Spaghetti ya leo fupi!

Spaghetti ya leo fupi!

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,328
Reaction score
23,909
SPAGHETTI ya leo fupi!

200px-Spaghettata.JPG

2000

Kusema kweli nadhani mwaka huu wa 2000 ndiyo kumbukumbu yangu ya kwanza ya interaction yangu na chakula hichi. KWa muda mwingi nyumbani wakati tunakua tulikuwa tumezoea kufanyiwa kila kitu na wadada wasaidizi wa kazi nyumbani.

Nakumbuka tulikuwa tukitoka shule tunaanza kuvulia nguo mlangoni mpaka unafika chumbani umebaki na chupi tu..well, kwa siku ulizokumbuka kuivaa au kama asubuhi dada alikuvalisha nguo.
Hali hii iliendelea hadi tulipofika darasa la sita.

Siku moja baba aliamka tu na kuwaambia wale dada wajiandae warudi kwao. Nilijua dunia itafikia mwisho. Baba alidhani tungeishije sasa? Kazi zote zile nani atazifanya? Kwa hakika sio sisi, kwani tusiende mbali, usafi tu wa miili yetu tu ulikuwa a big challenge kwetu.

Maisha yalianza kuwa magumu kwani mimi na kaka yangu ilitubidi kuamka mapema na kuandaa chai na maji ya baba ya kuoga. Wakati mmoja akiandaa chai mwingine alikuwa zizini kutoa mfori/samadi kwa ngombe na kukamua kisha kuwalisha ngombe pamoja na kuku.

Hapo tulikuwa darasa la sita. Hivyo basi yote hayo yafanyike na bado ukatafute kuni uwahi kushika namba shule la sivyo imekula kwako.

Ratiba ya chakula ilikuwa tu na vyakula common kama makande, wali maharage, wali nyama, ugali maziwa au na mboga nyingine tu, chapatti na pilau. Kwa kweli hivi ndivyo tulivyokuwa tumevizoea.

2000

Nakumbuka niliporudi nyumbani likizo ndipo nikakutana na hii menu item mpya nyumbani..spaghetti!
Mama alitufundisha kidogo jinsi zinavyopikwa. Upishi wake kwa kweli ni mrahisi tu. Chemsha maji yenye mafuta na chumvi kasha tia spaghetti zako ndani. Njia ya kujua kama zimeiva ni kuitoa moja na kuirusha ukutani na ikinata tu unajua zimeiva..hivyo unaziepua na kuziweka kwenye colander. Kwa njia hii tulifanikiwa sana kuuchafua ukuta wa jikoni.

Kipindi kile tulikuwa wachache nyumbani tulikuwa tukipika pakiti moja. Kuna nyakati ilitubidi kurudi jikoni kwani hazikutosha na nyakati nyingine hata zilibaki. Katika mafunzo yale mama hakuwahi kutufundisha kipimo cha spaghetti kama alivyokuwa akifanya kwa makande au wali.

Baadaye yakaja macaroni na variety zake na zote hizi hatukuwahi kuambiwa vipimo vyake.
Wageni wakazidi nyumbani, nakumbuka kuna kipindi tulinunua hadi pakiti tatu za spaghetti kwa ajili ya mlo mmoja tu. Hata kipindi hicho hatukujua vipimo vya mapishi ya spaghetti kwa idadi specific ya wageni.

Katika pitapita mjini nikajafundishwa mapishi ya kipemba ya spaghetti. Yaani kuzikaanga kabla ya kutia maji au kutengeneza zile za futari..zenye sukari. Hata huyu binti wa kipemba aliyenifunza hakuweza kunieleza kipimo maalum cha mapishi ya spaghetti. Ilikuwa zaidi kama mchezo wa kubahatisha.

Sasa ninaishi mwenyewe nashindwa kabisa kupima kipimo kinachoeleweka cha spaghetti. Kuna siku zinazidi na siku nyingine zinapungua naishia kushushia kwa maji ili shibe itimie.

NI KIPI KIPIMO SAHIHI CHA SPAGHETTI?

Wasalaam wapendwa,
Mentor.
 
Last edited by a moderator:
Kama uko peke yako ile pakti unaweza ukaipika mara nne, so ukiinunua gawanya into 4 equal parts then pika but hiyo pia inategemea na appetite yako ya kula, zaweza kuwa nyingi kama si mlaji utagawa mara 6 au 5 otherwise kwa mwanume mweye kula na kuskia tumbo limetanuka basi 4 equal parts in a pakti ni kipimo kizuri.
Try that.
 
Kakangu mdogo, tatizo tulikudekeza sana.
Kuna spagheti flani zimeandikwa 'instant noodles' zinapatikana supermarket. Hebu zicheki na ni portion ya mtu mmoja tu. Uzuri wake zinakuwa na flavour kapakti kadogoo. Ukichemsha tu unachuja maji unatia flavour kitu mwake.

As of kipimo hata mie huwa nabahatisha tu. Na utamu ukizidi wengine hupikiwa supplimentary juu ya uroho. Ila kuwaweza nahakikisha wanapata matango ya kutosha kwenye sahani.
 
Mentor hapa umenipa mtihani
nitadesea kwa wenzangu naona mida hii bado wapo njiani kwenye foleni.
 
Last edited by a moderator:
Mimi sijatajwa so naipotezea kama kawa!!!!!

Lakini hapana ngoja nikupe shule kidogo mnake mitoto ya kitaa ni mafundi wa kila kitu alaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!! Usiulize fani yangu manake huwezi kunielewa ila kwenye kuoroga mwiko jikoni naweza sema naongoza hahahhahahah!!!!!!!!!!!!

Ukitaka upike mlo wowote ushibe ni lazima uweke uwe mlo kamili ( sio kila siku ugali harage utatoka kinoli oohooo!!!!) ........Namna ya kufanya gawanya mfuko wako mara 3 hapa nimeasssume kwamba ni mwanaume wa shoka ( siyo kiepe yai kama akina anti fudenge)......... kisha pika kama kawaida unavyojua. Hakikisha una mboga ambayo hata kama ni nyama basi vegs ni compolsory as u know 'eths ni highly starched food so you shld avoid pellagra by supplimenting proteins and vits pia eka na tunda lolote la msimu ama juice natural. Kwa kufanya hivyo lazima utashiba tu and am telling you na kinolis utabaki kuwa flat with energetic body lolz!!!
 
hahahaaa mie kwenye masuala ya usafi na kuchota maji hunitoi round ila sasa kwenye mapishi mmmmmhh sifuri kabisa ila nikikamatika, napika. Ndio tatizo la wazazi kurundika mahausigeli nyumbani na kuwakataza watoto wasifanye chochote, nilipika wali nikiwa form two, ndio chakula changu cha kwanza kupika ambapo nilirudi shule, nikafika home hakuna mtu na baadae natakiwa nirudi shule tena (boarding) nikaamua kuingia jikoni, mpaka leo naweza kupika ugali na mboga ya mayai pengine na samaki, nikipika nyama hua haziivi, sijajua tatizo ni nini hadi leo...naumizwa sana na hali hii
 
Mentor Kiasi cha kupima kwa mlo mmoja inategemea sana na ulaji wako maana tunatofautiana wingi wa kula. Ila tip moja ninayoweza kukupa ni kuwa Kuchemsha maji kwanza ni sahihi ila unaweka maji ya kutosha ili hata zikiiva maji yasiwe yamekauka. Then ukimimina Tambi unachemsha kwa Dk 10 tu! Unaziepua unazichuja na unaweza kuendelea na mapishi mengine. Usisahau kuweka chumvi kabla kama unatumia chumvi. Mapishi mengine ni zikishaiva ndo unaednelea nayo. Ni chakula rahisi na cha haraka sana.

Mimi hupendelea kuchemsha na Mayai ya kienyeji ambayo kwa wastani nikishayaosha nayaweka kwenye maji hayohayo yaliyochemka kwa dk 3-5 (inategemea unapenda liive kiasi gani, dk zisizozidi 5 ni la afya) ikimaanisha utalitoa kabla ya tambi.

Ukiwa umeshakatakata vitunguu, carrots, hoho n.k. (nyanya si lazima) unavikaanga kwa moto wa wastani vikiiva unaweka tambi zilizokwisha chemshwa ndani unakoroga then unaweka mayai yaliyochemshwa. Weka maji kidogo sana ambayo ni rahisi kukaukia unapokoroga lengo ni kuzuia visishike chini. unakoroga kwa dk chache huna haja ya kufunika kwani muda mfupi wa kama dk 5-10 hivi vitakuwa tayari kuliwa. Kumla ya mapishi ya chakula hiki hauzidi dk 25! Pia huwa napenda kuweka juu nikishapakua supergate badala ya tomato source source ambayo hupatikana madukani.

Nikipata muda nitazungumzia Tambi za nyama ya Kusaga.
 
kwakweli afadhali umenikumbuka maana sijui nina gundu huwa sitajwi kabisa
turudi kwenye hizo tambi kama wanavyoziita waswahili inategemea shibe yako ikoje ila ukigawa mara tatu kwa mwanaume imekaa sawa,unaweza kuchemsha nzima kama wachina na waitaliano au ukazivunjavunja zikawa ndogo.chemsha hadi zilegee usiache zikawa uji utjikuta unakula uji wa ngano bila kupenda.zikishalegea unaweza tia chumvi kidogo ziwe na ladha. binafsi huwa nakaanga rosti langu pembeni la nyanya kitunguu hoho karoti na unaweka spice yoyote unayopenda then namix tambi zangu kwenye huo mchamganyiko wageuza kidogo kitu mwake. pia rosti hilo laweza kuwa la nyama ya kusaga au ya kawaida. pia unaweza kuchemsha spagghet pembeni ukala na rosti pembeni inalipa pia
hope nimekusaidia Mentor
 
Last edited by a moderator:
Lakini best spaghetti na noodles ni kitu mbili tofauti...

