BabaDesi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2007
- 6,122
- 4,060
Kweli! Ni Uhuni...!Kilimanjaro unapeleka single diff mbali kote huko! uhuni huo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli! Ni Uhuni...!Kilimanjaro unapeleka single diff mbali kote huko! uhuni huo
Mkuu haya mabasi wamesharudisha mchezo wakufunga engine za maloriNi kweli kabisa Aboud mabasi mabovu anayapeleka Mbeya na Tunduma!
Mara Ordinary mara Semi Luxury mbona hueleweki bwashee?Sio luxury bus wewe, kuitwa luxury ni tofauti na luxury
Njia ya Dar-mbeya-tunduma - swax hakuna luxury bus hata moja
Sio sauli, New force/Golden deer, Imani plus, tanzanite wala Hao kilimanjaro
Wote ni ordinary bus to semi luxury
Uzembe wa barabarani tusiutafutie justification mkuu!Mtu umezoea kuendesha gari dsm unakuja kumpa lawama dereva wa mkoa mnajua wanakutana na mangp jaribu hata ww kuendesha gari dar to moro utaona kama ni simple ivyo
Hiyo picha ya naona kama Kuna wahuni wameingilia hili tukio Kwa manufaa Yao binafsi, RIP marehemu woteBus la kampuni ya Kilimanjaro limepinduka asububuhi hii mkoani Songwe likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es salaam ambapo taarifa za awali zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi, taarifa kamili zitakujia hivi punde.
===================
Basi la Kampuni ya Kilimanjaro Express limepata ajali kwa kupinduka asubuhi ya leo Machi 14, 2022 Mkoani Songwe wakati likitokea Tunduma kuelekea Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali za mashuhuda waliopo eneo la tukio zinaeleza ajali hiyo imesababisha watu kadhaa kufariki na uwepo wa majeruhi.
Ofisa Mmoja wa Kilimanjaro Express amekiri kutokea kwa ajali hiyo lakini hakuwa tayari kuelezea kiundani kwa madai siyo msemaji wa kampuni. Juhudi za kumpata RPC wa Songwe, Janeth Mgomi zinaendelea ili kupata ripoti kamili.
UPDATES;
Watu wanne wamefariki papo hapo huku wengine 35 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la Kilimanjaro Express lililopindukia korongoni eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amesema ajali hiyo imetokea saa moja asubuhi baada ya dereva wa basi la Kilimanjaro Express kuwa kwenye mwendokasi na kutaka kuyapita magari mengine yaliyokuwa mbele yake.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amesema majeruhi wote 35 wanaendelea vizuri ambapo kati yao saba wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya na wengine 28 wakitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe
View attachment 2149697
View attachment 2149696
View attachment 2149698
View attachment 2149968
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Maumba alimjulia hali miongoni kwa majeruhi wa ajali ya basi kampuni ya Kilimanjaro, Yusuph Ramadhan ambaye yeye na wenzake sita walikimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyoko mkoani Mbeya. PICHA: Grace Mwakalinga, SONGWE
View attachment 2149979
Uzembe wa barabarani tusiutafutie justification mkuu!
Ndugu sibado mahakama Jpo sheria za usalama barabaran adhabu yake si kubwa hTa ukiiuwa mamiaHalafu madereva wengine wataendelea
Kuendesha magari kizembe barabarani wakijua hata likitokea la ajali hawatachukuliwa
Adhabu kali.
Eti kufutiwa leseni [emoji848][emoji848]
Futa maisha yataendelea vizuri tu pengine zaidi ya alivyokuwa dereva.
Kwani kazi ni udereva tu? Lakini anakuwa ameshaharibu maisha ya wengine halafu yeye aendelee kula maisha mema mtaani?! Hapana
Acha uongo huu!!.. Kilimanjaro njia hiyo ana Yard,petrol station na hotel kwasababu ya Gari zake za mizigo na bus!!..wewe Una ongea uongoKilimanjaro na Machame ni magari ya kisanii sana.
Yanaweza kukulaza popote!
Ruti ndefu nyingi hapa Tz hazina gari luxury kama ilivyo ruti fupi fupi za dar - Dom au Dar - Arusha Dar - Tanga.Nyanda za juu kusini aina zao za usafiri zinashangaza sana.
Kwa hiyo SUMATRA wanaruhusu magari mabovu yabebe abiria..![emoji848]Hayo mabasi mabovu mabovu sana.
Hata hilo single diff linaonekana kabisa ni mkweche.
Umeshaambiwa hakuna hiyo kitu SumatraKwa hiyo SUMATRA wanaruhusu magari mabovu yabebe abiria..![emoji848]
Hakuna Luxury bus TanzaniaNyanda za juu kusini hakuna gari luxury.
Ndio kilichosababisha waishie kwenye korongo?Kilimanjaro unapeleka single diff mbali kote huko! uhuni huo