Songwe: Mwendesha Bodaboda achinjwa mbele ya mke wake

Songwe: Mwendesha Bodaboda achinjwa mbele ya mke wake

0897

Member
Joined
Feb 25, 2022
Posts
39
Reaction score
92
WATU wasiofahamika wamemchinja dereva wa bodaboda Sadick Mwashambwa (24) akiwa na mkewe na mtoto wao mchanga. Mauaji hayo yalifanyika usiku wa kuamkia jana saa 11.20 usiku katika kitongoji cha Kamficheni kata ya Hasamba wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Inadaiwa kuwa wanaume wawili walikwenda nyumbani kwa Mwashambwa wakavunja mlango na kuingia hadi chumbani wakamkuta akiwa amelala na mkewe na mtoto wao mchanga, wakamkamata na kumchinja mbele ya mkewe. Mtendaji wa kata ya Hasamba, Imma Sichinga na mwenyekiti wa kitongoji cha Kamficheni, Justin Ngondo walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Ngondo alisema alipata taarifa kutoka kwa jirani wa marehemu na baada ya hapo aliwafahamisha wajumbe wa serikali ya kijiji ambao kwa pamoja walifika eneo la tukio na kujionea unyama uliofanyika.

“Mke wa marehemu ambaye kwa wakati mwingi alionekana kutokuwa sawa alitueleza kuwa wauaji wa mumewe walikuwa wanaume wawili na kwamba waliingia ndani kwa kuvunja mlango na baada ya hapo walimchinja mbele yake na kisha kutoweka bila kuchukua chochote” alisimulia Ngondo alisema alimfahamisha mtendaji wa kata, Sichinga ambae aliwataarifu polisi.
 
Wanyia wa Mbozi wakatili sana tumghoghe tumleshe? Walikua wanatumia hiyo kauli ya kuulizana wakiiba kuwa tumuache au tumuue mmoja tu akisema tumleshe ujue umepona...ukiwaona wanaongea kwa Upole utadhani watu...ukiharibikiwa na gari usiku kuanzia maeneo ya Mpemba mpaka Songwe darajani pale inabidi ulikimbie gari lako hata kama ni la mizigo wao kuua ilikua jambo la kwanza ili wachukue vitu kirahisi wameua sana watu hao jamaa na ishu ya kuchuna ngozi wao ndio wagunduzi pamoja na kile kijiji walikua wanatengeneza siraha yule Mzee alikamatwa ndio ikawa mwisho ya matukio ya kikatili huko..
 
Polisi wakiwapiga risasi washenzi kama hawa tusiwalaumu ni haki yao kufa kwa risasi, wala hawahitaji upuuzi unaitwa haki za binadamu.

Haki za binadamu ni kwawale wanaojali haki za wenzao, kama hujali haki za wenzio nawewe hustahili kupewa haki yoyote
 
Back
Top Bottom