Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Kwani kosa la Sofia Simba ni nini zaidi yeye afukuzwe, wengine waonywe?
 
"Ccm itauliwa na mtu kutoka ndani ya ccm" Mwl. JK Nyerere na inanikumbusha enzi za kifo cha KANU kinya na bwana MOI aliwafukuza kina KIBAKI yaliyokikuta chama sasa wote tunajua
 
Sasa sophia kasbiri hadi avuliwe alishindwa kusoma nyakati...lkn njoo tu mama haina shida!!
 
Chadema itisheni mkutano wa hadhara mumchukue Sophia....hamchelewi hata kutoa tamko....
 
Pole sana Sophia Simba kwa kupoteza Ubunge wa Viti Maalum
 
Mbona Waziri mkuu MKM alikuwa miongoni mwa watu waliosimama ukumbini na kuimba wimbo wa "Tuna imani na Lowassa"na hajafutiwa uanachama?

Ndiyo maana Taifa linakumbwa na misukosuko kila siku,kumbe hata sisi tusiomchagua tunaweza kuundiwa zengwe na kupoteza utanzania wetu,hii hatari sana.



Inawezekana aliungama kwa malaika mkuu.
 
Ccm ina haki kumwondoa au kumkubali mwanachama kupitia vikao n.k. lakini tuzingatie sana watanzania wote bila upinzani changamoto itakufa. Hata ktk biashara unahitaji upinzani ili uboreke uwe na nidhamu pia. Kwa nchi yetu kwa sasa upinzani upo dhaifu sana unachangiwa na mambo mengi. Illa ni muhimu na ni jambo zuri kwa Ccm kwa na Taifa kwa ujumla wake kuwepo na upinzani wenye nguvu ili Taifa lisonge mbele kwakutambua ufisadi ubadhirifu n.k. na pia ujue kipimo cha utawala wako. Lakini kwa upinzani huu sio jambo zuri kabisa kwa mustakbali wa nchi hii kisiasa na kiuchumi. Bado tu wachanga ktk demokrasia tunahitaji kupiga hatua. Hata kama Ccm inatawala uwepo upinzani wenye nguvu kiuchumi na katika sifa za viongozi wao pia sio kwa hali hii ya sasa ya upinzani wapo dhaifu. Ni maoni yangu tu.
 
Back
Top Bottom