Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

dah yani hakuna hata mmoja ambaye kamgusia sugu au ndio umri maana sugu akitisha enzi zile za 90s pamoja na kijana mmoja akiitwa balozi uyu jamaa alilkuwa balaa ila profesor jay alivyokuja kuimba chemsha bongo jamaa akaaga mashindani akaona isiwe tabu akatoa nyimbo yake ta mwisho , "kwenye nyati"
 
Kwanza Unit sidhani kama walishindana na Diplomats, diplomats wamekuja baade nadhani hata Nigger One alikuwa ameshafariki. Kunawatoto walikuwa wanaitwa Dar Young Mob nao walikuwepo mwanzoni mwanzoni mwa miaka ya 90
 
Huyu jamaa alikuwa mkorofi sana na nashangaa sana jinsi alivyobadilika, si nasikia kipindi fulani waliwahi kumnyoa nywele kisa kawaponda kwenye video yao kipindi cha planet bongo
Kalama Masoud kazeeka sasa,
 
Kwanza Unit sidhani kama walishindana na Diplomats, diplomats wamekuja baade nadhani hata Nigger One alikuwa ameshafariki. Kunawatoto walikuwa wanaitwa Dar Young Mob nao walikuwepo mwanzoni mwanzoni mwa miaka ya 90
Unawajua DIPLOMATS lakini!? Au nayo haudhani kama unawajua!?
 
dah yani hakuna hata mmoja ambaye kamgusia sugu au ndio umri maana sugu akitisha enzi zile za 90s pamoja na kijana mmoja akiitwa balozi uyu jamaa alilkuwa balaa ila profesor jay alivyokuja kuimba chemsha bongo jamaa akaaga mashindani akaona isiwe tabu akatoa nyimbo yake ta mwisho , "kwenye nyati"
Mkuu miaka ya 90 hakukuwa kuna msanii anaeitwa SUGU Bali miaka 95 sugu alikuwa akijulikana kama 2 proud na nyimbo iliyomtoaa ilikuwa ni NI WAPI TUNAKWENDA

BUT miaka 97 2 proud alibadilika na kujiitaaa Mr. Two hapo ndipo tulianza kumjua sugu akijulikana kama Mr .two na nyimbo iliyomtoa ilikuwa inaitwa deiwakaa , badae akashusha GWM walimshirikisha katika nyimbo yao ya YAMENIKUTA hapo ndipo nyota sugu ilianza kunga'aa ila yote Tisa nyimbo ya sugu ya MAMBO YA FEDHA akimshirikisha lady jay dee ndo ilikuwa ngoma hatari sana .

Kwa kifupi SUGU ni mmoja kati ya maufounder wa muziki wa bongo flevaaa
 
Kwanza Unit sidhani kama walishindana na Diplomats, diplomats wamekuja baade nadhani hata Nigger One alikuwa ameshafariki. Kunawatoto walikuwa wanaitwa Dar Young Mob nao walikuwepo mwanzoni mwanzoni mwa miaka ya 90
Hivi kati ya kwanza unit na diplomatics ni hivi ni nani walianza katika gemuu ya muziki
 
Kwanza imeanza mwaka 1990, diplomats wamekuja baadae kidogo. We unayewajua diplomats tupe historia
 
Daah kalapina alikuwaga mtata sana ila mwisho wa maneno ilikuwa dudubaya alivyompiga Mr.nice hadii akamvunja kiuonoo.

Bila kusahau kuna msanii kwa jina Steve to k alipigwagaaa kisu hadi kifoo sijui wangapi wanamkumbuka
Alipigwa kisu na producer wake dah sijui kesi ile iliishia wapi.
 
Ngoma kali ya Japharai Niko Bize na ile cheza ya yule mshakaji mwenye sweta la rangi black na white/milk (cmjui jina), jamaa ana.slide utadhani States vile.
Na pini la Kibanda cha simu -- (Soggy Doggy Anter) vile wana.walk na wale ma.shorty vitovu nje. Haaa raha sana!
Niishie hapo.
 
Wapi Nataka demu ya Jay mo kuwarusha madem wa bongo wakali wa enz zile faudhia Euginia kajala..... na likaja Goma la kufa mtu booonge la Hip hop ingekua Vipi Mwanafalsafa feat Jay mo ilkua balaa sana miaka ya 2002+.enz zile shigongo gazeti zake anaweka na Lyrics za nyimbo za bongo au America bila kusahau Billboard chart au Bamiza..
 
Back
Top Bottom