake wa miezi sita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe (RPC), Janeth Magomi amesema Jeshi hilo limebaini kuwa Kahinga alimchoma mtoto huyo kwa madai kuwa sio wake huku amtuhumu mkewe kuwa alipewa mimba na mwanaume mwingine.

Kamanda Magomi amekemea kitendo hicho na kuahidi kumfikisha mtuhumiwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Awali mama wa mtoto hiyo, Patricia Mwilenga aliwaambia waandishi wa habari kuwa kabla ya tukio hilo mumewe alikuwa akitamka kauli mbaya dhidi ya mtoto akidai siyo wake.

Amesema siku ya tukio yeye alikuwa akifua nguo nje ya nyumba huku mumewe akiwa ndani na baadaye mumewe alitoka nje.

"Aliponiona aliambia amemchoma mtoto ndipo nilipoingia ndani na kumkuta mtoto akilia sana", amesema .

Amesema mtoto ameunguzwa usoni, shingoni kwenye makalio hadi mguuni.

Ofisa Muuguzi Mfawidhi msaidizi wa Hospitali ya Mkoa wa Songwe, Wilson Kasanga amekiri kumpokea mtoto huyo Januari 1, 2022 akiwa na majeraha ya kuungua na kwa sasa yupo hospitali hapo kwa matibabu zaidi.

MWANANCHI
Mtoto kakosea nini kama alihisi ni mtt wa baharia angevunga huenda yeye ameshindwa tekeleza uumbaji
 
Dah,hakika inasikitisha Sana...nikivaa viatu vya huyu mama eti nenda ndani nimemchoma mtoto,uwiiiiiiiiii nahisi Mimi nitatangulia kaburini..
Na sie wadada tuache kupakazia watoto jamani,tuwape tu baba zao no matter Hali zao za kiuchumi inaleta hata ujasiri kudai matumizi ya mtoto unapojua Huyu Ni baba yake kweli.
 
Back
Top Bottom