Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Kweli nimezeeka. Kuna vijana wawili walikuwa wakisoma mlimani huku wakifanya muziki. Mmoja alikuwa Engineering akadico alikuwa akitamba na wimbo unaitwa Acquilina. Mwingine aliimba wimbo uliovuma sana "...bure mtakunywa sumu..." aliimba na Stara Thomas. Huyu aliokoka akaacha muziki.
 
Ebana unataaka kuniambia mchizi alikuwa udsm
 
Gonjwa hili limezua kizazaa, mzozoo.. gumzo..gumzooo kwa mabronzo, masista du, machizi, wazazi, walimu na wanafunzi..

Mzee wa kidhaa dhaa...
Mshikaji yupo mpaka leooo.

Ebana kulikuwaga song flanii linaitwaaa chelea pinnaaa ivi unawakumbuka hawa washikaji
 
Daa kumbe Castro ndo yupo jela mpaka leoo
 
Kwanza imeanza mwaka 1990, diplomats wamekuja baadae kidogo. We unayewajua diplomats tupe historia
Ebana Mkuu kuna SONG FLANI LILIKUWA LINAITWAA OYA MSELA OYAA OYAA MSELAA

HIVI UNAKUMBUKA WASHIKAJI WALIOTOA LILE GOMA LILIHIT SANA MIAKA HIYO.

BILA KUSAHAU ULE WIMBO MIMI NI MSELA SIWEZI KWENDA JELA NIKIENDA JELA NINARUDI NA MAHERA DAH HATA MSANII AMENITOKA
 
Huyu jamaa alikuwa mkorofi sana na nashangaa sana jinsi alivyobadilika, si nasikia kipindi fulani waliwahi kumnyoa nywele kisa kawaponda kwenye video yao kipindi cha planet bongo
Dah huyu mshikaji kuna tetesi nilikuwa nazisikiaga kipindi akiwa mkorofi alikuwa anaringia ana ndugu zake wengi wako serikalini hivyoo wangemtetea tuu
 
Mkuu hizo lyrics nilikuwa nahamishia kwenye daftari la shule.. Nakumbuka Salome ya dully ndio ilikuwa page ya kwanza.
 
jamaa aliye imba na stara thomas alikua anaitwa K Basil aise kitambo sana Mkuu
 
Nashindwa ku-upload video yenye documentary za hip hop ya bongo yenye watu kibao kama x plasterz,gwm,inspector,sugu etc...inafurahisha i think you will enjoy it...Anaejua vzr ku-upload anicheck 0767712840 nmtumie watsap ili tushee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…