Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Wanachoweza ni kumleta Diamond na Konde boy nawashauri vijana kwa ukata uliolikumba Taifa wakileta wasanii nyie nendeni mkawashangae lakini kura mnajua pa kuzipeleka. CCM wanawaona kama watoto wa kuku kuwa kesho mtanyonyeshwa.
 
Kweli jiwe limepata moto.
1 Elimu ya kuunga unga na mitaala mibovu.
2. Uhaba mkubwa wa Madawati, vitabu,waalimu,majengo ya madarasa nk.
3.Ukosefu wa Ajila ugumu wa maisha nk.

Mwambieni watanzania wana hofu ya kuzaaa. Vyuma vimekaza.
 
Kweli Polepole na Bashiru ndiyo mwisho wenu wa kufikiria umeishia hapo. Yani karne hii ya technologia na utandawazi na mwenyekiti wenu mkamshauri ivyo na bila kusita akakubali...
Miaka yote ccm huwa wanawaona watz wajinga , tena wajinga wa kutupwa, labda wewe ulikuwa hujagundua tu.
 
Hizi ndiyo kauli ambazo wafadhili hawataki kuzisikia, Wanabana misaada anayeumia Ni Mwananchi wa kakwaida ifike mahali zisitamkwe hadharani.
 
Anataka tuongeze wapiga kura wa CCM.
Umewaza vema....nchi ikiwa na idadi kubwa ya watu ni power kwa serikali kisiasa na kiuchumi maana itaongeza wapiga kura na walipa kodi...ingawa kwa mtu mmoja mmoja ni taabu tupu....Jiwe is on long plan for whose sake? Only God knows.
 
wakinamama zaeni hakuna haja ya kupanga uzazi, matiti ya kunyonyesha mnayo, wanaume wa kuwapeni mimba wapo.
Maneno haya yangesemwa na mwengine angeambiwa katukana. Yajayo yanafurahisha.
 
..huu ndio mtizamo ambao Magufuli ameujenga kwa muda mrefu, na amekuwa akipita kila mahali kusisitiza hilo.

..kwamba eneo husika kupata maendeleo raisi/magufuli ndiye muamuzi. Na asipojisikia, au asipokuwa na mahusiano mazuri na mbunge wa eneo hilo, basi hakuna maendeleo.

..kama anakusanya kodi kila mahali ktk nchi hii, basi miradi ya maendeleo igawanywe kulingana na mahitaji, na siyo raisi anajisikia vipi, au mbunge ana mahusiano gani na watawala.
 
Ulimbukeni wa ajabu, uzuri Watanzania wajinga wanapungua.
Leo Ikungi kasema ... Mtaturu miezi michache kaniomba maji..... wengine walikuwa hawaombi..( Lissu) ..
Aibu na fedheha kwa wananchi toka kwa mtawala.
 
Hupenda kuzuia maendeleo kwenye majimbo ya wapinzani mpaka siku akipita anaitisha mkutano anaomba wananchi waulize maswali baada ya maswali humdhalilisha mbunge wa upinzani na kisha kutoa Amri maendeleo yafanyike haraka na ndipo wananchi huona kuwa bila yeye mbunge angefeli kuleta maendeleo ni mbinu zake za kujionyesha kuwa bila yeye hakuna maendeleo popote Nchini.
 
Magufuli anaamini fedha zote za serikali ni mali yake na ana uwezo wa kuzitumia bila kupitia bungeni, ndiyo sababu amekuwa akichota fedha hazina na kuzitumia bila idhini ya Bunge. Full kuvunja sheria!
Akitoka madarakani kama tunavyotarajia atatakiwa kujibu mambo haya , hakutakuwa na mswalie mtume
 
Ulimbukeni wa ajabu, uzuri Watanzania wajinga wanapungua.
Leo Ikungi kasema ... Mtaturu miezi michache kaniomba maji..... wengine walikuwa hawaombi..( Lissu) ..
Aibu na fedheha kwa wananchi toka kwa mtawala.
Eti aombwe maendeleo utazani bila yeye hawapaswi kupata maendeleo wakati wanalipa kodi za maendeleo
 
Back
Top Bottom