BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Jeshi la Polisi linawashikilia watu 3 akiwemo Mchungaji Julius Mwasimba baba mzazi wa marehemu na watoto wake Elia na Emmanuel Mwansimba kufuatia kifo cha Anna Mwansimba.
Kamanda wa Polisi, Alex Mkama amesema ndugu hao walimfungia mgonjwa na kuanza maombi kwa siku 3 lakini baadaye waligundua amefariki ambapo Polisi walifika na kuchukua mwili.
Mdogo wa marehemu aliyefika kumuona dada yake hakufunguliwa mlango, alimtaarifu Mwenyekiti wa Kijiji ambaye aliagiza kuvunjwa mlango na kukuta Anna amefariki huku watuhumiwa wakiendelea na maombi.
=====================
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linawashikilia watu watatu wa familia moja kufuatia kifo cha ndugu wa wanafamilia hao, Anna Mwansimba (30) anayedaiwa kufariki wakati wakimfanyia maombi nyumbani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 16, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Alex Mkama amesema tukio hilo limetokea jana Jumanne baada ya Anna kurudi kijijini Ihowa wilayani Mbozi kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
Kamanda Mukama amesema wanaoshikiliwa ni baba mzazi wa marehemu, Julius Mwasimba (57) ambaye ni mchungaji pamoja na watoto wake, Elia Julius (24) na Emmanuel Julius (21), ambao wanadaiwa walikuwa wanamuombea kwa siku tatu.
Amesema ndugu hao walimfungia na kuanza kumuombea kwa siku tatu lakini baadaye waligundua kuwa amefariki dunia.
Kamanda Mkama amesema Jeshi hilo lilipata taarifa na kufika eneo la tukio na kuchukua mwili wa marehemu ambao ulionekana kubabuka na kuwa na mabaka maeneo ya usoni.
Akizungumza kwa simui, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihowa, David Mgogo amesema watu hao walijifungia ndani katika kipindi cha siku tatu wakimuombea mgonjwa ambaye anaishi Iyunga Mbeya ambaye alirudi nyumbani.
"Aliyegundua tukio hilo alikuwa mdogo wa marehemu ambaye anaishi Mlowo, jana alikuja kumuona dada yake ambaye alisikia ni mgonjwa, lakini alipofika nyumbani kwao alikuta mlango umefungwa huku watu wakiendelea na kelele za maombi," amesema Mgogo
Amesema baada ya kukuta mlango umefungwa na jitihada za kugonga ili afunguliwe kushindikana ndipo alipoita majirani ambao walipofika walivunja mlango.
Walipoingia ndani walikuta marehemu amelala kitandani ndipo walipopiga simu kumjulisha ofisa mtendaji wa kijiji ambaye alitoa taarifa Polisi.
Mgogo amesema baba mzazi wa marehemu ni mchungaji katika kanisa la Uinjilist lililopo kijijini hapo.
MWANANCHI