Kuna spagheti flani zimeandikwa 'instant noodles' zinapatikana supermarket. Hebu zicheki na ni portion ya mtu mmoja tu. Uzuri wake zinakuwa na flavour kapakti kadogoo. Ukichemsha tu unachuja maji unatia flavour kitu mwake.
 
Mentor
Binafsi enzi hizo nikiwa college nilikuwa nikila sana hiki chakula, lakini mara nyingi sikuwa nakila pekee kama mlo unaojitegemea.
Wakati ambao nilikuwa nikihitaji kula spaghetti alone, basi aina ya upishi ilikuwa tofauti kidogo na hii iliyozoeleka ya kuchemsha kwa mafuta na sukari/chumvi.

Nilikuwa natengeneza "Cheese Spaghetti" ambayo kwa muonekano ni kama hiyo picha hapo chini...

Utengenezaji wake wafanana sana na utengenezaji wa topping ya pizza, kimsingi haupo complicated...

Unachohitaji ni peeled cheese, nyama ya kusaga au iliyokatwa vipande vidogo au hata sausage, spaghetti, spices (binafsi ni mpenzi wa Indian spices au Thai),nyanya ya kopo, pilipili(kama ni mpenzi ila unaweza tumia hata hoho),mafuta na jiko la oven.

3431558249_70c39f2594.jpg
 
Kama uko peke yako ile pakti unaweza ukaipika mara nne, so ukiinunua gawanya into 4 equal parts then pika but hiyo pia inategemea na appetite yako ya kula, zaweza kuwa nyingi kama si mlaji utagawa mara 6 au 5 otherwise kwa mwanume mweye kula na kuskia tumbo limetanuka basi 4 equal parts in a pakti ni kipimo kizuri.
Try that.
Mwanamazoezi mwenzangu nawe umeingizwa mkenge na huyu chalii angu Mentor? Hahahahaha unadhani hapa anazungumzia spaghetti kama spaghetti?

Huyu kijana usipomsoma vizuri na kuunganisha dots unaweza ingia mkenge kirahisi kama ulivyoingia wewe.

BTW leo ni ijumaa, zoezi linaanzia wapi na saa ngapi? Mwenzio nimekuja na traksuti na raba mtoni tayari kwa kazi.
 
Last edited by a moderator:
Mentor Kiasi cha kupima kwa mlo mmoja inategemea sana na ulaji wako maana tunatofautiana wingi wa kula. Ila tip moja ninayoweza kukupa ni kuwa Kuchemsha maji kwanza ni sahihi ila unaweka maji ya kutosha ili hata zikiiva maji yasiwe yamekauka. Then ukimimina Tambi unachemsha kwa Dk 10 tu! Unaziepua unazichuja na unaweza kuendelea na mapishi mengine. Usisahau kuweka chumvi kabla kama unatumia chumvi. Mapishi mengine ni zikishaiva ndo unaednelea nayo. Ni chakula rahisi na cha haraka sana.

Mimi hupendelea kuchemsha na Mayai ya kienyeji ambayo kwa wastani nikishayaosha nayaweka kwenye maji hayohayo yaliyochemka kwa dk 3-5 (inategemea unapenda liive kiasi gani, dk zisizozidi 5 ni la afya) ikimaanisha utalitoa kabla ya tambi.

Ukiwa umeshakatakata vitunguu, carrots, hoho n.k. (nyanya si lazima) unavikaanga kwa moto wa wastani vikiiva unaweka tambi zilizokwisha chemshwa ndani unakoroga then unaweka mayai yaliyochemshwa. Weka maji kidogo sana ambayo ni rahisi kukaukia unapokoroga lengo ni kuzuia visishike chini. unakoroga kwa dk chache huna haja ya kufunika kwani muda mfupi wa kama dk 5-10 hivi vitakuwa tayari kuliwa. Kumla ya mapishi ya chakula hiki hauzidi dk 25! Pia huwa napenda kuweka juu nikishapakua supergate badala ya tomato source source ambayo hupatikana madukani.

Nikipata muda nitazungumzia Tambi za nyama ya Kusaga.

Duuh..!!!maisha ya ubachelor kazi sana...!!!nlikua naumiza kichwa leo ntakula nn...!!!Asante sana aisee hapa ni kudesaa tu...!!!!:mwaaah::mwaaah::mwaaah:
 
Mwanamazoezi mwenzangu nawe umeingizwa mkenge na huyu chalii angu Mentor? Hahahahaha unadhani hapa anazungumzia spaghetti kama spaghetti?

Huyu kijana usipomsoma vizuri na kuunganisha dots unaweza ingia mkenge kirahisi kama ulivyoingia wewe.

BTW leo ni ijumaa, zoezi linaanzia wapi na saa ngapi? Mwenzio nimekuja na traksuti na raba mtoni tayari kwa kazi.

Kweli kaniingiza kingi hebu nistue maana kama hakuwa anamaanisha spageti kweli anayake mambo anazidi kuongeza uhasana na mimi, maana ile ya kuniida daladala naona haikumtosha. Yaani hapa ni ama zake ama zangu............
Leo friday bana mazoezi kama kawa kituo ni pale BP petrol station ambayo iko near na AMREF pia karibu na zamani nyumba ya sanaa. Hope umepanyaka muda sa kumi na moja na rpbo ukichelewa umeachwa, zingatia muda.
Umekuja na truck suit kweli umejiandaa heheheheeee see u there heheheheeee
 
ndetichia : nusu pakiti kwa watu 4. Maana yake ni pakiti moja kwa watu 8 ??? hapa unaongelea watoto au mtu wa miraba minne kama mimi?
sakapal : pakiti moja kwa watu wa nne.... thanks! ila hiki kipimo ni chako mwenyewe hakuna member mwingine amataja hivyo sijui huwa unaongezea na msuba kiasi? yaani familia yako ni: baba - Rural Swagga, mama - sakapal, mtoto - Smile ??!
King'asti : noodles nazifahamu sana dada..ila ki ukweli noodles pakiti moja hainitoshi lazima tu ntaongezea something else. Kuna dada yangu mmoja kila tukikutana mjini lazima anipeleke supermarket kuninunulia noodles... otherwise nmefurahi hadi wewe muke ya moderator Paw pia unabahatisha vipimo vya spaghetti.
Mamndenyi na Evelyn Salt kweli????
nsee a muro : mkuu jina lako gumu kumention mkuu! ila umesema pakiti moja kwa watu watatu nashukuru walau kidogo kuna mwingine amesema vivyo hivyo. Hapo kwenye mtu fidenge nilidhani ni nyumbani kwetu tu tulitumia hilo neno...hata sijui maana yake. Thanks pia kwa kukumbushia mboga mara nyingi huwa nanunua ila nkishamaliza kupika chakula naona uvivu kuuunga tena mboga za majani..sijui hili tatizo nitalitatuaje.
Elli : wewe unahitaji msaada mkubwa kuliko mimi mkuu! hahaha..
Profesa : kweli unastahili rank hiyo profesa! asante sana...ila hapo kwenye 'inategemea' bado umeniacha njia panda mkuu. Anyway, nasubiria kwa hamu hayo mapishi yako ya spaghetti na minced meat nifanye comparison ya notes na nipikavyo mimi.
shansarie : pakiti moja kwa watu watatu...naona umefanana na mkuu mwingine hapo juu. Nadhani hii ndiyo niichukue kama most right answer..thanks a lot dadangu!
watu8 : huyu muke ya moderator anatuchanganyia habari...angeongelea na macaroni pia! BUT go back to the topic na unisaidie hapo acha kuzunguka mbuyu....
 
Last edited by a moderator:
Mentor kanambia nije nipike
Hapo ndipo Mentor aliponishangaza..... kwamba anadhani hata wewe unajua kupika? Khaaa!!

Kweli kaniingiza kingi hebu nistue maana kama hakuwa anamaanisha spageti kweli anayake mambo anazidi kuongeza uhasana na mimi, maana ile ya kuniida daladala naona haikumtosha. Yaani hapa ni ama zake ama zangu............
Leo friday bana mazoezi kama kawa kituo ni pale BP petrol station ambayo iko near na AMREF pia karibu na zamani nyumba ya sanaa. Hope umepanyaka muda sa kumi na moja na rpbo ukichelewa umeachwa, zingatia muda.
Umekuja na truck suit kweli umejiandaa heheheheeee see u there heheheheeee

Hahahahaha pole mwaego... huyu dogo Mentor inabidi uwe makini naye sana. Eti anataka kujua kipimo cha spageti lakini akaanza na stori ndeeefu mpaka ya akitoka shule anaanza kuvulia nguo mlangoni.....Stuka mwanamazoezi mwenzangu... Think!!

Eneo la tukio nimeshalinyaka.... ili niiendane na muda ntatia timu hapo na tukutuku ili nikuwahi. Biashara ya kuambilia harufu yako nikiwa nyuma yako itanishinda. Shurti tuende sambamba. Pale Kebby's nshabook siti mbili kwa ajili ya kushusha pumzi. Ujue kabisa chips yai/ndege/mshikaki ni strictly prohibited.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom