Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

ah! huyu nae yumo tu nae anatumia haki yake ya mtandao anachguliwa RAIS sio STUFF SERGENT.

Msimpe kazi Mkuu wa majeshi Mwamunyange.Yaani mtu anashimdwa hata kupanda jukwaa dogo tu kuhutubia mnataka Mwamunyange ajitwike mgongoni kumpandisha jukwaa lile la uwanja wa Taifa?

Raisi anatakiwa awe fit kiafya.Likitokea hata la kutokea ukimwambia oyaaa kimbia unajua kuna wanga wanakuja awe na uwezo wa kukimbia.Hatakiwi kuwa mbovu kiafya wa kubebwa na mabody guard hawezi hata kukimbia.Uraisi sio ujumbe wa nyumba kumi ujue!

Kura yangu nampa Magufuli
 
Huenda ameshaona upepo unaovuma utamfunua shati
kweli magufuli amekua tofauti, ila mi naamini huyo ndio "real magufuli"
huko kwingine alikua anafake
 
CCM na MREMA wote ni wa kuachwa walivyo.hali mbaya sana.
 
Magufuli wazee wa zamani wangesema hana 'koromeo'
yeye ni mtu ambae hawezi kujizuia kuropoka....ni aina ya watu ambao ukiwabana live mbele ya watu
anaweza ongea usicho tarajia......

Nadhani pia wazazi hawakukosea kumpachikia jina la Magufuli wakijaribu kumziba kinywa
 
Usiwachongee wanajeshi na siasa. Toa sababu ingine lakini siyo hii. Kama ingekuwa ni wanajeshi tu wanapiga kura ingeeleweka hivyo; lakini hata asilima 0.1 hawafikii kulinganisha na wapiga kura wote.


Si hao tu wasio walutheri na wasio wachaga watamnyima kura sababu ya yeye na mkewe regina kuendekeza udini na ukabila

Wasikilize kwenye hii video uone Lowasa na Mkewe walivyojaa Udini na ukabila.Hawapati kura sehemu zingine.

https://www.youtube.com/watch?v=0Tl48gwQN84
 
Nimesoma,aliwaambia wamchague Shirima,ndo first choice hiyo,then akasema incase hawamtaki Shirima basi MREMA.Ila wewe lofa story ulivyoileta ni kama vile Magufuli first choice yake ni MREMA

Yaani anaweka option dhidi ya chama chake, ni hatari. Je Kinana akisema mchague Magufuli, na kama hamtaki Magufuli basi mchague Anna Mugwira, je inakuja hapo!?
 
2013 nchini Kenya alitokea mwanazuoni moja aliyepata umaarufu sana katika vyombo vya habari na hata kwa wananchi.

Mutahi Ngunyi aliibuka na " Tryanny of Numbers Kenya" falsafa kubwa katika hii hypothesis ilikuwa ni kuonyesha uwiano wa kura watakazopata muungano wa Jubilee (Uhuruto) na ule wa CORD (Raila na Kalonzo)..

Mutahi Ngunyi kwa mahesabu yake na kwa kuangalia uandikishaji wa kadi za mpiga kura kwa jamii ya GEMA, Kalenjin, Luo, na Kamba alisema wazi kuwa Uhuruto na muungano wao wa Jubilee watashinda urais, tena kwenye firts round. Na kwa hakika hicho ndicho kilichotokea...

Mutahi Ngunyi alieleza mapema kabisa kuwa uchaguzi ni mahesabu. Na kama hauna numbers usijaribu kuingia kwenye uchaguzi... Kuna ambao watasema siasa za Kenya ni tofauti na za Tanzania, hawako sahihi..

Uchaguzi wa sasa lazima tukubali mgombea atapata kura kadri anavyokubalika katika eneo husika (we call it block). Uchaguzi wa sasa utaangalia nani aliinvest mapema kwa wananchi. Uchaguzi wa sasa utaangalia zaidi jina na umaarufu wa mgombea husika. Uchaguzi wa sasa utaangalia mtandao waliojiwekea kwa miaka 20 au zaidi iliyopita.

Uchaguzi wa sasa utaangalia nguvu waliyonayo kwa kundi la vijana. Uchaguzi wa sasa utaangania ni jinsi gani unaungwa mkono na makundi maalum kama machinga, bodaboda, mamantilie ambao ndio wako wengi zaidi..

Lowassa ambaye ni mgombea wa Chadema na anayeungwa mkono na umoja wa Ukawa ana kila dalili za kushinda huu uchaguzi. Lowassa alijipanga sana kwa muda mrefu, zaidi ya miaka 20. Lowassa alijipanga kwa wananchi (na kumbuka hii ni kampeni yake ya pili anafanya, baada ya ile ndani ya CCM aliyozunguka nchi nzima, na karibia wilaya zote).

Lowassa aliwekeza kwenye vyombo vya usalama. Lowasaa aliwekeza kwenye chombo cha mahakama. Lowassa aliwekeza ndani ya usalama. Na kubwa zaidi Lowassa aliwekeza kwenye jumuiya za kijamii....

Ukitumia methodology ya Mwanazuoni Mutahi Ngunyi lazima utaona kwamba Lowassa atakuwa na uwakika wa kushinda katika mikoa mingi. Tena mikoa ambayo ina idadi kubwa ya wapiga kura... Lowassa ana100% confidence level kushinda, mikoa ifuatayo....

