Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Wakuu kama mwezi nyuma nilipata kukaa na classmate wangu huyu jamaa yupo kwenye usalama wa taifa, lakini anatumika kisiasa sana(anatumiwa na ccm) kimaslahi. Alinidokeza kuwa kuna watu watatumbuliwa kwenye chama cha ccm na hao watakaotumbuliwa, watatumika kama majasusi wa kusambaratisha upinzani. Hao waliotumbuliwa watajiunga na Chadema,Nccr na Nld kusudio kuisambaratisha UKAWA. Kutokana na Cuf bwana yule anatumika hawakuona umuhimu wa kupandikiza mtu wao sababu bwana yule anatumika wamtakavyo mpaka sasa. Pia huyu rafiki yangu aliniambia ikifika 2018 ccm itawafukuza baadhi ya vijana wao watakaojifanya kwenda kinyume na chama, nao watakimbilia Chadema,Cuf,Nccr na Nld. Hao vijana watatumika kuleta nguvu lakini wengi wa watu watakao jifanya wanawaunga mkono nao pia wamepangwa kutoka ccm ili kuja kufanya hujuma kwa viongozi wa vyama vya upinzani.
Ushauri wangu kama vyama vya upinzani mtawapokea watu hao wafanyeni wanachama wa kawaida tu lakini mkiwapa nafasi za juu pole yenu.
Acha kulialia. Umeona ujio wao utawanyima fursa nyie novice, hiyo ndo hali halisi, Sofia atapata ujumbe wa kamati kuu ya chadema ilhali nyie akina wema sepetu mtabaki kutumika tu majukwaani na kwenye maandamao tu.
 
Hili sakata la wanachama wa CCM waliopewa adhabu mbalimbali na kufukuzwa mbona halielezi sababu? Je hao wanachama walipewa nafasi za kujieleza na kujitetea kwa tuhuma zao? Au wamefukuzwa na kuadhibiwa kwa kuwa na fikra tofauti ambazo hazikubaliki na mwenyekiti wao. Mpaka sasa inaonekana taarifa za kuadhibiwa tu bila kuelezwa walifanya nini mpaka uamuzi huo ukakafikiwa. Mimi nilifikiri CCM wana uwazi lakini kumbe sivyo hivyo hii kweli ni demokrasia nzuri.
 
Ccm haitetereki hata kidogo
Sufuria imegandia mauchafu usikwangue ukapikia ikiwa safi upikie hivyohivyo chafu kuliza itatoboka haiwezekani lazima isafishwe ndio ikae tena jikoni
Ok
 
Na tumaini wote ni wazima..

Twende moja kwa moja kwenye mada. Sote tunakumbuka maneno aliyokuwa akiyasema JPM... "Kuna wenzetu mchana CCM usiku wapinzani"

Alikuwa akiwazuumzia baadhi ya wanachama wa CCM ambao kwa namna moja au nyingine walishirikiana na wapinzani kipindi cha uchaguzi.

Sofia kama wote mnakumbuka alikuwa katika kamati iliyoundwa ya kuratibu ushindi wa mgombea urais wa CCM. Inasemekama kuna taarifa nyingi za mikakati ya ushindi zilikuwa zikivuja. Ikapelekea mikakati mingi kushindikana na ratiba kubadilishwa mara kwa mara.

Na ilifikia kipindi baadhi ya wajumbe wa kamati kupunguziwa
majukumu au kutoshirikishwa baadhi ya mambo. Na inasemekana Mama yetu alivujisha sana taarifa. Na ndio maana kwenye mikutano mingi walimtoa au kutomhusisha.

Kuimba tunaimani na Lowasa si kigezo maana hata JK naye aliimba nao.

Naipongeza CCM kwa maamuzi haya ya busara. Viva CCM
 
Duuuu ccm imeshikwa na watindiga sasa tooba jaman mmmhh... Kazi ipo.....miungu watu... Cjuw nani amewaongopea hawa... [emoji95] [emoji95] [emoji95]
 
Hili sakata la wanachama wa CCM waliopewa adhabu mbalimbali na kufukuzwa mbona halielezi sababu? Je hao wanachama walipewa nafasi za kujieleza na kujitetea kwa tuhuma zao? Au wamefukuzwa na kuudhibiwa kwa kuwa na fikra tofauti ambazo hazikubaliki na mwenyekiti wao. Mpaka sasa inaonekana taarifa za kuadhibiwa tu bila kuelezwa walifanya nini mpaka uamuzi huo ukakafikiwa. Mimi nilifikiri CCM wana uwazi lakini kumbe sivyo hivyo hii kweli ni demokrasia nzuri.
Mkuu uwazi na ukweli "uko" TBC. Ndani ya vyama tanzania hakuna uwazi na ukweli na haijalishi ni chama gani. Kila chama kina wababe wake na wanachama wavumilivu. Umesikia leo Polepole akisema "Kikao kwa sauti moja............"
 
