Wakuu kama mwezi nyuma nilipata kukaa na classmate wangu huyu jamaa yupo kwenye usalama wa taifa, lakini anatumika kisiasa sana(anatumiwa na ccm) kimaslahi. Alinidokeza kuwa kuna watu watatumbuliwa kwenye chama cha ccm na hao watakaotumbuliwa, watatumika kama majasusi wa kusambaratisha upinzani. Hao waliotumbuliwa watajiunga na Chadema,Nccr na Nld kusudio kuisambaratisha UKAWA. Kutokana na Cuf bwana yule anatumika hawakuona umuhimu wa kupandikiza mtu wao sababu bwana yule anatumika wamtakavyo mpaka sasa. Pia huyu rafiki yangu aliniambia ikifika 2018 ccm itawafukuza baadhi ya vijana wao watakaojifanya kwenda kinyume na chama, nao watakimbilia Chadema,Cuf,Nccr na Nld. Hao vijana watatumika kuleta nguvu lakini wengi wa watu watakao jifanya wanawaunga mkono nao pia wamepangwa kutoka ccm ili kuja kufanya hujuma kwa viongozi wa vyama vya upinzani.
Ushauri wangu kama vyama vya upinzani mtawapokea watu hao wafanyeni wanachama wa kawaida tu lakini mkiwapa nafasi za juu pole yenu.