Sophia Mjema ateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Anachukua nafasi ya Shaka Hamdu

Bado haijafahamika kama Hamdu Shaka atapangiwa majukumu mengine au ndio Kabwagwa jumla.

===

Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kimemteua Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema kuchukua ya Shaka Hamdu Shaka

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Mohamed Said Mohamed Dimwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar

---

Halmashauri Kuu Maalum ya CCM Taifa Leo imekutana na kufanya UTEUZI wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo,

====
1. Daniel Chongolo - Katibu Mkuu

2. Anamringi Macha - Naibu Katibu Mkuu Bara

3. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Said Mohamed Dimwa

4. Ndugu Sophia Mjema
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi

5. Dkt. Frank Haule
Katibu wa Uchumi na Fedha

6. Mbarouk Nassor Mbarouk
Mkuu wa Idara ya Kimataifa

7. Issa Haji Gavu
Idara ya Organaizeisheni

----

Makada wengine waliowahi kuwa Makatibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi soma
 
Naona wameruhusu mikutano ya siasa wanabadilisha na Katibu Mwenezi, wameona watafute mtu wa kuendana na kasi ya upinzani, waachane na mentality za kichawa..

Shaka alikuwa "mweupe" sana.
 
Anachukua nafasi ya Shaka Hamdu

Bado haijafahamika kama Hamdu Shaka atapangiwa majukumu mengine au ndio Kabwagwa jumla .
Wangapi humu tunaweza kuanzisha chama cha siasa maana naona hakuna mawzo mbadala ya kitaifa zaidi ni siasa za chumia tumbo na pia ni walewale tu wanazunguka kwenye mfumo wa wizi, undugu, ukanda, na kwambaaali ukichunguza kuna udini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…