Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Kwi kwi kwiii hili liongo aisee nimeongea na watu wa Mbeya wanasema sasa ivi mkutano ndo unafanyika na watu sio weng kivile
 
Haijawai kutokea, maelfu kwa maelfu kujitokeza kesho mjini Mbeya Kumlaki mh Magufuli.
 
Hahahah mh Magufuli yuko mbeya sa hivi na anaonyeshwa live na clouds TV, star tvNa TB1, uongo sio dili kabisaa
 
Kachanganyikiwa mwacheni, mkutano ndo unafanyika aangalie star tv watu wachacheee
 
Kesho Ni Siku ya UKAWA Jangwani.. Mambo Ya Magufuli Tumeshayasikia Ni yaleyale ya CCM Siku Zote...
 
Hatimaye Mh John Pombe Magufuli apokelewa kwa shangwe na MAELFU ya wakazi wa Mbalizi, Mbeya.

Hata hivyo rais huyo mtarajiwa aliwahakikishia wakazi hao serikali yake itatoa kipaumbele katika kufufua viwanda, ikiwa ni kusaidia kutengeneza ajira nyingi kwa vijana. Aidha Mh Magufuli pia kasisitiza kuboresha miundo mbinu hususani ujenzi wa barabara za kisasa ambazo zitakuwa ni kitovu cha kuinua uchumi wa nchi hii na kuondoa umaskini.
Hata hivo katika mkutano huo zaidi ya wanchama 1000 wa CHADEMA wamerudisha kadi zao na kujiunga rasmi na CCM.
Wanachama hao wapya wameahidi kuachana na porojo, kubuluzwa, hatimaye kuchukua hatua mapema, wamempongeza sana Dr Magufuli kwa utendaji wake uliotukuka.

KAZI NI KAZI TU
 
Ni zaidi ya mafuliko mbeya mjini, matangazo kurushwa live zaidi ya channel 4 za tv nchini

Kwa hiyo? Na wote waliojaa uwanjani wamevaa njano na kijani. Huyo mgombea anaomba kura kwa watanzania au wana-CCM pekeyao?
 
Nimeshangaa nilipoona na kusikia mh.Magufuli alipokuwa akinadi sera huko mbeya alisema:

"Nimeamua kutembea kwa gari ili nione matatizo na changamoto za barabara japo wengine watakuja kwa ndege na helkopta hawawezi kujua changamoto za barabara"

Najiuliza hivi katika miaka 20 aliyohudumu kama waziri miaka 20 amehudumu kama waziri wa Ujenzi sasa leo anasema ndiyo anatembea kwa gari ili kujua changamoto za barabara ataweza kuzijua chanhamoto hizo kwa siku za kampeni wakati ameshindwa kwa miaka 20?

Bungeni alikuwa akitoa takwimu za barabara na kilomita nyingi,kumbe zilikuwa za uongo?alizitoa wapi hizo takwimu wakati hata changamoto hazijui?

Wananchi yeye amesema anashangaa wanafunzi kukaa chini? Anashangaa kuona kina mama wanajifungulia chini? Anashangaa kuona dawa hazionekani na hazipo hospitalini?

Je wananchi nyie hammshangai?

Hivi anashangaa hayo au anaishangaa ccm kuongoza miaka hamsini na nne bila hzo huduma?

Mshangaeni! Chukueni hatua.
 
Wadau naomba tujiulize suala moja kuhusu mgombea wa CCM ambaye ni waziri wa ujenzi, wizara inayotuhusu sisi sana. Magufuli anasema nitaongeza ajira kwa vijana. Najiuliza amefanya juhudi gani kuinua wakandarasi wazawa? Anatoa takwimu kwamba kuna waandisi 15,000 wana kazi za maana. Anaweza kutuonyesha angalau wakandarasi wazawa 10 wanaoweza kufanya kazi kwenye nchi za East Africa Class one? Au hawa wanaoshinda whatsapp ? Kama ameshindwa kutengeneza wazawa contractors akiwa ujenzi wa kueleweka ataweza vipi nchi nzima? Bajeti ya wizara ya ujenzi ni kubwa kuliko wizara zote lakini pesa yote inarudi China. Sababu wachina wanaagiza kila kitu toka kwao. Tunachoambulia sisi ni pesa ya mchanga, hata kokoto wanapasua wao, wanakula kwenye migahawa yao kila kitu ni wao. Kwa nini hakuweka sera nzuri kwenye ujenzi? Uchumi lazima udumae hakuna mzunguko wa pesa kwa hawa watu kila kitu kinatoka kwao kuanzia nondo mpaka tooth pick. Hata wenye nyumba hawapati pesa maana wengi wanalala site. Wakipanga wanakaa nyumba moja watu hamsini kwenye nyumba moja. Unajivunia kuwa na waandisi wengi wasiokuwa na kazi. Na waliothubutu kujikakamua hawalipwi, wengine washauziwa mali zao na benki. Pesa inayozunguka kwenye barabara na miradi ya majengo toka mifuko ya jamii, NHC na taasisi ya serikali, kama kungekuwa na mipango madhubuti ya kuwaendeleza waandisi wazawa wangekuwa mbali sana sasa hivi. Sasa mtu kama huyu ameshindwa kuwa mlezi mzuri wa sekta moja anaweza nchi nzima. Tafakari.
 
Back
Top Bottom