Mpenzi wa Yanga alipochoma jezi ya Niyonzima Uongozi wa Yanga ukalaani, maana yake ni kutokubaliana na kitendo hicho baada ya nyinyi na magazeti yote kusema kwamba Yanga imechoma jezi ya Niyonzima. Ndio ishara ya uongozi unaojitambua. Kama kweli Uongozi unaojitambua wa Simba haukuhusika na kauli za wawili hao kusajiliwa nao ila ulikaa kimya kwa sababu haukuona haja ya kukanusha, nini tafsiri ya viongozi wenu wa usajili kuongezea kauli kwamba Yanga vocha imekata na ndio adha ya kumtegemea mtu mmoja? Nini tafsiri ya yinyi kudai jukwaani humu kwamba Niyo hawezi kuweka picha ya kusainishwa Simba mpaka mkataba wake na Yanga kumalizika? Nini tafsiri ya Dalali kusema Ngoma na Niyonzima ni wachezaji anaowakubali tangu zamani na amefurahi kuwa wamesajili Simba? Basi Uongozi unaojitambua wa Simba usingejaribu angalau kumnon'goneza mzee wa watu huyo kwamba hali haiko hivyo? Si kwa sababu Uongozi wenyewe ndiyo chanzo cha habari hizo? Na kama hamkuwa kweli na imani ya dhati kwamba wawili hao wanakuja kwenu, kwa nini mnatoa povu hivi sasa kwamba eti Yanga ni vigeugeu? Kwani kusema kwamba wameshindwana na Niyonzima maana yake kwamba Niyonzima hangeruhusiwa tena kusajiliwa hata kama atarejesha majeshi nyuma? Kwani kusema Ngoma ni msumbufu ndiyo kusema hatakubaliwa tena klabuni hapo? Kwani hamjapata kusema Okwi ni msumbufu? Mbona Yanga hawajatoa povu kulaani mlipomsajili tena kama mnalotoa nyinyi dhidi ya kusajiliwa Ngoma?