Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Ukiona wenye kukijua chama wanaondoka au wanatoswa ujue chama hicho kinapoteza utambulisho wake.
 
Na tumaini wote ni wazima..

Twende moja kwa moja kwenye mada. Sote tunakumbuka maneno aliyokuwa akiyasema JPM... "Kuna wenzetu mchana CCM usiku wapinzani"

Alikuwa akiwazuumzia baadhi ya wanachama wa CCM ambao kwa namna moja au nyingine walishirikiana na wapinzani kipindi cha uchaguzi.

Sofia kama wote mnakumbuka alikuwa katika kamati iliyoundwa ya kuratibu ushindi wa mgombea urais wa CCM. Inasemekama kuna taarifa nyingi za mikakati ya ushindi zilikuwa zikivuja. Ikapelekea mikakati mingi kushindikana na ratiba kubadilishwa mara kwa mara.

Na ilifikia kipindi baadhi ya wajumbe wa kamati kupunguziwa
majukumu au kutoshirikishwa baadhi ya mambo. Na inasemekana Mama yetu alivujisha sana taarifa. Na ndio maana kwenye mikutano mingi walimtoa au kutomhusisha.

Kuimba tunaimani na Lowasa si kigezo maana hata JK naye aliimba nao.

Naipongeza CCM kwa maamuzi haya ya busara. Viva CCM
Kama kweli Kikwete aliimba nao, basi naye hayuko salama...tusubiri. Tunakwenda kuwa kama China na Chama cha Kikomunisti cha China. Mwenyekiti ana ndoto hii.
 
Hiyo hoja ni dhaifu sana.
Mwalimu Nyerere alituambia kwamba,"Upinzani Imara utatoka CCM".Kinachoendelea ni ukamilifu wa maneno ya kinabii.
 
Mkuu hivi kweli msalitiwe kias hicho na bado mumpe huyo "msaliti " ubunge viti maalum??
Like seriously?
Vip ule msemo wenu wa " sasa yamepita, umoja ni ushindi"?
Anyways, the ussue at hand still hot,and never will it be fixed......
Dhambi ya chuki, visasi na "ubaguzi" itawamaliza.....
Alipewa ubunge wa viti maalumu kama Mwenyekiti wa UWT si Kama Sophia Simba. Hata Mwenyekiti atakaye chukua nafasi yake naye atakuwa "automatically" mbunge. Hii ni kufuata kanuni za kupata wabunge wa viti maalumu kwa CCM
 
Wakuu kama mwezi nyuma nilipata kukaa na classmate wangu huyu jamaa yupo kwenye usalama wa taifa, lakini anatumika kisiasa sana(anatumiwa na ccm) kimaslahi. Alinidokeza kuwa kuna watu watatumbuliwa kwenye chama cha ccm na hao watakaotumbuliwa, watatumika kama majasusi wa kusambaratisha upinzani. Hao waliotumbuliwa watajiunga na Chadema,Nccr na Nld kusudio kuisambaratisha UKAWA. Kutokana na Cuf bwana yule anatumika hawakuona umuhimu wa kupandikiza mtu wao sababu bwana yule anatumika wamtakavyo mpaka sasa. Pia huyu rafiki yangu aliniambia ikifika 2018 ccm itawafukuza baadhi ya vijana wao watakaojifanya kwenda kinyume na chama, nao watakimbilia Chadema,Cuf,Nccr na Nld. Hao vijana watatumika kuleta nguvu lakini wengi wa watu watakao jifanya wanawaunga mkono nao pia wamepangwa kutoka ccm ili kuja kufanya hujuma kwa viongozi wa vyama vya upinzani.
Ushauri wangu kama vyama vya upinzani mtawapokea watu hao wafanyeni wanachama wa kawaida tu lakini mkiwapa nafasi za juu pole yenu.
NAFASI LAZIMA WAPEWE, LOWASA SI NDIYO MWENYE CHAMA NA MBOWE. WAKISEMA THIS WAY, NANI ATASEMA THAT WAY? THUBUTU UNAFUTWA UANACHAMA.
WATANGAZE MALI ZAO WAJE ACT CHAMA MAKINI.
 
