Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Kile kitendo cha wao kutoka kwenye kikao cha Kamati Kuu na kujitenga na maamuzi ya kikao kwakweli walistahili adhabu kali....

Najua wangekuwa chadema wangefukuzwa siku hiyohiyo ila CCM kwakuwa inaamini katika vikao ilisubiri wakati ufipe na umefika hatua zimechukuliwa.



Ficha upumbavu wako wewe kibwenye!Mapenzi hayalazimishwi,mbona Waziri mkuu Majaliwa alikuwa ni miongoni mwa walioimba wimbo wa imani na Lowassa na hajachukuliwa hatua?Huo ni uonevu wa dhahiri kwa mama Sophia Simba.


 
Kweli nyumbu mna Akili za kuku! Hivi chadema inavyoendeshwa kibabe kuna chama kinachozidi chadema kwa ubabe!? By the way Ben Saanane yuko wapi? Chacha wangwe yuko wapi? Zitto naye alitimuliwaje!
Nyumbu ni nyinyi mnaongozwa na mtindo wa zidumu fikra za mwenyekiti.

Wewe hata akisema leo hii uolewa huwezi hata kuhoji bali utakubali tu.
 
Kila chama kina miiko yao, kama mtu akikiuka anaondolewa aende sehemu ambapo anadhani ni sahihi. Kumbukizi CDM pia iliona ZZK alikiuka miiko, tuwe na kumbukumbu
 
Hizi tabia za kuwakashfu waliokuwa viongozi ktk chama ama nchi sio nzuri sana. Ikitokea leo Rais Magufuli akakiacha chama cha CCM, naona bwana Lizaboni povu litakutoka kwa kashfa nyingi juu yake.
Tujifunze kuwapinga watu kwa hoja zenye manufaa hata kama bado ni wenzetu,sio pale wanapokuwa nje tu.
Natama utuwekee orodha unayodhani hawapaswi kuwa wanachama wala viongozi ndani ya ccm na uweke sababu kwa nini iwe hivyo.
 
Bora CCM wameamua kuvua unafiki ....wapinzani wanaibeza CCM inayojitengeneza ...watatutawala hadi labda wajukuu zetu wajielewe lakini si upinzani huu uliojaa ujanja ujanja ....
Mkuu,
Huna chama kabisa..?
 
Akija CHADEMA huyo mama SIMBA ghafla anakuwa mtakatifu, chadema wanamfutia tuhuma zote anazituhumiwa, kama mwenzake LOWASA na MAHANGA, manake huko nyuma CHADEMA mlikuwa mnahoji uhalali na upatikanaji wa PhD ya Dr mahanga, ila leo hii mahanga wamemfutia tuhuma (CHADEMA wana mamlaka kama ya mahakama), Lowasa miaka nane ya matusi, kutukanwa na kejeli kutoka CHADEMA na gazeti lao la MWANAHALISI leo hii anaonekana DHAHABU ngojea tusubirie kwa huyu mama SIMBA sijui itakuwaje.
Kwani kosa lake kubwa ni lipi? Kama ni kuongea msimamo wake wafukuzeni wooooote walioimba wana imani na lowasa,mmemuonea kwakuwa,ni mwanamke...NCHIMBI MKAMPA UBAROZI KWA SABABU MMEONA ANGEWESUMBUA AKIJA UPINZANI....
Wasimsahau Jesica Msavatavangu
 
Back
Top Bottom