Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Hili swali anaweza kutusaidia mh. Mbowe au waulizwe akina prof. Mkumbo na Mwigamba walipoamua kumuunga mkono Zitto ili awe top wa CDM kama ili kuwa kosa ama la.
Mimi nauliza ya ccm wewe unaniletea habari za chadema, kwahiyo na nyie mnawaiga chadema.
 
Well said kaka
 
chadema ni upinzani, na viongozi wake ni wanadamu, haiwezekani akosekane mtu wa kuwabeza ikiwa hata wa ccm wanabezwa, ikiwa hata rais anabezwa.

ila ni vyema tukatambua lugha za staha, na kujifunza kujua kwamba mema yapo na mabaya yapo
 
Ngoja tuone, ukujitahidi kulipa visasi jiandae siku moja wengine nao kujibu mapigo!
 
Wasaliti wa chama walikuwa wengi sana. Sauti zilizosikika ukumbini zikiimba wimbo wa kuwa na imani ya Lowassa ni nyingi kuliko waliofukuzwa. Hii ina maana kuwa tatizo bado limejichimbia humohumo ndani ya CCM
 
Nawaza kwa sauti tu
hii timua timua inacreate makundi mapya ndani chama chetu CCM
Mwenyekiti angaliwaza kwa upana zaidi kwamba yaliyopita yamepita tutazame ya mbeleni
 
Mida ya saa tano asubuhi maeneo ya CCM ofisi ndogo Lumumba mama Sophia Simba ameonekana akiingia na gari aina ya landcruiser (namba zimeifadhiwa) ambapo baada ya dakika 47 alikuja kuchukuliwa na gari aina ya Toyota Prius (namba zimeifadhiwa) ,mwandishi wetu aliotaka kumhoji alikataa kuhojiwa na akasema ataongea kwenye Press conference atakayoitisha wiki inayoaanza kesho.
 
Huyu mama nilijua hawezi bakishwa kiporo. Sasa sijui ahamie cuf
 
Tuliambiwa kuwa kua wanachama wa CCM Zanzibar walikisalitichama na kupelekea kuangushwa vibaya na CUF, mbona hatukwasikia kuchukuliwa hatua. Au kufutwa Uchaguzi na Jecha ulisafisha madhambi yao?
2. Kumbe hata CCM wanafukuzana chama hata bila ya kujitetea. Hivi wanappaswa kufuata taratibu za demokrasia ni vyama vya Upinzani tu?
3.Je tutarajie kupata Mbubge wa Msajili wa vyama Kisiasa ikionekana kuwa kumfukuza chama Mbubge bila ya kujitetea kama Lipumba aendelee na Ubunge.
4. Kumbe hata ukiwa msomi na busara kiasi gani ukishajiunga tu nao unakuwa kama wao?
 
Hata mkeo kukimfukuza au ikimuacha huwezi kutoa sababu kila mmoja ajue siri ya kumuacha IPO moyoni kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…