Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Mbowe kama namuona vile akipiga jalamba kwa ajili ya usajili wa ghafla wa dirisha dogo.
 
Ahamie CHADEMA, shimo la uchafu na vitu vibovu

So far Chenge bado yupo CCM. Huyu amethibitika kula pesa ya Rada. Sio kuhisi. Uchafu upo CCM.

Mmesafisha ila sio kwa maadili bali kwa mambo ya kisiasa. Tunasubiri mshughulike na mafisadi wa kweli.
 
Sio CHADEMA wala Sio CCM, tena afadhali huku CCM kwa sasa wanafagia fagia hakuna anaeona vizuri hasa watu wa chini wapo tu tunakoenda ndio huko huko, utamshangaa mtu wa CHADEMA pove linamtoka utadhani kwake hakuna udikteta, tena huyo Tundu Lizu nani wa kupinga wazo lake, semeni ukweli? Na Mbowe nani wa kumkosoa kwa sasa? Si umeona waliojaribu yaliyowakuta, na najua hamna uchaguzi wa Mwenyekiti tena dah...

Siasa za Tanzania ni bora wale wasio na vyama lakini hawa mashabiki uchwara ambao hata katiba za vyama vyao hawazijui ni shida... wako kusubiri nani wa kumtukana na kuongea USHILAWADU badala ya kujadili hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa hili..

CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.
Haaaa mm sikujua mkuu,
Kumbe post inahusu chadema na siyo walofukuzwa ccm,
 
Mimi sio mshabiki wa vyama lakini kwa hili naomba niseme CCM inapoelekea nitaenda kujiunga mwenyewe bila kulazimishwa!!...kama hawa watu walionekana 'taxi bubu' acha wapate walichokitafuta..
CCM keep it up n' CDM iwapo itawachukua hata mmoja kati yao ntaichukia rasmi!..Mtu mchafu hafai kama aliweza saliti alipolelewa then atashindwa nini kusaliti akija kwako!?..


Alisaliti kivipi? Usaliti ni nini? Kuwa na maoni tofauti ni usaliti. Kupenda mtu asiyependwa na wenye madaraka ni usaliti? Mtu aliyetoka hadharani kulikosoa chama chake kwa kukiuka kanuni za uchaguzi, je ni msaliti? Yupi bora, msaliti au mnafiki? Ukiangalia kwa macho yanayoona vizuri unaona mwendelezo wa mnyukano wa kambi za uchaguzi uliopita.
 
Dah! mkuu ulikuwa umetoa makombora kabisa?

Mbona tayari nina "anti missile" ya uwezo wa kati?

Kama ungesogea kungefanyika "counter attack".

😀😀😀

Nilidhani wataka kuleta u "call me jay" maana huyu mtu file lake nalifahamu kinaga ubaga hasa ukikaribia maeneo ya pale karibia na IFM .

Ila ulivyosalimu amri ikabifi Yale madude yangu ya Intercontinental Ballistic Missile (IBM ) niliyarudishe kama nungu nungu afanyavyo.
 
Hapa mimi naona double standards tuu, au utakuwa mfumo dume umetumika hapa.

Kosa la Sophia ni sawa na Nchimbi na Kimbisa kwanini hukumu zitofautiane?!
 
Wakienda Chadema ni mtaji tosha. Kama walimpoke wema basi hawa ni watakatifu ndani ya chadema

Kama alivyo Chenge ndani ya CCM. Huyo jamaa ndio kipimo cha uwezo wa CCM kujisafisha. Nje ya hapo ni uozo tu. Hao popote watakapoenda haiwahusu maana si mshawafukuza?

CCM huwa kuna roho fulani ya kisasi cheusi kabisa mmeambukizana. Kwamba mkifukuza mwanachama basi mnataka afe kabisa kisiasa. Guys, hii ni karne ya 21.
 
Ningeelewa kama wangedil na wale wanaofuja mali za umma ambao ndo wamejazana CCM.. Hii ya kuwavua uanachama wenye mawazo tofauti ni udicteta na chuki. Huku sio kujenga chama ni KUTISHIA WANACHAMA WASITHUBUTU KUMPINGA MGOMBEA
DJ wa ufipa kuna wakumpinga mawazo yake au huo udikteta ni sehemu moja tu unaonekana?...
Acha tuwapongeze kwa walichofanya ni maamuzi mazuri pia!.
 
Duh! E bhana eh! Leo silali walahi.
Hii sinema si ya kawaida. Nina kopo la popcorn na soda za kutosha za Cocacola bashite.

Magu lete mambo.
 
Zito hakuwa msaliti
kilicho mponza ztt ni Kuwa mkweli
ndani ya cdm nimarufuku kuwa mkweli
hupaswi kuhoji wala kuuliza Pesa ya chama inakwenda wapi,
marufuku kuonyesha kugombea Uenyekiti
mwenyekiti wa milele ni Mbowe pekee

Simba alipokua mkweli kuwa anamtaka Lowassa ndipo akaitwa msaliti. Hayo ya Zitto unabuni. Hakuna ushahidi. Hili la Simba ni wazi.

CCM huwa haikubali ukweli kamwe. Nyie ndo mna kauli zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Jamani tutashangaa kama waliotimuliwa ccm watakimbilia chadema na kupokelewa. Hapo tutaendlea kutambua kuwa chadema ni Chama cha kupokea mabaki.

Mbona mnajiumiza sana roho. Yani umtaliki mke halafu umuamulie wa kumuoa na kuanza kumuonea wivu?
 
Back
Top Bottom