Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Uwe una acha uongo. Odessa ili pigwa makombora. Na baadae UN ika omba port ya Odessa iwe huru kuruhusu nafaka kusafirishwa. Ebu tumia akili ndogo tu ya Google: Odessa Port Hited by Russian Forces uone maajabu ya Google
Hivi Mkuu; Odessa ilipigwa makombora baada ya Ukraine kuwa imeshapokea hizo anti Drones system (the Drone dome) au kabla? Hiyo data ya Google ni ya lini?
 
Mkwara wa ku'tishia nyukilia mimi nauita ni "Bogus Threats". Russia hawezi kutumia nyukilia anajua kabisa kitakachofuata dhidi yake na watu wake. U.S, NATO na washirika wata respond accordingly.
Ah! Mbona watakuwa wamemlamba kichwa kabla hajazifikia hizo nyuklia zake? Putin anao maadui wengi sana kwa sasa - Nje, Ndani na Miongoni mwa watu wake. Wote wanamlia Time tu ajichanganye kidogo waondoke na kichwa chake fasta.
 
Hivi Mkuu; Odessa ilipigwa makombora baada ya Ukraine kuwa imeshapokea hizo anti Drones system (the Drone dome) au kabla? Hiyo data ya Google ni ya lini?
Muulize swali dogo, kuna Wanajeshi wa Urusi wamekanyaga Odessa? Hata hayo Makombora ni machache yaliyopenya. Wakati vita inaanza kila Mwananchi Odessa alipewa Bunduki AK 47.

Kuna makombora yanaponyoka ndo yatua kwa raia.

Muulize kambi gani ya Ukraine bomu la Urusi limetua Odessa? Kumbuka ule ni Mkoa.

Hata hivyo kuwajibu hawa unajipotezea muda. Achana nao.

Wanataka tuanze kubishana. Urusi walijaribu kutua Odessa na Askari wa Miamvuli wote wakatunguliwa kabla hawajafika chini. Hawajarudia tena. Nia ya Urusi ni kuteka Bandari ya Odessa. Wameshindwa. Eti UN. Urusi inaheshimu UN? Mbona waliwaambia waondoke Ukriane hawaondoki. Kenge hasikii hadi damu itoke masikioni. Ndicho kiantokea wanaretreat
 
Wakiomba Afrika, wanaweza kupata vijana wengi wenye nia ya kupigana kwa kujiunga na jeshi lao
Thubutu! Mbona walishaomba na kuweka ahadi za mishahara minono kwa anayejiunga ikiwa ni pamoja na malipo kwa familia yake atakayoiacha nyumbani? Je, Walipata wangapi? Vijana wakwake yeye mwenyewe wanamkimbia - hawataki vita ya kijinga kihivyo.
 
Kwa mfano, kwa hapa kwetu vijana wengi wanatafuta nafasi za jkt n.k, kama watapewa hiyo fursa watajiunga
 
Kwa mfano, kwa hapa kwetu vijana wengi wanatafuta nafasi za jkt n.k, kama watapewa hiyo fursa watajiunga
Nasemaje? Vijana wengi wa hapa kwetu wanaotafuta nafasi za JKT wanafanya hivyo ili kupata sifa mojawapo ya kujiunga na JWTZ, Magereza , Polisi, Uhamiaji au Ulinzi kwenye Makampuni na baadhi ya Asasi zisizo za kiserikali. Halafu mkuu, unazungumzia vijana gani -wa hapa kwetu? Mbona vijana wa hapa kwetu ndo hao wanakimbizwa na panya rodi? Hivi watauweza mziki wa Frontline ya Ukraine??? Wewe unataka kuwaponza vijana wa kibongo wala chips dume hawana hata pumzi ya kukimbia. 😆 😆 😆 🏃‍♂️ Waache bhana vijana wetu waendelee kuvaa mlegezo kwa raha zao.
 
Hivi Iran ilitoa drones ngapi? Nadhani zinakaribia kuisha. Hii gapa nyingine umeangushwa Odessa
IMG_20220927_133731_205.jpg
 
Hawa Warusi baada ya kuona wenzao wengi wamekufa na wengine kujeruhiwa, ikabidi wajisalimishe. Ni baada ya kupelekewa moto. Muda wote walikuwa hawajaona drone kama ipo juu yao
 
Back
Top Bottom