Wewe umenena vyema mkuu ijapo baadhi yetu humu tunajifanya kutetea huu uozo. Usaliti usikie tu kwa wengine, hakuna kitu kinaumiza kama kusalitiwa hata kama ni mwanao maamuzi magumu ni lazima yampate na hata kama ni urithi kuna sehemu itapunguzwa tu
 
Leta kopi harisi ya madai yako ama uweke picha ya maongezi yenu
 
Mkuu binafsi kwanza sikutaka kumuamini huyu rafiki yangu mpaka yalipotokea ndio nimemuamini. Kuna baadhi ya mambo huwezi kuyasema kabla ya tukio
hembu ishia zako wewe pascal mayalla alitamka wazi mapema kabla hata ya 2015 kuwa magufuli ndio atateuliwa na ccm na imekua sembuse wewe na hako kahabari kako ka ujasusi hamna kitu hapo,ngoja nikwambie hata lowassa alivokua anahamia chadema walisema hivyohivyo so hamna tofauti hapo hii sio habari tena rudi kalale uote vizuri
 
Kila lenye mwanzo halikosi mwisho, na mtu mwenye hekima hukubali kukosolewa pale anapokuwa kakosea, bali mpumbavu hung'ang'ania upumbavu wake.
Waingereza wana msemo, "The wise eases, but the fool maintains his folly ".
Mambo yote yanayoendelea dhidi ya chama dola ni mwenye hekima pekee ndo anaweza kuona kuwa ccm ipo mahututi tayari na ipo chumba cha ICU inapumulia oxygen.
Kila jambo baya linapoitokea ccm, makada waliokunywa maji ya bendera wanadai chama bado kipo imara.
1.Lowassa =out
2.Kingunge=out
3.Sumaye=out
4.Masha=out
5.Sophia Simba =out
Wema akiwa bado ccm alikuwa ni binti safi kabisa kwao, baada ya kuondoka tu eti ni "Malaya ".
Wasioona hali inayoendelea ndani ya ccm ni wa kuonea huruma Sana.
Taarifa za uhakika nilizonazo ni kuwa, Kwa JF pekee, ccm imeajiri zaidi ya vijana 30 maalumu Kwa Sababu za propaganda.
Ndugu zangu wana ccm nataka mjue kuwa kizuri chajiuza na Kibaya chajitembeza Kama mnavyoshinda humu mitandaoni kupiga propaganda, mnajitembeza, imefikia hatua hata kinyesi hamtaki kusema ni kinyesi, mnasema ni keki.
Hadi kufikia 2020,hakutakuwa na ccm tena, bali ni police na vyombo vingine vya dola.
Dalili Zipo wazi, nyie mnajitengenea Kaburi wenyewe mkidhani kuwa mna hati miliki na Tanzania, poleni Sana, ugomvi wenu ndo furaha kwetu.
 
Wewe umenena vyema mkuu ijapo baadhi yetu humu tunajifanya kutetea huu uozo. Usaliti usikie tu kwa wengine, hakuna kitu kinaumiza kama kusalitiwa hata kama ni mwanao maamuzi magumu ni lazima yampate na hata kama ni urithi kuna sehemu itapunguzwa tu
Mkuu hata wale wanaosema sema humu siyo kwamba hawajui machungu ya usaliti, wanayajua ila tu kumbuka imesemwa "adui wa adui yako ni rafiki yako"
 
Walijitakia CCM isingetoa mfano kwa matendo waliyofanya ndio ingekuwa jambo la kushangaza; hakuna chama cha siasa duniani kingeweza vumilia ukosefu wa nidhamu kiasi kile.
 
Ccm haina haja ya kufanya upuuzi huo inadola kubwa na mbinu nyingi huo utoto tupa kule
 
Back
Top Bottom