Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Anaposema ataongeza ajira kwa vijana yupo sahihi na anaamini hivyo, uboreshaji tu wa miundo mbinu hususani barabara katika kipindi chote akiwa wizara ya ujenzi bado katengeneza ajira nyingi kwa vijana. Sasa anakuja na mikakati ya kufufua viwanda vya ndani ili kutengeneza ajira nyingi kwa vijana wote. Hakika huyu ndiye kiongozi tunayemtaka kwa sasa Tanzania.
 
Anapozungumzia kufufua viwanda atuambie nani aliviua ikiwa wenzake waliotangulia wameshiwa hata kudhibiti wanyama wetu yy atawezaje atueleze kwanza udhaifu wa watangulizi wake kisha atuambie atarekebisha
 
Ni watu wajinga na wenye upeo mdogo hutumia ukanda katika kuleta hoja, kwann mnapenda ukanda?
siku haya mawazo yenu yakizaa matunda ni nani atakayepona?
Ebu tumia key board yako kuleta changes, si kupandikiza ukanda, unapumbaza akili yako, ahsante kama utaelewa.
 
Nimeshangaa nilipoona na kusikia mh.Magufuli alipokuwa akinadi sera huko mbeya alisema:

"Nimeamua kutembea kwa gari ili nione matatizo na changamoto za barabara japo wengine watakuja kwa ndege na helkopta hawawezi kujua changamoto za barabara"

Najiuliza hivi katika miaka 20 aliyohudumu kama waziri miaka 20 amehudumku kama waziri wa Ujenzi sasa leo anasema ndiyo anatembea kwa gari ili kujua changamoto za barabara ataweza kuzijua chanhamoto hizo kwa siku za kampeni wakati ameshindwa kwa miaka 20?

Bungeni alikuwa akitoa takwimu za barabara na kilomita nyingi,kumbe zilikuwa za uongo?alizitoa wapi hizo takwimu wakati hata changamoto hazijui?

Wananchi yeye amesema anashangaa wanafunzi kukaa chini? Anashangaa kuona kina mama wanajifungulia chini? Anashangaa kuona dawa hazionekani na hazipo hospitalini?

Je wananchi nyie hammshangai?

Hivi anashangaa hayo au anaishangaa ccm kuongoza miaka hamsini na nne bila hzo huduma?

Mshangaeni! Chukueni hatua.

Nadhani huyo ni mpinzani.Maana hana tofauti na fast jet yeye alisema hajui kwanini Tanzania ni maskini.Sasa huyu hajui kwanini akina mama wananifungulia chini.Duh ukiwa mnafiki ni shida kabisa.

Mpinzani hakika katika vazi lake halisi la upinzani.Kwa kweli hatufai hata kwa bure.
 
Wadau naomba tujiulize suala moja kuhusu mgombea wa CCM ambaye ni waziri wa ujenzi, wizara inayotuhusu sisi sana. Magufuli anasema nitaongeza ajira kwa vijana. Najiuliza amefanya juhudi gani kuinua wakandarasi wazawa? Anatoa takwimu kwamba kuna waandisi 15,000 wana kazi za maana. Anaweza kutuonyesha angalau wakandarasi wazawa 10 wanaoweza kufanya kazi kwenye nchi za East Africa Class one? Au hawa wanaoshinda whatsapp ? Kama ameshindwa kutengeneza wazawa contractors akiwa ujenzi wa kueleweka ataweza vipi nchi nzima? Bajeti ya wizara ya ujenzi ni kubwa kuliko wizara zote lakini pesa yote inarudi China. Sababu wachina wanaagiza kila kitu toka kwao. Tunachoambulia sisi ni pesa ya mchanga, hata kokoto wanapasua wao, wanakula kwenye migahawa yao kila kitu ni wao. Kwa nini hakuweka sera nzuri kwenye ujenzi? Uchumi lazima udumae hakuna mzunguko wa pesa kwa hawa watu kila kitu kinatoka kwao kuanzia nondo mpaka tooth pick. Hata wenye nyumba hawapati pesa maana wengi wanalala site. Wakipanga wanakaa nyumba moja watu hamsini kwenye nyumba moja. Unajivunia kuwa na waandisi wengi wasiokuwa na kazi. Na waliothubutu kujikakamua hawalipwi, wengine washauziwa mali zao na benki. Pesa inayozunguka kwenye barabara na miradi ya majengo toka mifuko ya jamii, NHC na taasisi ya serikali, kama kungekuwa na mipango madhubuti ya kuwaendeleza waandisi wazawa wangekuwa mbali sana sasa hivi. Sasa mtu kama huyu ameshindwa kuwa mlezi mzuri wa sekta moja anaweza nchi nzima. Tafakari.
Sijui kama hawa wakandarasi wetu wanaweza kushindana katika soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki!
 
