Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Hapo ndipo Mentor aliponishangaza..... kwamba anadhani hata wewe unajua kupika? Khaaa!!
he he he najua kupika asikuambie mtu!!!!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo ndipo Mentor aliponishangaza..... kwamba anadhani hata wewe unajua kupika? Khaaa!!
Evelyn Salt : ataanza nitamalizia hapo baadae kidogo.
Kakangu mdogo, tatizo tulikudekeza sana.
Kuna spagheti flani zimeandikwa 'instant noodles' zinapatikana supermarket. Hebu zicheki na ni portion ya mtu mmoja tu. Uzuri wake zinakuwa na flavour kapakti kadogoo. Ukichemsha tu unachuja maji unatia flavour kitu mwake.
As of kipimo hata mie huwa nabahatisha tu. Na utamu ukizidi wengine hupikiwa supplimentary juu ya uroho. Ila kuwaweza nahakikisha wanapata matango ya kutosha kwenye sahani.
watu8: hebu malizia mapishi ya hiyo kitu mkuu. Ila wewe noma college ulikuwa na oven ya nini sasa mkuu??
Asprin : babu naona unanchonganisha na sakapal, unajua ndo huwa tunavutaga naye bangi? #SInA MAANA HIYOOOOOOO
Shixi889: haha mkuu ni balaa kufikiria cha kupika aisee..ila ngoja nkuulize swali..una maanisha ushaoa? Na je, ukishaoa ndo mwisho wa kupika? maana nnaeza nisioe kwa hali hiyo...i love cooking..ts one of my hobbies.
Mamndenyi na Evelyn Salt : shukeni basi hivyo mnavyojua kupika na mm nipaje ujuvi zaidi...
Anza wewe mi ntarudi kupika chai!!!
baadae ugali wa kisukuma ule mgumu kumeza.....
Hahahaha kwa jinsi unavyopenda chumvi, hauzidishi kwenye mchuzi kweli?he he he najua kupika asikuambie mtu!!!!!!
Hahahaha kwa jinsi unavyopenda chumvi, hauzidishi kwenye mchuzi kweli?
[h=3][/h]
Mapishi ya Ndizi za nazi na utumbo
Mahitaji
Ndizi mshale 10
Utumbo wa ng'ombe 1/2 kilo
Nazi ya kopo 1
Nyanya 1
Kitunguu kikubwa 1
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chakula
Olive oil kiasi
Limao 1
Chumvi
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Coriander ya powder 1/2 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Pilipili kali nzima (usiipasue)
Matayarisho
Safisha utumbo kisha uweke ktk pressure cooker pamoja na chumvi kiasi, limao, tangawizi, swaum na maji kiasi kisha uchemshe kwa muda wa nusu saa.
Baada ya hapo menya ndizi kisha zikate vipande vidogo kiasi ili ziwahi kuiva, kisha ktk sufuria ya kupikia tia vitunguu na nyanya kisha ndizi kwa juu yake na supu ya utumbo kiasi chumvi kidogo na mafuta kiasi kisha bandika jikoni na uchemshe mpaka ndizi zikaribie kuiva.
Zikisha karibia kuiva tia utumbo na spice zote, pilipili nzima na tui la nazi kisha changanya vizuri na uache vichemke mpaka ndizi na tui la nazi vitakapoiva na rojo ibaki kiasi. Baada ya hapo Ndizi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Baada ya msosi matunda.........
![]()
Mahitaji....(Kwa mtu mmoja)
Ndizi mbivu 1
parachichi (avocado) 1/2
kipande cha tikiti kidogo (water melon)
kipande kidogo cha nanasi
kipande kido cha embe lililoiva vizuri
sukari kijiko kimoja cha chakula
maji robo kikombe
jinsi ya kutengeneza....
.kata kata matunfa yako katika vipande vidogo vodogo uchanganya katika bakuli moja (sio kwenye sufuria au chombo cha aluminium yanakuwa meusi)
.weka suraki katika mchanganyiko wa matunfa na uchanganye vizuri
weka maji nauendelee kuchanganya hadi matunda yachanganyikane vizuri
Matunda yako yapo tayari kwa kuliwa
![]()
CC: Asprin
Karibuni chakula.....
kwa hisani ya Mamndenyi na Evelyn Salt
Kakangu mdogo, tatizo tulikudekeza sana.
Kuna spagheti flani zimeandikwa 'instant noodles' zinapatikana supermarket. Hebu zicheki na ni portion ya mtu mmoja tu. Uzuri wake zinakuwa na flavour kapakti kadogoo. Ukichemsha tu unachuja maji unatia flavour kitu mwake.
As of kipimo hata mie huwa nabahatisha tu. Na utamu ukizidi wengine hupikiwa supplimentary juu ya uroho. Ila kuwaweza nahakikisha wanapata matango ya kutosha kwenye sahani.
Kula kidogo tu...
ukibakiza nitamalizia
watu8: hebu malizia mapishi ya hiyo kitu mkuu. Ila wewe noma college ulikuwa na oven ya nini sasa mkuu??