Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Lizaboni bhana... eti anauliza "wako wapi waliokuwa wanametea Nchimbi" wakati kila mmoja anafahamu Nchimbi bado anapeta!!

Yaani huyu jamaa anaipenda sana CCM lakini sijui kwanini CCM wanapenda kumpuuza!!

Kawafanyia fitina Emmanuel Nchimbi, Ali Hapi, Bernard Membe, William Lukuvi, Nape Nnauye, Rajabu Luhwavi lakini wote hao bado wanapeta na kinyume chake wametumbuliwa wengine!! Hii inaonesha kumbe hata CCM yenyewe haijui!!!
 
Hawataenda ufipa wala Buguruni....hao watabaki tu kwani washaona wakizengua zaid hata kile kidogo walicho nacho kitawaponyoka...bora wavunge tu kimya. Piga kimya mambo Haya yatapita.
NB:wasijichanganye kuitisha press conference kuchanganua au kufafanua sababu za Wazo kuvuliwa gamba, wakae kimya tu wataepusha mengine mengi.
 
High table wakati wa kumsikiliza kero za wananchi kulikuwa na mwenyeji wa ccm mkoa wa Dar na mkuu wa mkoa wa Dar kuna kila dalili ya kuwa na sura Mpya tupu
 
Fukuza wote baba,lazima waisome namba. Najua unaitaji wanachama watiifu,wasiokupinga na utakaowapeleka kama kondoo.
 
Madabida akithubutu kwenda CDM ajue kesi ya ARV's feki itapamba moto,TRA watamwangukia kama mwewe,na atanyang'anywa kiwanda cha madawa Arusha
 
Hata wewe unaweza kusaidia lizaboni kutoa jibu,wewe binafsi unaonaje usaliti uliofanywa na kina zzk na kutumbuliwa vs wasaliti wa CCM walofikuzwa Leo?mambo ya like humu hayatufai

Kumbe ujumbe wangu nilioutuma Kwako wa Kifalsafa umekuingia kisawasawa Mkuu? Safi sana.
 
Sio CHADEMA wala Sio CCM, tena afadhali huku CCM kwa sasa wanafagia fagia hakuna anaeona vizuri hasa watu wa chini wapo tu tunakoenda ndio huko huko, utamshangaa mtu wa CHADEMA pove linamtoka utadhani kwake hakuna udikteta, tena huyo Tundu Lizu nani wa kupinga wazo lake, semeni ukweli? Na Mbowe nani wa kumkosoa kwa sasa? Si umeona waliojaribu yaliyowakuta, na najua hamna uchaguzi wa Mwenyekiti tena dah...

Siasa za Tanzania ni bora wale wasio na vyama lakini hawa mashabiki uchwara ambao hata katiba za vyama vyao hawazijui ni shida... wako kusubiri nani wa kumtukana na kuongea USHILAWADU badala ya kujadili hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa hili..

CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.

Watu wa dizaini yako ndo BASHITE. Mada ya CCM umeishia kuongelea CDM.
 
Husika na Kichwa cha uzi hapo juu, unafikiri wasaliti hawa waliofungashiwa virago CCM mwisho wao / wataangukia chama gani cha siasa hasa ukizingatia kwasasa tuna vyama vingi vya siasa vyenye ushawishi mkubwa. Karibu utiririke, kejeli hazitakiwi.

Kumbuka siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.
Watamfata Mzee wao hilo linajulikana
 
Mimi sio mshabiki wa vyama lakini kwa hili naomba niseme CCM inapoelekea nitaenda kujiunga mwenyewe bila kulazimishwa!!...kama hawa watu walionekana 'taxi bubu' acha wapate walichokitafuta..
CCM keep it up n' CDM iwapo itawachukua hata mmoja kati yao ntaichukia rasmi!..Mtu mchafu hafai kama aliweza saliti alipolelewa then atashindwa nini kusaliti akija kwako!?..
 
Back
Top Bottom