Mgombea Urais kwa tiketi ya CHAUMA, Bwana Hashim Rungwe ana hoja ya msingi anayotaka kutuambia watanzania, tusimpuuze na kauli yake ya lishe Bora na kula ubwabwa.
1. Lishe bora hutatua changamoto za maradhi ya mara kwa mara. Hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa kujenga hospital, kununua vifaa vya tiba na madawa. Naamini ubwabwa ambao watu wa vijijini hula siku ya sikukuu tu, ukitumika vema tutakuza uchumi kwa kupunguza bajeti ya wizara ya Afya na kupeleka kwenye viwanda.
2. Lishe bora huongeza kuzaliana, watu watazaliana na kukua bila shida, hapa nchi itapata nguvu kazi ama rasilimali watu ya kutosha. Hawa ndiyo watakaoipeleka Tanzania kuwa donor country huko mbeleni.
3. Ubwabwa huu huu ambao tunaudharau, utawafanya watanzania waishi kwa furaha sana. Ukizingatia hiki ni chakula pendwa kwa Watanzania wa rika zote. Furaha ni chimbuko la fikra chanya. Mwenye njaa siku zote hawezi kuwaza maendeleo. Atawaza chuki, unafiki, wivu na visasi. Lakini ukishiba, Wala huwazi hayo.
4. Watanzania wengi sasa hivi ni legelege, watoto wao wanaozaliwa ni lege lege. Tunakaribia kupoteza ile spishi ya majayanti. Kwasababu, wazazi wao kwa kukosa lishe wanatoa sperms na mayai yasiyo bora kwa kukosa Lishe. Tusiipuuze hoja ya Mh. Rungwe ili tuzae watoto kama akina Goliath na Samson.
Wachache sana tumemwelewa huyu mzee. Ana hoja za msingi kabisa.