Mkuu hivi kweli msalitiwe kias hicho na bado mumpe huyo "msaliti " ubunge viti maalum??
Like seriously?
Vip ule msemo wenu wa " sasa yamepita, umoja ni ushindi"?
Anyways, the ussue at hand still hot,and never will it be fixed......
Dhambi ya chuki, visasi na "ubaguzi" itawamaliza.....
Ubunge wake in wa kikatiba, sio wa kuteuliwa. Tumia kichwa chako vizuri
 
Naona ndugu zetu wanataka kututoa kwenye mjadala.....tunataka vyeti vya bashite
Bashite ni kama usingizi wa usiku tu, hata ulale vipi mchana usiku utalala tu hata kwa kusinzia!
 
Itakuwa una akili za hovyo kama za mwenyekiti wako kujifanya anajua kila kinachotokea duniani ili kujustify roho mbaya yake. Mtafute Nikki Haley alikuwa ana masimamo gani wakati wa movement za Trump na Trump aliposhinda imekuwaje. Trump alipingwa waziwazi kwenye harakati zake lakini aliposhinda wengine kawapa uwaziri na hajamfukuza chama hata mtu mmoja. Akili za kiafrika hata kwenye kucha hazijai. Kweli dunia ya leo unataka kila mtu akusujudie?
Ni hivi unapokwenda kwenye uchaguzi wa ndani ya chama its common sense wote amuwezi kuwa wamoja kushinda lazima u mobilize support za ndani maana wanachama wenzako ndio wapiga kura wenyewe.

Kwa hivyo issue hapa sio walikuwa upande gani na uchaguzi unapoisha sio ugomvi kiasi kwamba uwezi fanya nao kazi wale waliokuwa upande mwingiene.

Swala la kuadhibiwa ni wao kukosa nidhamu mbele ua umma lazima mtu wao apite na kukejeli taratibu za chama ndio maana hata huyo Lowassa akutaka Bashe akaidi maamuzi ya chama na wala husikii kuadhibiwa leo.

Halafu binafsi sikulisema leo hili siku ile ile walipotoka nje nikasema wanastahili adhabu na hakuna aliejua kama Magufuli atakuwa raisi. Its simple mwanachama awezi kwenda kinyume na taratibu za maamuzi ya ndani hadharani ndio maana vyama vina whips ukubali utaambiwa ama popote duniani.
 
Mwisho wa vyama vikongwe ni pale vikianza timua timua hasa ya wabeba maono na wanakamati wakuu wa timu za ushindi..
Vipi wale wabeba maono wanapohamishia maono yao upande wa pili huku wakijaribu kukuaminisha wapo na wewe?? Na wewe ukawashtukia?? Je Utawaacha au??
 
amfate lowasa c alisema ana iman nae
Lakini kwani kuimba c ni kundi kubwa linaimba siyo mtu mmoja moja na makofi tunapopiga huwezi kuyatofautisha huyu anayefukuzwa kwa kuimba anahatia gani ? Kwani ndani ya ccm demokrasi haipo?
 
Huyu bashe nae atacost chama..sio wa kuachwa
IMG_20170312_043718.jpg
 
Baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kutoa unabii kwamba,"Upinzani Imara utatokana na CCM".Ikiwa na maana kwamba baadhi ya wanaccm watakaoondoka CCM ndio wataweza kuunda upinzani imara utakaoitikisa CCM na kuiondoa Madarakani
Tumeona Mawaziri wakuu wastaafu wawili-Edward Goyai Lowasa na Fredrick Tluway Sumaye wakiondoka na kujiunga na Upinzani.Mwanasiasa nguli na ambaye alikuwa ndio alama ya CCM-Kingunge Ngombare Mwiru nae kakimbilia Upinzani.Orodha ya wanasiasa nguli wa CCM waliokimbilia Upinzani ni wengi mno lakini hili la jana la kuwatimua Mwenyekiti wa UWT,baadhi ya Wenyeviti wa Mikoa na Wilaya na Wajumbe waandamizi wa chama nadhani ndio linaipeleka CCM karibu kabisa na utimilifu wa Unabii.
Kama unabii huu utatimia nategemea Tanzania kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo maana hakuna chama kitakachobweteka pindi kipatapo ridhaa ya kuwatumikia wananchi.
 
Back
Top Bottom