Special thread: Interesting (best) Quotes | Misemo yenye hekima ndani yake, Nukuu
"Mambo makubwa yanayosababisha mishipa ya moyo kuziba ni pamoja na ulaji wanga, mafuta na sukari.

Watu wengi wanadhani mafuta tu ndio yananenepesha. La hasha, wanga ndio mbaya zaidi. Wengi wananenepeana kutokana na wanga. Ndio maana utafiti uliofanywa unaonesha watu wanaonenepeana wako zaidi nchi za Kiarabu.

Mwezi wa Ramadhani waislamu wenzangu wengi huongezeka sana uzito. Hii ni kwasababu ya kula vyakula na mahanjumati yenye wanga mwingi. Pia, vyakula hivyo huliwa muda mbaya (ftari saa 12 na daku kuanzia saa 6 usiku) ambapo mwili unakuwa hauna activities na hivyo metabolism huwa ni kwa kiasi cha chini sana. Kwa siku, Sisi tunakula wanga mwingi asubuhi lakini hatuna activities tunapanda magari na kushinda ofisini tumekaa siku nzima!!!.

Lazma tutanenepeana tu, hamna namna. Hii ni tofauti na wenzetu wa vijijini. Wao wanaruhusiwa kula vyakula vya aina zote kwani wana activities nyingi. Hivyo, nashauri mle vyakula stahiki, mfanye mazoezi na mywe maji kiasi. Maji mengi sana hayafai kabisa kwani yanayayusha madini mwilini ambayo ni muhimu. Kunywa lita moja na nusu tu. Mimi sijala mkate, chapati, vitumbua, maandazi nk kwa miaka 10 na sijanywa juisi na soda kwa miaka 3.

Pendelea kula matunda badala ya juisi na pia kula sana mboga mbalimbali za majani. Nakusihi sana usisikilize tumbo, mdomo wala macho kwani vitakupotosha, badala yake sikiliza ubongo wako ukikwambia _"Prof. Jannabi aliniambia nile nini?"_. "DIET" ni sawa na SALA. Maana yake ni kuwa unajiandalia huko mbeleni. Uchaguzi ni wako".*

Prof. M. JANNABI,
 
😂 Daktari wengine wapo very biased kwa nini asieleze madhara ya caffein hiyo anayo claim kuitumia kila asubuhi????
 
Na anza na hizi...
wall1559217541373.jpeg
wall1559217563161.jpeg
wall1559217574514.jpeg
wall1559217614434.jpeg
wall1559217664538.jpeg
temporary_file.jpeg
1559218944404.jpeg
wall1559217727767.jpeg
wall1559217698208.jpeg
 
Salamu!

Kumekuwa na nukuu mbalimbali ama kwa lugha ya Kiingereza 'Quotations' hasa kutoka kwa watu maarufu ambazo zinafahamika sana huku zingine zikionekana kama hazina maana yeyote ama zingine zina ujumbe uliofichwa kiasi kwamba pengine unahitaji uwe 'Great Thinker' ndio uweze kung'amua maana zake la sivyo utaishia kutoka kapa.

Kuna baadhi ya nukuu huwa zinafikirisha sana ingawa kwa wengine zinaweza kuwa kama upuuzi huku upande fulani wakiona kuwa zina maana fulani ambayo si yakuidharau na zinakufanya ufikirie sana kwamba ni kwanini muhusika aliamua kuzungumza vile. Mifano yake ni hizi hapa;

  • "If you want to steal, steal a little in a nice way. But if you steal too much to become rich overnight, you'll be caught". - Mobutu Sésé Seko kuku ngbendu wa za Banga

Kwa kiswahili, Mobutu Sésé Seko aliwahi kusema kwamba "Ukitaka kuiba, basi iba kidogo kidogo na kwa njia nzuri lakini ukiiba sana uwe tajiri kwa usiku mmoja, utakamatwa tu"

Nukuu nyingine hii hapa;

  • "The only white man you can trust is a dead white man". - Robert Mugabe

Mugabe
aliwahi kusema kwamba "Mtu mweupe (Mzungu) pekee wa kumuamini ni mtu mweupe aliyekufa"

Kuna nyingine nyingi tu kama;
  • Everything has its limit, Iron ore cannot be educated into gold. (Mark Twain)
  • The difference between stupidity and genius is that genius has its limits. (Albert Einstein)
  • An intelligent hell would be better than a stupid paradise. (Victor Hugo)
Naam! hizo ni baadhi tu ya nukuu zenye jumbe za kufikirisha sana kutoka kwa watu mbalimbali maarufu waliowahi kuwepo hapo zamani na waliopo hivi sasa ambao walitoa mawazo yao tu kutokana na maswala mbalimbali waliyokutana nayo katika maisha yao ila jukumu la kukataa ama kukubaliana ni hicho walichokizungumza linabaki kuwa ni la mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom