Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Kumbe zogo lote ilo wameshtushwa na huyu mama tu?? tukiskia wanampango wakujenga chama kuimarisha chama, kuwatoa wasaliti kwenye chama kumbe mtu 1 tu akiiyumbisha ccm??
 
Bora CCM wameamua kuvua unafiki ....wapinzani wanaibeza CCM inayojitengeneza ...watatutawala hadi labda wajukuu zetu wajielewe lakini si upinzani huu uliojaa ujanja ujanja ....
Mkuu safi sana tuko pamoja
 
Mkuu huyu jamaa ni mtu wa visasi na ana roho mbaya sana pia hajui kusamehe! Kaja kulipa kisasi baada ya karibu miaka miwili! Ogopa sana watu wenye visasi kama huyu malaika Mkuu.

Mzimu wa election ya 2015 utamfuata Mtukufu siku zote za maisha yake. Kwa nini mama Sophia Simba hakuvuliwa uanachama toka siku zile?
 
DUU MAREHEMU ALISEMA JOGOO AMEWEKA NDO KWANZA KUMEKUCHA BORA YA BASHITE ANAPUMZISHA AKILI BONDENI
 
Sofia simba karibu sana cdm ili tuzidi kuisambaratisha ccm na waendelee kufukuzana hadi abakie lizaboni tu
 
Bora CCM wameamua kuvua unafiki ....wapinzani wanaibeza CCM inayojitengeneza ...watatutawala hadi labda wajukuu zetu wajielewe lakini si upinzani huu uliojaa ujanja ujanja ....
we nawe sofia simba anakashfa gani ambayo imeliumiza taifa. kama ccm wangemtosa mkapa. chenge kikwete ndo ungecomment. unawezaje kumfukuza uanachama mtu ambaye ni innocent ukawaacha wale walioumiza watu mill 40.
 
Nchimbi mafia wao wataanzaje kumtumbua!
 
Walio Fukuzwa Uanachama wa CCM Kuanzia leo
1. Sophia Simba
2. Madabida
3. Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa
4. Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na
5. Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga Jumlisha Wanec na Wenyeviti wakutosha. CCM MPYA INAKUJA
 
Kafanya nn kakaangu jamani? Muacheni apumzike sasa loh!! Leo wanapunguzwa wasaliti tu ila vyeti vyao ni Halali.... Bro sio msaliti ila............ Teh teh teh!! Muacheni kabisa kaka angu plizzz!! Mmempiga pabaya kalia weeeee kaona bado mnaongea kasepa zake
 
Bora CCM wameamua kuvua unafiki ....wapinzani wanaibeza CCM inayojitengeneza ...watatutawala hadi labda wajukuu zetu wajielewe lakini si upinzani huu uliojaa ujanja ujanja ....
CCM ipi inayojitengeneza? Wewe toka Slaa kaweka mpira kwapani, akili zako zimekuwa clotted...umekuwa lightweight sana chief...

Kumfukuza Sophia ndiyo kujitengeneza? Ipi misingi yao ya kujitengeneza? Yaani kutotaka upinzani ndani ya chama ndiyo kujitengeneza? Chama kuwa na wanachama wa ndiyo mzee ndiko unakokuzungumzia?

Kujitengeneza gani huko ilhali bado CCM imekumbatia mafisadi? Tena mafisadi wao wengine ndiyo wenyeviti wa Bunge la Jamhuri, huku wengine wakiwa ndiyo wenyeviti wa chama! Kujitengeneza gani wakati bado inaogopa kufukua makaburi? Bado inakutumbatia mikataba iliyoitwa ni ya kisanii? Bado inakumbatia watu walituuzia ARV feki?

Yaani CCM ni wepesi mno. Washukuru tu watanzania ni watu wafu, wasiojielewa kama wanadamu. Kama wangekuwa wanajielewa, no matter how weak the opposition is, CCM haipaswi kushinda hata uongozi kwenye kijiji. Kwani CCM wamesha-prove failure. Hawana jipya! No matter what games they play, CCM kitabaki kuwa chama cha kisanii tu. AND THIS IS PROVEN.
 
Ni kweli upinzani bongo ni Janja ya nyani, CCM Ipo imara ila kuna mambo fulani ya kibabe yanatakiwa yafanyiwe kazi.
 
Back
Top Bottom