Mentor
JF-Expert Member
- Oct 14, 2008
- 20,328
- 23,909
SPAGHETTI ya leo fupi!
2000
Kusema kweli nadhani mwaka huu wa 2000 ndiyo kumbukumbu yangu ya kwanza ya interaction yangu na chakula hichi. KWa muda mwingi nyumbani wakati tunakua tulikuwa tumezoea kufanyiwa kila kitu na wadada wasaidizi wa kazi nyumbani.
Nakumbuka tulikuwa tukitoka shule tunaanza kuvulia nguo mlangoni mpaka unafika chumbani umebaki na chupi tu..well, kwa siku ulizokumbuka kuivaa au kama asubuhi dada alikuvalisha nguo.
Hali hii iliendelea hadi tulipofika darasa la sita.
Siku moja baba aliamka tu na kuwaambia wale dada wajiandae warudi kwao. Nilijua dunia itafikia mwisho. Baba alidhani tungeishije sasa? Kazi zote zile nani atazifanya? Kwa hakika sio sisi, kwani tusiende mbali, usafi tu wa miili yetu tu ulikuwa a big challenge kwetu.
Maisha yalianza kuwa magumu kwani mimi na kaka yangu ilitubidi kuamka mapema na kuandaa chai na maji ya baba ya kuoga. Wakati mmoja akiandaa chai mwingine alikuwa zizini kutoa mfori/samadi kwa ngombe na kukamua kisha kuwalisha ngombe pamoja na kuku.
Hapo tulikuwa darasa la sita. Hivyo basi yote hayo yafanyike na bado ukatafute kuni uwahi kushika namba shule la sivyo imekula kwako.
Ratiba ya chakula ilikuwa tu na vyakula common kama makande, wali maharage, wali nyama, ugali maziwa au na mboga nyingine tu, chapatti na pilau. Kwa kweli hivi ndivyo tulivyokuwa tumevizoea.
2000
Nakumbuka niliporudi nyumbani likizo ndipo nikakutana na hii menu item mpya nyumbani..spaghetti!
Mama alitufundisha kidogo jinsi zinavyopikwa. Upishi wake kwa kweli ni mrahisi tu. Chemsha maji yenye mafuta na chumvi kasha tia spaghetti zako ndani. Njia ya kujua kama zimeiva ni kuitoa moja na kuirusha ukutani na ikinata tu unajua zimeiva..hivyo unaziepua na kuziweka kwenye colander. Kwa njia hii tulifanikiwa sana kuuchafua ukuta wa jikoni.
Kipindi kile tulikuwa wachache nyumbani tulikuwa tukipika pakiti moja. Kuna nyakati ilitubidi kurudi jikoni kwani hazikutosha na nyakati nyingine hata zilibaki. Katika mafunzo yale mama hakuwahi kutufundisha kipimo cha spaghetti kama alivyokuwa akifanya kwa makande au wali.
Baadaye yakaja macaroni na variety zake na zote hizi hatukuwahi kuambiwa vipimo vyake.
Wageni wakazidi nyumbani, nakumbuka kuna kipindi tulinunua hadi pakiti tatu za spaghetti kwa ajili ya mlo mmoja tu. Hata kipindi hicho hatukujua vipimo vya mapishi ya spaghetti kwa idadi specific ya wageni.
Katika pitapita mjini nikajafundishwa mapishi ya kipemba ya spaghetti. Yaani kuzikaanga kabla ya kutia maji au kutengeneza zile za futari..zenye sukari. Hata huyu binti wa kipemba aliyenifunza hakuweza kunieleza kipimo maalum cha mapishi ya spaghetti. Ilikuwa zaidi kama mchezo wa kubahatisha.
Sasa ninaishi mwenyewe nashindwa kabisa kupima kipimo kinachoeleweka cha spaghetti. Kuna siku zinazidi na siku nyingine zinapungua naishia kushushia kwa maji ili shibe itimie.
Wasalaam wapendwa,
Mentor.

NI KIPI KIPIMO SAHIHI CHA SPAGHETTI?
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
Last edited by a moderator: