Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Hamna haja ya kuumiza kichwa kwa jambo kama hilo mpokee kama Mtoto wako na usimbague au kumnyanyasa kwa chochote, Mungu akusaidie maisha yaendelee.
 
Unaonekana umepaniki pole sana ukivaa uhusika kweli ni kitu kigumu lakin pambana nacho hamna namna

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
Sijapaniki in such lakini mawazo ya hapa na pale hayakosi. Kwanza tayari mtoto ni adolescent so ni tofauti na mtoto under five or 6,7. Handling ya adolescent si mnajua! halafu najua maswali kutoka kwa waja yatakuwepo. Huyo ni nani? alikuwa wapi? kumbe mume wako alikuwa na mtoto? maswali hayo najua yatakuwepo sana tu but nayo yatapita. Kuna siku tulikuwa mahali na huyo mtoto sasa baba yake hakumu introduce. Wale ndugu wawili tuliyokuwa nao ( ndugu upande wa mume wangu) hiyo sehemu wakaniuliza kwani huyu nani. Nikawaambia. Jamani jibu nililopata? Khaaa! eti its a big joke. Hawezi kuwa mtoto wake. Sasa mambo gani tena hayo! maneno kama hayo sio mazuri hata. Ukweli mtoto hafanani na mr labda anafanana na mama yake sijui. Mama yake mimi sijawahi muona. All in all !Kwa kuji evaluate mwenyewe mimi ni mama bora tu sina mambo ya manyanyaso. Niko tu positive. Mengine yatajiset huko mbele kwa mbele kama wadau wengi hapa ambavyo wamesema. Maisha yanaendelea na kazi lazima iendeleee!
 
Fuata ushauri huu
 
mamy acha uoga, hayo mabond sijui nn ni terminology tu. Nililetewa mtoto mkubwa tu na alyekua mume wang. Alikuwa anapata tabu mwanzoni akawa ananiita mama mdogo nikaishi nae kama mwanang nikawazoesha watoto wangu kumuita kaka.

miaka ikapita akaanza kuniita mama mwenyewe bila kuambiwa. Had nilipohama kwenda sehem nyingine walijua nna watoto wa3 yeye akiwa wa kwanza na hakuna aliyejua sio mtoto wang na sikumueleza mtu maana hayawahusu.Ninavyokwambia hapa ni miaka imepita nimeachana na baba yake lakini mtoto bado anaona mimi ni mama yake ananipigia simu kila apatapo nafasi. Na kasema mwezi wa 6 akifunga shule anaomba aje kukaa kwangu (yupo form 2 ss).

Bond inakujaga naturally bila kutengenezwa, kwa malezi niliyompa hiyo bond tuliyonayo haiwezi kufa milele. So be a mother sio mama wa kambo.
 
Relax sister interpersonal skills ni muhimu sana hutakuwa na sababu yoyote ya msingi kuhalalisha ubaya ukimtenda ndivyo sivyo,
 
Hahaha comment yangu bora kabisa
 
Nilichojifunza una roho mbaya inaonekana umepata mshituko kama vile ndio umeambiwa Leo ungekua kama sisi mama yetu wa kambo mzee alimletea watoto 6 na kila mtoto na mama yake lakn katulea vizuri tumekua na tunamtunza mpaka mzee analalamika tunampendelea bi mkubwa
 
Hii ndio perception ya watu kwa baadhi ya step mothers. Roho mbaya hiyo vipi! roho mbaya labda unayo wewe na mawazo yako negative towards wengine. Mimi nimeshaandika toka mwanzo roho mbaya sina. Na ningekuwa nayo wala asingesema anamleta mtoto.
 
As
Asante kwa ushauri na ushuhuda
 

Fungua moyo mwanamke mwenzangu......... huyo mtoto ulimjua na ulimkuta.
Mpokee kwa moyo mmoja bila kwanini kwanini na Mungu atakubariki..........

Pia hadi mume kaamua kumleta bila maelezo kwako jiangalie, utakua unapitwa na mengi kwa sababu ambazo labda huzijui
 
Maelezo kanipa na hata tarehe kanipa na sababu kanipa. Mengi ninayopitwa nayo ni yapi kwa mfano? Mimi nampokea na maandalizi nafanya. Hiyo haina tatizo.
 
Unaendeleaje? ulimaliza ile ishu ya kumpa pigo takatifu baba mtoto wako?
 
Be positive, naona kama umejiandaa na mapambano. Be positive please, kulea mtoto wa mmeo si dhambi. Narudia tena, be positive na Mungu akusaidie
 
Huyo mume anakupenda na hauoni ni vzr zaidi kuliko kukutana huko nje na mazazi mwenzie kila mara kwa kisingizio cha kutoa matumizi? Mpende tuu mtoto na bond itaform automaticaly. Kama unaweza kukaa na wafanyakazi wa ndani hata hujui walipotoka sembuse mtoto wa mume wako? ambaye ni ndugu wa damu wa wanao? Legeza moyo relaaaax and enjooooy.
 
Mengi ninayopitwa nayo ni yapi kwa mfano? Mimi nampokea na maandalizi nafanya. Hiyo haina tatizo.

Kwa maelezo yako alikuambia anataka kumpima DNA na hakukuweka wazi tangu awali kwamba atamleta umlee na hajamuweka karibu na watoto wako kivilee..... Unaijua sababu? DNA wameshapima??

Wanaume nao ni binadamu wenye utashi mkubwa...... Labda alikua anakuangalia na kukusikilizia kama unaweza kuishi nae kiroho safi au alikua anasubiri akuekue aweze kujitetea ndio amlete😂😂😂
 
Usijiite 'mama wa kambo' hii haijakaa poa sana dada yangu. Wewe ni mama sio mama wa kambo.

Binafsi nimewahi kuishi na mama wawili nyakati tofauti tofauti na love ilikuwepo kama kawaida tu, sikuwahi kutendewa ubaya na yeyote kati yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…