Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu



Leo Dkt. Magufuli, mgombea Urais kupitia chama cha mapinduzi yuko viwanja vya Bombadia vilivyopo manispaa ya Singida mkoani Singida kwenye kuendeleza ngwe yake ya kampeni. Leo ametokea mkoani Dodoma na alisimama vituo vitatu vidogo vya Bahi, Ikungi na Manyoni kabla hajafanya mkutano mkubwa wa kampeni mkoani Singida.

Kuwa nami kukujuza yanayojiri kutoka viwanja hivi vya Bombadia.
========
Wasanii wa kuvutia watu hawajaanza kukata mauno, naomba pia mumuulize aliempiga risasi 16 kijana wenu Tundu Lissu yupo wapi. Cc YEHODAYA johnthebaptist

Sent from my Infinix X573 using JamiiForums mobile app
 
Nanyie wabongo acheni kulalamika mkiambiwa uzazi wa mpango mnasema Mara Freemason hao mara new world order! Mkiambiwa mzae napo mnalalamika sasa mnataka nini?
Kama waliosoma hadi level ya PHd ndio wana mawazo ya ajabu kama ya Magufuli, mimi ni bora nibaki na degree zangu mbili za ubanduaji maganda ya mawese.
 
Mpaka sasa Magufuli anatiririka vizuri sana.kama ni mshambuliaji basi mpaka sasa kesha pachika hertrick anasubiri dk 90 ziishe achukue mpira wake.
 
Yaani ccm pamoja na kazi zote wanazo jisifu wamezifanya bado hawajiamini wanatembea na wasanii wa music ili kuwavuta wananchi! dah kumbe ndiyo maana Kingunge alisema ccm imekata pumzi
 
Wafanyakazi walikuwa wanapumbazwa na mbio za mwenge wa uhuru, ni fursa nziri kwao kuzikata nira za CCM zilizopo shingoni mwao mwaka huu, suluhu kubwa kwao ni kuikatalia mbali tu ktk sanduku la kura.
 
Kweli Polepole na Bashiru ndiyo mwisho wenu wa kufikiria umeishia hapo. Yani karne hii ya technologia na utandawazi na mwenyekiti wenu mkamshauri ivyo na bila kusita akakubali.

Kweli wasanii ndiyo mmeona ni njia ya kuwadanganya/ kuwarubuni Watanzania ili wawachague tena.

Yani Mtanzania mwenye miaka 18+ na akili zake timamu usawa huu aende kuchagua kiongozi sababu tu ya matamasha ya wasanii ya bure?

Mimi hapa mimi nikupe kura sababu umaleta wasanii 200+ kutumbuiza kijijini kwangu na umewalipa mabilion ya pesa huku maji hatuna. Kweli yani kweli.

Kweli CCM ndiyo imefikia hatua ya kutushusha Watanzania namna hii?

Hawa wasanii wenyewe tunapiga nao pombe huku kitaa wakiwa wanatutambia kuwa wapo msimu wa mavuno ila wanajua baada ya kampain maisha yao yanarudi kulekule.
 
Back
Top Bottom