Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Magufuli ni mpinzani na anazungumza kupinga mfumo na namna ambavyo CCM na serikali yake inajiendesha. Yeye ni anti establishment. Anabomoa nyumba alimo,sasa najiuliza yeye ni mpinzani ndani ya chama na serikali? Na je unaweza kubomoa mfumo ambao yumo ndani yake?
 
Mwigulu akomae jimboni kwake, anaweza asipate huo ubunge.
 
Tumeshaamua wala huwezi kubadilisha mawazo yetu Watanzania tumeamua ccm OUT...nendeni kuzimu
 
Pole sana Mkuu. Kwani Lowasa alipohutubia pale Jangwani aliitaja CHADEMA ama UKAWA? Magufuli amekuwa mtiifu kwa CCM siku zote. Huwezi kuanzisha propaganda za kipuuzi wakati huu

Lowassa mzee wa maigizo anapaswa kuwa rais wa THT
 
Magufuli anakuwa mpinzani kwenye chama kilichomlea.
 
Pole sana Mkuu. Kwani Lowasa alipohutubia pale Jangwani aliitaja CHADEMA ama UKAWA? Magufuli amekuwa mtiifu kwa CCM siku zote. Huwezi kuanzisha propaganda za kipuuzi wakati huu

kimsingi lizaboni , ukumbuke hakuna mgombea binafsi sheria inatamka mgombea kubebwa na chama.hapa twende mbele serikali hii kule Ruvuma imekopa watu mahindi na mengine wakatakataa kuyanunua kutaja ccm maanake ni kaa la moto.
 
Magufuli haoneshi kwamba CCM haijafanya kitu hapo awali, ila anaonesha sehemu ambazo zinahitaji kushughulikiwa. Marekani ina zaidi ya marais 40 lakini kila anayekuja anatangaza sera mpya, ina maana kuwa Marais wa Marekani waliopita hawakufanya kitu chochote? la hasha bali hakuna uongozi unaoweza kufanya kila kitu na utambue kuwa mahitaji ya wanadamu hayaishi kamwe.

Magufuli ni mgombea mzuri na anafaa zaidi kuiongoza Tanzania kuliko mgombea mwingine yeyote; tumchague kwa maendeleo ya Taifa letu
#hapakazitu
 
Magufuli hajui hata anaongea nini maana marais wa CCM waliotangulia wamemuharibia hadi anaonekana ndio walewale.
 
Kama hujitambui utaweza kutambua fikra za watu wengene?

Kwani nani amekuambia Magufuli anagombea uongozi wa CCM?

Magufuli anatafuta mandate ya Watanzania wote na siyo ya CCM.

Kwenye mambo ya CCM alishamalizana na CCM yake.

Kwenye mambo ya kitaifa, taifa kwanza, chama baadaye.

Kalagabaho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…