Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Kuna mambo yanakera sana. Kwani kuzaa ni shule tu. Na wafanyakazi watapewa likizo ya uzazi kila mwaka. Tuache kupotosha watu.
 
Hayo ameyasema raisi Pombe, muda siyo mrefu kwenye kampeni zinazoendekea mkoani Singida, nanukuu.

"Elimu ni bure, wakinamama zaeni hakuna haja ya kupanga uzazi, matiti ya kunyonyesha mnayo, wanaume wa kuwapeni mimba wapo."

Toa maoni je ni kweli kupanga uzazi hakuna maana kama wataalamu wanavyo shauri, hii siyo mara ya kwanza Magufuli kuwaambia watanzania kuwa zaeni, msipange uzazi.
Kwani sifa za pombe huzijui kaka?
Unajua majina kwa asili hutoa tafsiri halisi
 
Mgombea wa ccm ninakujulisha kuwa najua uwezo wako wa kukalili mambo kama kipindi kire unafundisha chemistry umepungua sanaaa nafahamu kiwango chako cha kukalili ila nmeshutushwa na wewe kushindwa kumeza Ilani nzuri ya chama cha mapinduzi.

Ninajua kuna yaliyoandikwa hutaki kutataja kisa unaogopa kuongopa kwa sababu uwezekano haupo ila ninakushii tafadhali jitaidi kusema yalitofnywa na yatakayo fanywa maana ni ilani tambua hata husipotenda wewe atakae kuja badala yako anaweza tenda ila kama ni mazuri.

Mwisho nawapongeza mliojitokeza mwanza kumpokea Tundu Antipas Lissu maana mmevunja rekodi
 
Mgombea wa ccm ninakujulisha kuwa najua uwezo wako wa kukalili mambo kama kipindi kire unafundisha chemistry umepungua sanaaa nafahamu kiwango chako cha kukalili ila nmeshutushwa na wewe kushindwa kumeza Ilani nzuri ya chama cha mapinduzi...
Mawazo ya Magufuli na yaliyomo kwenye ilani ya ccm ni ardhi na mbingu
 
Mgombea wa ccm ninakujulisha kuwa najua uwezo wako wa kukalili mambo kama kipindi kire unafundisha chemistry umepungua sanaaa nafahamu kiwango chako cha kukalili ila nmeshutushwa na wewe kushindwa kumeza Ilani nzuri ya chama cha mapinduzi..
Wamevunja record ipi ebu acha unafiki
 
Mkuu hoja yangu ya msingi ni IPI lugha Kali IPI so lugha Kali. Kwa mujibu wa maelezo yako ni kuwa lugha kuwa kali ama sj Kali inatokana na perception ya MTU ..Mimi sikubaliani na wewe! Maelezo yako hayajitoshelezi...
Hakjna ukakasi hapo ngono zembe ndiyo kitu nyie mnaleta interpretation tofauti kabisa ya hoja ya JPM..Mimi sikumsikia ila maelezo ya humu inaelekea aliwaambia wannanchi waendelee kuzaa na kwamba matiti yapo kwa anili ya kunyonyesha what is wrong with that kumbuka JPM ni mwalimu na anaweza akatumia maneno kuijenga hoja yake.

Sasa ngono zembe ndiyo Nini...yeye amesema wazae na hajasema waende kufanya ngono..ipo tofauti hapo.....ila kwa kuwa wengi mnafikiri kibeberu na kutafuta makosa inakuwa shida kwenu.
 
Mada Maalum itakayozungumzia ziara nzima kwenye mchakato wa kampeni za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mama Samiah Suluhu.

Agosti 25, 2020
M/Kiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage kwa mamlaka aliyopewa amemteua Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mama Samia Suluhu kuwa mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais kupitia CCM.

UPDATE:-

IMG_5988.png
 
Back
Top Bottom