Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Ukiona wenye kukijua chama wanaondoka au wanatoswa ujue chama hicho kinapoteza utambulisho wake.
 
Kama kweli Kikwete aliimba nao, basi naye hayuko salama...tusubiri. Tunakwenda kuwa kama China na Chama cha Kikomunisti cha China. Mwenyekiti ana ndoto hii.
 
Hiyo hoja ni dhaifu sana.
Mwalimu Nyerere alituambia kwamba,"Upinzani Imara utatoka CCM".Kinachoendelea ni ukamilifu wa maneno ya kinabii.
 
Alipewa ubunge wa viti maalumu kama Mwenyekiti wa UWT si Kama Sophia Simba. Hata Mwenyekiti atakaye chukua nafasi yake naye atakuwa "automatically" mbunge. Hii ni kufuata kanuni za kupata wabunge wa viti maalumu kwa CCM
 
NAFASI LAZIMA WAPEWE, LOWASA SI NDIYO MWENYE CHAMA NA MBOWE. WAKISEMA THIS WAY, NANI ATASEMA THAT WAY? THUBUTU UNAFUTWA UANACHAMA.
WATANGAZE MALI ZAO WAJE ACT CHAMA MAKINI.
 
Ubunge wake in wa kikatiba, sio wa kuteuliwa. Tumia kichwa chako vizuri
 
Naona ndugu zetu wanataka kututoa kwenye mjadala.....tunataka vyeti vya bashite
Bashite ni kama usingizi wa usiku tu, hata ulale vipi mchana usiku utalala tu hata kwa kusinzia!
 
Ni hivi unapokwenda kwenye uchaguzi wa ndani ya chama its common sense wote amuwezi kuwa wamoja kushinda lazima u mobilize support za ndani maana wanachama wenzako ndio wapiga kura wenyewe.

Kwa hivyo issue hapa sio walikuwa upande gani na uchaguzi unapoisha sio ugomvi kiasi kwamba uwezi fanya nao kazi wale waliokuwa upande mwingiene.

Swala la kuadhibiwa ni wao kukosa nidhamu mbele ua umma lazima mtu wao apite na kukejeli taratibu za chama ndio maana hata huyo Lowassa akutaka Bashe akaidi maamuzi ya chama na wala husikii kuadhibiwa leo.

Halafu binafsi sikulisema leo hili siku ile ile walipotoka nje nikasema wanastahili adhabu na hakuna aliejua kama Magufuli atakuwa raisi. Its simple mwanachama awezi kwenda kinyume na taratibu za maamuzi ya ndani hadharani ndio maana vyama vina whips ukubali utaambiwa ama popote duniani.
 
Mwisho wa vyama vikongwe ni pale vikianza timua timua hasa ya wabeba maono na wanakamati wakuu wa timu za ushindi..
Vipi wale wabeba maono wanapohamishia maono yao upande wa pili huku wakijaribu kukuaminisha wapo na wewe?? Na wewe ukawashtukia?? Je Utawaacha au??
 
Hii ni kanuni yetu sisi wavuvi,,, anayetoboa jahazi ambalo sisi wote tunasafiria anatoswa yeye baharini, hakuna namna
Tunamtosa kabla hajatoboa baada ya kubaini tu anataka atuzamishe..bora afe peke yake
 
amfate lowasa c alisema ana iman nae
Lakini kwani kuimba c ni kundi kubwa linaimba siyo mtu mmoja moja na makofi tunapopiga huwezi kuyatofautisha huyu anayefukuzwa kwa kuimba anahatia gani ? Kwani ndani ya ccm demokrasi haipo?
 
Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kutoa unabii kwamba,"Upinzani Imara utatokana na CCM".Ikiwa na maana kwamba baadhi ya wanaccm watakaoondoka CCM ndio wataweza kuunda upinzani imara utakaoitikisa CCM na kuiondoa Madarakani
Tumeona Mawaziri wakuu wastaafu wawili-Edward Goyai Lowasa na Fredrick Tluway Sumaye wakiondoka na kujiunga na Upinzani.Mwanasiasa nguli na ambaye alikuwa ndio alama ya CCM-Kingunge Ngombare Mwiru nae kakimbilia Upinzani.Orodha ya wanasiasa nguli wa CCM waliokimbilia Upinzani ni wengi mno lakini hili la jana la kuwatimua Mwenyekiti wa UWT,baadhi ya Wenyeviti wa Mikoa na Wilaya na Wajumbe waandamizi wa chama nadhani ndio linaipeleka CCM karibu kabisa na utimilifu wa Unabii.
Kama unabii huu utatimia nategemea Tanzania kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo maana hakuna chama kitakachobweteka pindi kipatapo ridhaa ya kuwatumikia wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…