Sophia Mjema, baada ya kuzuia upigaji Vishikwambi. Angazia na hawa HESLB waturejeshee pesa walizotukata kimakosa. Prof. Mkenda limemshinda

Sophia Mjema, baada ya kuzuia upigaji Vishikwambi. Angazia na hawa HESLB waturejeshee pesa walizotukata kimakosa. Prof. Mkenda limemshinda

TRAT

Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
73
Reaction score
160
Hawa HESLB wana tabia ya kuzidisha makato ya marejesho ya mkopo bidi unapomaliza marejesho ya mkopo kwa kuendelea kukata mishahara yetu kila mwezi, hata kwa zaidi ya miezi 3 hadi 6 inategemea ya wepesi wako wa kuwafuata kwenda kulalamika.

Baado ya hapo ukiomba kurejeshewa makato yaliyokatwa kimakosa wanakwambia subiri siku 90.

Siku zikifika ukiwafuata wanakwambia endelea kusubiri. Hiki ni kilio cha watumishi wengi sana.

Ukienda pale ofisi zao utakutana na watumishi wengi wanalalamika kwa kupigwa danadana pesa hazirejeshwi.

Ni wakati sasa Sophia Mjemawa kutolewa tamko la kukomesha upuuzi huu kwani waziri husika wa Elimu ameshindwa kutatua hili licha ya kulalamikiwa sana.
 
Hivi aliyepaswa kutoa tamko walimu wote wapewe Vishikwambi ndani ya siku 3 alipaswa kuwa waziri wa Tamisemi au CCM? Nadhani kuna mahali tumekwama.
 
Nchi hii ukiwa na cheo cha kisiasa rahisi sana kupata umaarufu wa kisiasa hasa kwenye nchi yenye mfumo mbovu kiutendaji serikalini kama Tanzania.
 
Hawa HESLB wana tabia ya kuzidisha makato ya marejesho ya mkopo bidi unapomaliza marejesho ya mkopo kwa kuendelea kukata mishahara yetu kila mwezi, hata kwa zaidi ya miezi 3 hadi 6 inategemea ya wepesi wako wa kuwafuata kwenda kulalamika.. Baado ya hapo ukiomba kurejeshewa makato yaliyokatwa kimakosa wanakwambia subiri siku 90. Siku zikifika ukiwafuata wanakwambia endelea kusubiri. Hiki ni kilio cha watumishi wengi sana. Ukienda pale ofisi zao utakutana na watumishi wengi wanalalamika kwa kupigwa danadana pesa hazirejeshwi. Ni wakati sasa Sophia Mjemawa kutolewa tamko la kukomesha upuuzi huu kwani waziri husika wa Elimu ameshindwa kutatua hili licha ya kulalamikiwa sana.
True point
 
Hivi aliyepaswa kutoa tamko walimu wote wapewe Vishikwambi ndani ya siku 3 alipaswa kuwa waziri wa Tamisemi au CCM? Nadhani kuna mahali tumekwama.
Hii nchi ina mambo ya ajabu hata ugawaji wa vyeo fikiria sofia mjema alikuwa RC amepewa uenezzi wa ccm taifa....lakini aliyekuwa mwenezi wa taifa amepewa uDC. Inamaa mwanaozni hawakuona kuwa dogo hakuwa mkomavu kushika wadhifa wa kitaifa?
 
hii nchi ina mambo ya ajabu hata ugawaji wa vyeo fikiria sofia mjema alikuwa RC amepewa uenezzi wa ccm taifa....lakini aliyekuwa mwenezi wa taifa amepewa uDC. Inamaa mwanaozni hawakuona kuwa dogo hakuwa mkomavu kushika wadhifa wa kitaifa?
Hili nalo neno.
 
Japo na mimi ni Kanda hiyo. Ukweli Loan Board imejaa Kanda pendwa awamu ya 5. Wanajisahau hii siyo awamu yetu. Hata Mimi ni mwafirika ni mwezi wa 5 tangu nijaze loan refund online system Kila nikiingia kwenye system hawajafanyia kazi yoyote madai yangu ya marejesho. Ujeuri tu ukiwapigia simu. Wakati mwingine unaombea hata Mkurugenzi HESLB Mungu ampende zaidi.
 
Tupo wengi, tupaze sauti zetu ili warudishe pesa yetu. Million 2 ni kubwa sana aiseee! Hili jambo siyo dogo, ni janga la kitaifa na waathirika wake ni wengi mno. Ukiona hadi viongozi wetu hawalikemei unaweza kudhani kuwa wao pia ni wanufaika wa hizo pesa zinazoibwa na bodi ya mikopo.
 
Hawa HESLB wana tabia ya kuzidisha makato ya marejesho ya mkopo bidi unapomaliza marejesho ya mkopo kwa kuendelea kukata mishahara yetu kila mwezi, hata kwa zaidi ya miezi 3 hadi 6 inategemea ya wepesi wako wa kuwafuata kwenda kulalamika.

Baado ya hapo ukiomba kurejeshewa makato yaliyokatwa kimakosa wanakwambia subiri siku 90.

Siku zikifika ukiwafuata wanakwambia endelea kusubiri. Hiki ni kilio cha watumishi wengi sana.

Ukienda pale ofisi zao utakutana na watumishi wengi wanalalamika kwa kupigwa danadana pesa hazirejeshwi.

Ni wakati sasa Sophia Mjemawa kutolewa tamko la kukomesha upuuzi huu kwani waziri husika wa Elimu ameshindwa kutatua hili licha ya kulalamikiwa sana.
Kwa nafasi au cheo gani alichonacho? Yeye akaitangaze ccm tu.
 
Hivi aliyepaswa kutoa tamko walimu wote wapewe Vishikwambi ndani ya siku 3 alipaswa kuwa waziri wa Tamisemi au CCM? Nadhani kuna mahali tumekwama.
Hatujielewi kwa kweli!
 
Hao board ya mikopo wana urasimu wa ajabu inawezekana hizo online refund wala hawahangaiki kuzipitia kwani hata kutuma feedback kwenye simu au email ya mtu aliyeomba kurudishiwa hela yake kwa kuwa si mnufaika wa hiyo board hakuna ofisa yeyote anayejali .Hivi mna nini lakini?Kweli mmekosa hata kifurushi cha sms ili kumjulisha anayewadai mchakato ulipofikia
 
Back
Top Bottom