loyan20
Member
- Oct 16, 2014
- 29
- 18
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi never give upUmesoma au kusikia maneno mengi yatiayo moyo na msukumo katika mambo yako mengi, pale ukatapo tamaa au kuvunjika moyo..
Ni neno lipi kwako linakusimamisha pale unapolegea Katika majaribu au kukatishwa tamaa, na kuwa chakula cha roho!
Mimi la kwangu ni hili
View attachment 614441
kasemaje vileee!!!!!!Good morning mkuu.... Ujumbe mzuri
soma kilichomo ndani utaelewakasemaje vileee!!!!!!
Mkuu nimeapriciateNUKUU ZA LEO
1. Napenda kuwaambia wale wanaodhani siasa haiwahusu, Moja ya madhara ya kukataa kujihusisha na siasa ni kwamba utaongozwa na watu uliowazidi akili. Na kwa upungufu wao wa akili watafanya maamuzi ya kila kitu kinachohusu maisha yako - Plato
2. Moto mkali zaidi wa jehanam wameandaliwa wale wanaojifanya wapo neutral mahali ambapo wanyonge wanaonewa - Martin Luther King, Jr
3. Kama hatuamini uhuru wa maoni kwa wapinzani wetu, basi hatuamini katika uhuru wa maoni kabisa. Kwa sababu wafuasi wetu hawahitaji uhuru wa kusema, bali wapinzani wetu - Noam Chomsky
4. Binadamu kwa asili ni mnyama wa kisiasa. Kumtenganisha na siasa ni sawa na kumzuia kuishi - Aristotle
5. Changamoto kubwa ya ulimwengu kwa sasa ni kwamba wenye akili hawataki kujihusisha na siasa, na hivyo wajinga wamepewa mamlaka ya kuwatawala wenye akili na wasio na akili - Donald Trump
6. Siamini kama tofauti ya mawazo katika siasa, au imani ya kidini inaweza kupoteza urafiki wangu na mtu yeyote - Thomas Jefferson
7. Wanaosema dini na siasa havina uhusiano, hawajui maana ya dini - Mahatma Gandhi
8. Siasa ni sanaa ya kuibua matatizo ya jamii, kuonesha unaumizwa nayo, kisha kujifanya unayatatua kumbe unayaongeza. Maana bila matatizo ya jamii hakuna wanasiasa - Groucho Max
9. Siasa ni vita isiyo na damu, na vita ni siasa yenye damu" Mao Tse Tsung
10. Sipendi vichekesho (comedy), lakini napotaka kucheka hufuatilia namna serikali inavyofanya mambo yake - Will Rogers
Malisa GJ
Nae kaka
1. "Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo." Napoleon_Bonaparte.
2. "Lengo la kwanza la vita sio kufa kwa ajili ya nchi yako, hapana. Bali ni kuua mtu mwingine kwa ajili ya nchi yake." George_Patton.
3. "Lazima nisome siasa na vita ili mwanangu apate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa." John_Adams.
4. "Washindi wanashinda kwanza halafu wanakwenda vitani, wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndio wanatafuta ushindi." Sun_Tzu.
5. "Inafahamika vizuri katika vita, majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kwamba, wakati wa vita, ukweli huharibiwa vibaya na propaganda."
Harry_Browne.
6. "Propaganda ikitumiwa vizuri inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso." Adolf_Hitler.
7. "Mtu mwenye ufahamu wa kweli, si tu kwamba atawapenda maadui zake wanapofanya vizuri, bali pia atawachukia marafiki zake wanapokosea." Friedrich_Nietzsche.
8. "Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka." Confucus.
9. "Tofauti kati ya akili na ujinga ni kuwa, akili ina kikomo, ujinga hauna kikomo." Albert_Einstein.
10. "Kuna watu wawili tu wasioweza kubadili mawazo. Mpumbavu kuliko wote na mwenye hekima kuliko wote." Plato.
11. "Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo." Harry_Truman.
12. "Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili." Benjamin_Franklin.
13. "Unajisi wa sheria hutokea pale ambapo mahakmu/majaji, hujiweka mikononi mwa watawala na kuamini watawala wana nguvu kuliko sheria" Lamar_Smith.
14. "Kuliko kuwapa wanasiasa ufunguo wa maisha yako, ni bora ubadili kitasa" . Doug_Larson
15. "Siasa ni hatari kuliko vita. Kwenye vita mtu hufa mara moja tu, lakini kwenye siasa mtu hufa na kufufuka mara nyingi kadri iwezekanavyo" . WinstonChurchil.