1. Dar es Salaam
2. Mbeya
3. Mwanza
4. Arusha
5. Tanga
6. Kilimanjaro
7. Mara
8. Geita
9. Kagera
10. Shinyanga
11. Singida
13. Pemba
14. Mtwara
15. Ruvuma (*upepo unaweza kubadilika)
16. Njombe
17. Iringa
18. Manyara
19. Katavi

Ukipiga mahesabu kwa hiyo mikoa, ni wazi Lowassa atashinda. Haya sio maajabu wala miujiza. Ukitumia fomula ya Muhayi Ngunyi huwezi kuwa na wasiwasi kwenye hili (kwa kujua fomula husika, goolge Mutayi Ngunyi "Election hypothesis")...

Huu uchaguzi sio miujiza. Tofauti kubwa ni kwamba Lowasaa kaingia kwenye huu uchaguzi akiwa tayari ana numbers kama ilivyokuwa kwa Uhuruto. CCM hasa "mgombea wa CCM" kaingia kwenye huu uchaguzi kwa mara ya kwanza wakiwa hawajui idadi yao kamili ya kura watakazopata kwenye mikoa husika na hata wilaya husika...

Lowassa alihamasisha sana wananchi hasa vijana kujiandikisha kwa wingi. Lowassa alikuwa na makundi zaidi ya 6 yanayomuunga mkono, na hayo makundi yalifanya kazi kubwa sana ya kuhamasisha vijana kujiandikisha kwa wingi sana. Na ndio mana leo hii tunaona kwamba vijana zaidi ya asilimia 68.58% ndio waliojiandikisha (NEC, record)....

NB: Naomba niwambie wazi kabisa, CCM kushinda huu uchaguzi ni ndoto. Ukawa/Lowassa watashinda tena kwa asilimia nyingi sana...

Baada ya siku 15 nitarudi tena hapa. Na kwa hakika mtasema Ocampo four kawa Mutahi Ngunyi wa Tanzania....
 
Hatumuogopi tunamtaka huyo huyo Magufuli.
JPM ni mjanja sana. Anatafuta mbinu zake mwenyewe nje ya CCM kuingia madarakani.
Hataki aambiwe amewekwa marakani na CCM maana anakusudia kuwatia adabu viongozi waliokuwapo kabla yake. Ndiyo maana anasema chagua Magufuli, Serikali ya Magufuli, Tanzania ya Magofuli. Kwa mara ya kwanza nchi hii itakuwa na Rais dikteta na atatesa watu sana.

Salama ya JK na familia yake ni kumweka kando JPM.
JK aliposema serikali yake haina ubia ilikuwa anachekesha na ameshindwa, JPM anataka kumaanisha kweli kuwa hii yake ndo haina ubia kiukweli maana kila kitu ni yeye

Huyu Bwana ni wa kuogopa kama ukoma.
 
Nimesoma,aliwaambia wamchague Shirima,ndo first choice hiyo,then akasema incase hawamtaki Shirima basi MREMA.Ila wewe lofa story ulivyoileta ni kama vile Magufuli first choice yake ni MREMA

dah unajikanyaga kanyaga tu sasa hiyo siyo kampeni?
 
Ukilinganisha na jinsi alivyosema na kutenda kwenye uzinduzi wa kampeni zake Jangwani,Dr. Magufuli amebadilika sana. Mwanzoni alikuwa akizungumzia hoja za Ilani ya CCM kwa umahiri na kueleweka.

Katika siku za karibuni,Dr. Magufuli amekuwa akisema na kutenda mambo ya kushangaza. Amepiga hadi pushup jukwaani pamoja na kurukaruka kama afanyaye mazoezi. Jana alipomuacha mgombea wake wa CCM na kumuombea kura Mrema wa TLP kwenye Ubunge wa Vunjo,amezidi kushangaza.

Kimsingi,lipo jambo lililombadilisha. Kama si uchovu itakuwa msongo wa mawazo. Au hata kukata tamaa kwaweza kuwa sababu ya mabadiliko yake.


haya yote ni matatizo ya ajali mkuu.inapotokea ajali chochote chaweza kutokea.hii ni shida ya kumpata mgombea asiyetarajiwa,yaani hakujiandaa na wala hakuandaliwa,so inafika sehemu anakuwa hajielewi elewi tu
 
Nimefuatilia na sijaona sehemu hata moja Magufuli akiwaambia wana Vunjo wamchague Mrema katika ubunge,Wewe unaumwa unahitaji kumwona DR wa akili
What was the point of Mrema staging up alongside Pombe at a Ccm rally?

Pome kachanganyikiwa kuliko hata alivochanganyikiwa Kiraracha
 
What was the point of Mrema staging up alongside Pombe at a Ccm rally?

Pome kachanganyikiwa kuliko hata alivochanganyikiwa Kiraracha
Mrema ndo alimsubiri Rais Magufuli ,jamani Magufuli ni Rais wa wote bila kuja;i itikadi za vyama vyenu
 
Upepo wa siasa unavuma kwa kasi kuelekea mabadiliko
 
Back
Top Bottom