Kumbe hii sera ya kisanii ya wanachama wa upinzani kurudisha card CCM bado inaendelee,ina maana CCM wamechoka kiasi hiki hata uwezo wa kutunga usanii mwingine hawawezi tena.
 
Nimeshangaa nilipoona na kusikia mh.Magufuli alipokuwa akinadi sera huko mbeya alisema:

"Nimeamua kutembea kwa gari ili nione matatizo na changamoto za barabara japo wengine watakuja kwa ndege na helkopta hawawezi kujua changamoto za barabara"

Najiuliza hivi katika miaka 20 aliyohudumu kama waziri miaka 20 amehudumu kama waziri wa Ujenzi sasa leo anasema ndiyo anatembea kwa gari ili kujua changamoto za barabara ataweza kuzijua chanhamoto hizo kwa siku za kampeni wakati ameshindwa kwa miaka 20?

Bungeni alikuwa akitoa takwimu za barabara na kilomita nyingi,kumbe zilikuwa za uongo?alizitoa wapi hizo takwimu wakati hata changamoto hazijui?

Wananchi yeye amesema anashangaa wanafunzi kukaa chini? Anashangaa kuona kina mama wanajifungulia chini? Anashangaa kuona dawa hazionekani na hazipo hospitalini?

Je wananchi nyie hammshangai?

Hivi anashangaa hayo au anaishangaa ccm kuongoza miaka hamsini na nne bila hzo huduma?

Mshangaeni! Chukueni hatua.

Mimi mwenyewe ninamshanga makofuli anavyoshangaa matatizo ya watanzaniaas if kama ndio kayajua wakati huu. Wakati anashangaa watendaji nao wanamshangaa, nao wananchi wanamshangaa kwa waziri WA utawala uliopo madarakani anashangaa kero za watanzania. Watanzania atudanganyiki rais ajae kesho atanguruma tusikilize hoja na mipango yake thabiti yenye lengo la kuwaondoa watanzania kwenye dimbwi la umaskini,ukosefu WA ajira,elimu bora,kilimo cha kisasa na chenye tija,na uchumi mathubuti na WA kumkomboa mtanzania. Twende na lowasa 2015.
 
Atuambie kwani Nani aliviua halafu yeye avifufue vinginevyo ni maigizo maana angetuonyesha hata kiwanda kimoja alivyo kua uvuvi
 
Anapozungumzia kufufua viwanda atuambie nani aliviua ikiwa wenzake waliotangulia wameshiwa hata kudhibiti wanyama wetu yy atawezaje atueleze kwanza udhaifu wa watangulizi wake kisha atuambie atarekebisha

Kama kaweza kwenye barabara hicho ni kilelezo tosha kuwa yeye akiwa ndiye rais atayaweza na hayo yaliyo shindikana kwa wengine.

Lazima tukubali jamaa Mungu kamjalia talanta ya ukiranja, ni hapo sasa Mungu akipenda akawa kiranja mkuu wa taifa, ndipo tutakapo ona vizuri hiki kipaji chake
 
Back
Top Bottom