Songwe: Mchungaji akamatwa kwa kumuombea mtoto wake hadi kufariki

Dini ni ulevi wa akili..yani kwa maisha ya sasa ya matibabu ya kisasa bado watu wanaamini kuomba tu..kwani matibabu yalishindikana?

#MaendeleoHayanaChama
 
Hamna kesi hapo. Hamna sheria inayowafunga. Maana kama wagonjwa kufa majumbani kwa kukosa kupelekwa hospitali basi 50% ya masikini wangefungwa jela.

Tuwekeni sawa suala la afya kwa taifa. Huyo mgonjwa mpk anaenda kwao ujue alishashindwa matibabu mjini alienda tu kufia huko

Na ukute alifariki siku aliyofika tu na hao wachungaji walikuwa wanaangaika kumfufua ambayo ni imani yao



Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Hawa wachuna ngozi wana shida sana aisee yaani mnaacha kwenda hospitalini mtu akatibiwe mnajidai maombi sijui kitu gani , inamaana uumwe na mbu badala ya kula dawa za malaria uende kwa maombi hiyo ni akili ama upuuzi yaani kimsingi watu wanaangamia kwa kukosa maarifa , ndiomaana wanaojiita walokole nawalaani sana kwa kuwa na akili finyu.
 
Watu wangu wanangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
 
Kuna makanisa ukiombewa unachezea na makofi mchungaji anakukanyaga mgongo hujakaa sawa unapigwa kofi ya utosi
Sasa ndo wakuombee hivyo siku 3 lazma ukate moto
 
Wakiongozwa na wahuni wakina CAPO DELGADO vibesen xxx na Execute .
Kwanza hapo hakuna kosa lolote kisheria maana huyo mgonjwa aliacha kwenda hospitali huko iyunga akasafiri kama km 25 kwenda kwao.

Pengine hawakuwa na hela za matibabu wakaamua kumuombea. Imani ilikuwa pungufu au labda siku yake ilikuwa imefika ndio maana hawakufanikiwa.

Sasa waislam mkileta kejeli zitasaidia nini? Nyie kutukana ni kawaida yenu hapa jukwaani.
 
Sheria ya nyokwe!! huoni wameua mtu kabisa kwa kumfungia ndani wakati anaumwa wakiamini mambo ya kijinga.
 
Duh inasikitisha niliona hii Jana UTV maombi yakufunga Kwa SIKu tatu na mtu ni mgonjwa kwelii duhh
 
Yaani huko Songwe kuna shida si bure.
 
Wanalaumiwa tu hawa waombaji badala ya watu kuhoji mazingira ya maombi hayo.
Moja huyu dada amerudi nyumbani baada ya matibabu kushindikana huko alikokuwepo.
Pili Hospitali nyingi siku hizi huruhusu wagonjwa kurudi makwao huku wakijua mgonjwa hana tena siku za kuishi.
Tatu huduma za matibabu ni kubwa kiasi cha kufanya watanzania wengi kutokuzimudu.
Nne na linaloweza kuwa kubwa kwa wanafamilia huenda walimpenda sana ndugu yao kiasi kwamba baada ya kuona kuwa kafa hawakuanini kirahisi jambo lililopelekea wajaribu karata ya mwisho ya imani kwa kuomba Mungu wao aingilie kati .
Tusikimbile kulaumu jamani kuna watu wanapitia magumu yasiyomithilika kutamkwa.
Tupendane!!
 
Akafie Hospital muidai familia 3M?

Ndugu wameona kuumwa huku hospital hatoboi. Wametest maombi hayajajibu
 
SASA WARUHUSIWE KUENDELA NA MAOMBI YAO YA KUKUFUA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…