Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Mlimpa kura Kikwete kwa kuwa mkewe alikuwa mwalimu lakini maisha ya Waalimu wa Tanzania mpaka leo ni ya kubahatisha
 
Kigezo kingekuwa ualimu siku nyingi mngekuwa mmemchagua MVUNGI
 
Ahahaha maccm yanavyojipa matumaini hadi huruma, amini msiamini mwaka huu labda mpigiwe kura na wanyama sio wananchi maana wananchi wameamua ku delete ccm.
 
Lowasa amejenga chuo kikuu cha dodoma,shule za kata,maji kanda ya ziwa;ufisad wake siujui hata nikiujua lazima nimchague nimechoka na ccm,wanaahadi,maneno,hotuba ndefu,wataalamu wa kuzungumza lakini kutekeleza 21%
 
Walimu tutampa Mwalimu mwenzetu Dr John Pombe Magufuli. Lowassa amesomea B.A. in fine and performing Arts!
 
Mimi mwalim nakuambia hapa shure walimu wote ni team lowasa,hata kama mnamuita fisadi,2tamchagua,2mechoshwa na ngonjera zenu
 
Kutegemea mabadiliko ndani ya Ccm kisa yupo Magufuli (Mwalimu) ni sawa na kutegemea kuvushwa Bahari kwa Boti iliyotoboka kisa yupo Nahodha Mpya"
 
Yalimshinda shemeji mmebaki na njaa zenu;
rudieni makosa yale yale, shauri zenu.
 
Mwalimu mwenye uelewa wa kutosha hawezi kushawishiwa kwa namna yeyote kukichagua chama cha mapinduzi na wagombea wake. Hili ni kutokana na ukweli kwamba ccm na wapambe wake wamewahi kuwatukana walimu na kukataa kura zao hadharani.

Walimu wengi wanataka mfumo mpya wa kuendesha nchi ili wananchi wengi wanufaikw na rasilimali za Taifa. wanafunzi wengi wamedumaa kiakili kutokana na lishe duni na hali mbaya ya maisha ya wazazi wao ambao imechangiwa na uongozi mbaya wa viongozi wa chama cha mapinduzi.

Kila mwalimu anataka mabadiliko ili keki ya Taifa igawiwe kwa usawa na kuborsha mazingira yao ya kazi, hivyo ni vigumu kwa mwali mu kujitokeza wazi na kusema anamuunga mkono nani kati ya wagombea wote japo anahitaji kusikia hoja na kummunga anayejipambauna vema kuboresha miundo mbinu na maslahi katika sekta ya elimu, afya, maji na uchumi wa nchi.
 
MAGUFULI NI ZAIDI YA LOWASA KWA 100% KIUTENDAJI:

Mgombea mteule wa CCM, Mh Magufuli ameonyesha uwezo wa hali ya juu kiutendaji akiwa waziri zaidi ya Mzee Lowassa katika kipindi chake akiwa waziri. Mh Magufuli ameonesha uthubutu katika majukumu yake katika wizara alizopita.

Wote hawa wawili wamelitumikia taifa hili katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Uwaziri. Kati ya hawa wawili, mmoja ambaye ni Magufuli kote alikopita ameweka record ya kipekee kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kutamani apewe majukumu makubwa zaidi.

Mh Magufuli, amekua tunu hata wizara nyingine alizokwenda na kumfanya ang'are zaidi tofauti na mzee Lowassa, katika wizara zote alizopita hakuna jipya alilolifanya zaidi ya kuacha malalamiko ya kero mbalimbali.

Mh Magufuli ndiye aliyeokoa upotevu wa magari ya miradi ya serikali ambayo watumishi wengi walikua wakijimilikisha magari hayo na kuyatumia vibaya kwakua yalikua na namba za kiraia na baadae akaanzisha program kuweka namba mpya za magari yote ya serikali, Mh Magufuli akiwa wizara ya ujenzi Watanzania tumempongeza sana na kwa juhudi,uboreshaji wa miundo mbinu kama barabara za kisasa, hakika huyu ndio kiongozi tunaemhitaji kwa sasa.

Mh Magufuli alipambana na wavuvi haramu waliokua wanatumia mabomu na nyavu haramu ijapokua wengine wachache walimchukia lakini wananchi wengi tumempongeza kwa kazi nzuri hata akiwa wizara ya mifugo, Magufuli mara nyingi ameonekana akiwa sites mbalimbali za ujenzi akisimamia shughuli zinazofanyika iwe usiku au mchana akishirikiana na sisi wanainchi. Hakika huyu ndiye kiongozi tunayehitaji kwa sasa.

Jimboni kwake, Mh Magufuli kupo vizuri barabara za lami, shule, ujenzi vituo bora vya afya na amekuwa karibu sana na wanainchi wake ukilinganisha na Lowassa kule Monduli. Lowassa katika kipindi chake wizarani ametumia fursa hiyo kujilimbikizia mali, kufanya biashara haramu na mataifa ya Ulaya, alijikita katika kutengeneza makundi yasiyokuwa na tija kwetu sisi wanainchi na zaidi kutuongezea umasikini.

Kama wazalendo tujiulize, huyu Lowassa anayedai kuchukia umasikini, katengeneza ajira ngapi kwa vijana wa Monduli? Zaidi ya maigizo anayofanya makanisani na misikitini, atueleze ni bodaboda wangapi kawapa mitaji zaidi ya kuwaburuza hususani wale wasiojitambua, vijana wengi wa kimasai kawapa fursa kiasi gani zaidi ya kukimbilia Dar es Salaam?

Kwa miaka zaidi ya 20 akiwa kiongozi hajaonesha nia ya dhati ya kumkomboa kijana, ataweza vipi kwa sasa na uzee unaomkabili ukiachilia maradhi anayokabiliana nayo. Alipokua waziri Mkuu Wafuasi wake wamekua wakimpongeza sana kwamba ana maamuzi magumu ambayo kama ni shule za kata zimechangiwa na wanainchi chini ya ilani ya chama cha CCM, yeye alikuwa na jukumu la kusimamia zoezi hilo tu.

Jimboni kwake kwenyewe hakuna maendeleo yeyote yale, maisha ni magumu sana kuliko majimbo mengine.
Zaidi ya kujilimbikizia mali hakuna jipya alilofanya mzee Lowassa pamoja na kupendwa na bodaboda wachache wasiojitambua maana ukiwauliza kwanini wanampenda watakujibu basi tumempenda tu"

Ahahahaaa, wengine watakujibu kuwa wanataka mabadiliko, sasa hebu jiulize mabadiliko gani atakayokuletea wakati Jimboni kwake kwenyewe ni njaa tu!!! Ninachokiona kwa babu yetu ni safari ya Matumaini kweli!!
 
Shemeji unatuachaje?
Katuachia pombe na makufuli mlangoni ili tusitoke. Kama tuna akili timamu, CHAGUA E.N. LOWASA.
 
Alituambia kigamboni tupige mbizi.

Lowassa hana maneno mengi wala kauli za kuudhi..RAIS
 
Magufuli ndiyo chaguo sahihi anafanya anacho kiamini yule mwingine maneno yake na matendo vinatofautiana sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…