Songwe: Mwendesha Bodaboda achinjwa mbele ya mke wake

Songwe: Mwendesha Bodaboda achinjwa mbele ya mke wake

Wanyia bhana pana kipindi ilitokea ajali kijiji kimoja hao jamaa wakataka kumuaa dereva wa ile Coaster akafanikiwa kukimbia wao wakaamua kuichoma moto gari mpya baadae wale madereva wakaweka mgomo hicho kijiji hakipo mbali na Mlowo walikua hawasimami na kituo kinachofuata ni mbali kidogo walipata tabu Kamanda wa mkoa sijui alikua Mzee Zerote Stiven nakumbuka Kijiji kilichangishwa walinunua 1HZ mpya kutoka Japan toka hapo huko wanajua haya magari ni gharama na kuyaheshimu hao jamaa nawajua vizuri sana kwa kweli...Wakumbozi..
Safi sanaaa,adhabu nzuri sana na iliwafaa,
 
WATU wasiofahamika wamemchinja dereva wa bodaboda Sadick Mwashambwa (24) akiwa na mkewe na mtoto wao mchanga. Mauaji hayo yalifanyika usiku wa kuamkia jana saa 11.20 usiku katika kitongoji cha Kamficheni kata ya Hasamba wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Inadaiwa kuwa wanaume wawili walikwenda nyumbani kwa Mwashambwa wakavunja mlango na kuingia hadi chumbani wakamkuta akiwa amelala na mkewe na mtoto wao mchanga, wakamkamata na kumchinja mbele ya mkewe. Mtendaji wa kata ya Hasamba, Imma Sichinga na mwenyekiti wa kitongoji cha Kamficheni, Justin Ngondo walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Ngondo alisema alipata taarifa kutoka kwa jirani wa marehemu na baada ya hapo aliwafahamisha wajumbe wa serikali ya kijiji ambao kwa pamoja walifika eneo la tukio na kujionea unyama uliofanyika.

“Mke wa marehemu ambaye kwa wakati mwingi alionekana kutokuwa sawa alitueleza kuwa wauaji wa mumewe walikuwa wanaume wawili na kwamba waliingia ndani kwa kuvunja mlango na baada ya hapo walimchinja mbele yake na kisha kutoweka bila kuchukua chochote” alisimulia Ngondo alisema alimfahamisha mtendaji wa kata, Sichinga ambae aliwataarifu polisi.
Ndugu zangu wa mbozi ni hatari kuriko Taliban,Kuna msemo wao mmoja ukisikia"tumreshe ...tumjege"?(naweza kuwa nakosea maandishi) Kimbia,tumuue au tumuache!?
 
Safi sanaaa,adhabu nzuri sana na iliwafaa,
Zerote Stiven namkubali sana yule Mzee ndio RPC wangu bora wa muda wote alipunguza ujambazi na mauji mbeya kwa kiasi kikubwa kwanza alikua anashinda vijiwe vya draft kama hana vyeo ataua kingi hapo na anapata taarifa sahihi kutoka wa watu wasio wema tena alikua anakuja bila ulinzi..
 
Hawana dini mtu mwenye Imani hawezi kumchinja binadamu...wapo wenye Iman iliyosimama viumbe hai tu hawawezi kuua...Mimi Mzee alitufundisha kutokuua viumbe visivyodhuru binadamu kama mijusi mpaka leo nikiona mjusi ndani namfukuzia nje hata watoto wangu washaelewa hayo maisha...
Utajuaje kama mtu ana Imani?
 
Mambo ya imani ni magumu sana! Hapo waliamini mgojwa atapona tu kwa maombi japo hata kama angeenda hospital kama alikuwa wa kufa angekufa tu
 
Back
Top Bottom