Songwe: Miaka 200 jela au faini Tsh Milioni 52 kwa makosa 60 ikiwemo kughushi nyaraka

Songwe: Miaka 200 jela au faini Tsh Milioni 52 kwa makosa 60 ikiwemo kughushi nyaraka

3*40=120 yrs plus 4*20=80

120+80=200

Miaka 3 makosa 40
Miaka 4 makosa 20
Hesabu iko wazi kabisa mkuu, hawa wanaosema atatumikia miaka 4 au 3 wamefanya hesabu gani? Labda watupigie hesabu ya wazi kama ulivyoonyesha hapa ili tuelewe.
 
Nadhani alishindwa tu kusema kifungo cha maisha, pia jamaa sijui alikuwa anafikiria nini kashitakiwa leo na kukubali makosa kirahisi na hukumu yake nzito 200yrs😭😭😭
Kitu ambacho kitakushangaza ni pale akili yako itakapokutuma kuwa amekiri kwa bahati mbaya, la hasha. Kwa vyovyote vile amekiri kitarajia kuhukumiwa kifungo au faini. Hivo ni suala la muda tu hiyo milioni 30 atailipa na atakuwa yuko huru
 
Mahakama za wilaya zina hukumu za ajabu sana ngoja niendelee kuwasililiza...
 
Kitu ambacho kitakushangaza ni pale akili yako itakapokutuma kuwa amekiri kwa bahati mbaya, la hasha. Kwa vyovyote vile amekiri kitarajia kuhukumiwa kifungo au faini. Hivo ni suala la muda tu hiyo milioni 30 atailipa na atakuwa yuko huru
Sio million 30 tu. Ili atoke anatakiwa kulipa million 82. (52+30)
 
Waandishi makanjanja sana siku hizi.

Vifungo vinaRun Concurrently hivyo atatumikia adhabu kubwa kuliko zote hapo hata kama amekutwa na hatia makosa 60 mfano kosa kubwa adhabu ni 5yrs hayo mengine labda ni 4 au 3 basi ataenda jela miaka 5 tu hata kama jumla ya miaka yote ni 200

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Sio million 30 tu. Ili atoke anatakiwa kulipa million 82. (52+30)
Hakimu huyo pia alimwamuru Mshtakiwa alipe faini ya Tshs.1,000,000/= au kwend jela miaka minne(4) kwa kila kosa la wizi kwa Mtumishi wa Umma ,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa ishirini(20).Pamoja na kulipa faini hizo,Mahakama ilimwamuru Mshtakiwa ajereshe katika halmashauri husika fedha alizoiba kiasi cha Tshs.30,850,000/=.Mshtakiwa alishindwa kulipa fedha.
Kuna tungo tata hapa kutoka kwa ripota
 
Majizi papa yanapeta tu kwenye mtandao hayagusiki kama Kigwa,Ila vidagaa kama hivi ndo vinanyoroshwa.Kweli duniani hamna haki!labda peponi.
 
Adhabu zinakwenda sambamba atafungwa miaka minne tu.
Hii taarifa nimesikia kwenye taarifa ya habari asubuhi. Hakimu hakutamka miaka 4 ni 200. Kesi nyingine hakimu anasema wazi adhabu zinaenda pamoja. Wewe unaaminj kosa ambalo faini yake mill. 52 kifungo chake miaka 4.Kama unakumbuka kesi yoyote ya nyuma kumbushia. Na Kama ni rahisi hivyo akina Rugemalila wagekiri makosa yao,maana kesi zote uhujumu uchumi.
 
Hakimu huyo pia alimwamuru Mshtakiwa alipe faini ya Tshs.1,000,000/= au kwend jela miaka minne(4) kwa kila kosa la wizi kwa Mtumishi wa Umma ,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa ishirini(20).Pamoja na kulipa faini hizo,Mahakama ilimwamuru Mshtakiwa ajereshe katika halmashauri husika fedha alizoiba kiasi cha Tshs.30,850,000/=.Mshtakiwa alishindwa kulipa fedha.
Kuna tungo tata hapa kutoka kwa ripota
Hapa anamaanisha hata kama atatumikia miaka hiyo au atalipa faini hiyo mill 52, hizo mill.30 lazima alipe kwani alizidraw acc. ya halmashauri. Ina maana kama hana ni kukamata mali yake hata akiwa ndani.
 
kosa alilolifanya ni kukiri [emoji23][emoji23],kesi ikaishia hapohapo hakimu akagonga nyundo miaka 200
 
Duh!miaka 200!!! umri wa kuishi binaaadamu umeshuka miaka 60, sasa miaka 200 ndio nini tena hicho? aise
Hakuna kifungo cha miaka kinachozidi miaka 30 ktk sheria za Tz labda angekuwa ameua au kubaka , unaweza kuta huyo hakai zaidi ya miaka minne jela makosa yote atatumikia kwa pamoja
 
Mahakama ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, imemhukumu Semeni Gwewa Mswima, aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mlowo kifungo cha miaka 200 jela au kulipa faini ya Mil.52, na kuamuru pia arejeshe Mil.30.8 alizoiibia halmashauri ya wilaya ya Mbozi kwa kughushi nyaraka za kutolea fedha.
PICHA%20YA%20WEBSITE.jpg

Semeni Gwewa Mswima, akipanda gari la polisi baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 200
Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 01 ya mwaka 2021, ilitolewa jana Mei 7, 2021, na TAKUKURU mkoa wa Songwe mbele ya Hakimu Mkazi wa wilaya hiyo Vitalis Changwe, ambapo mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa 60 ambayo ndani yake kuna makosa ya kutumia nyaraka za uongo pamoja na wizi kwa mtumishi wa umma.

Back
Top Bottom