Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Inaweza kuwa kweli maana Germany ametoa ofa kwa wanajeshi wa Russia ambao hawako tayari kupigana vita atawapokea na kuwapa hifadhi ya ukimbizi ,vile vile akasema hata kama kuna watu wengine raia wa Russia ambao hawakubaliani na Putin waende watapokelewa.

Huu ni mtego na mwiba kwa Putin maana wanaweza kupewa mafunzo na kurudi nchini mwao na kuanzisha vugu vugu la mapinduzi au uasi.

Kama unavyosema hawa wanaweza kuungana na wale wanaompinga na kuleta mapinduzi ndani ya nchi yake.
 
Odessa inashambuliwa kwa meli. Odessa ni pwani na kuna bandari kubwa, ndo kila siku Urusi wanapambana waiteke ila kila wwkipanga shambulizi wanakuta Ukriane wapo Vizuri.
Na ni mji wa Kitalii kwahiyo Russia anatamani aiteke ili avuruge utalii ndio maana alikuwa akilenga majengo ya zamani kwenye huo mji lengo ayaharibu.
 
Wananchi wa Jamhuri ya Czech, wametenegenza sanamu la Putini akiwa amekalia cho dhahabu na kuiweka mbele ya Ubalozi wa Urusi
View attachment 2369583
Kama Putin na Genge lake bado wanazo chembe za Ufahamu vichwani mwao; hii ni salaam tosha kutoka kwa watu walio nje na ndani ya nchi yake wanavyomwona Putin katika vita hii baina yake na Ukraine. Wanamwambia yupo uchi, asimame chap avae boxer yake na kuisitiri aibu yake i.e. Abadilike na aachane na hiyo vita ya kunya - haina maslahi kwake.
 
Wanajeshi wa Urusi waliojisalimisha wakiwa wanapewa Huduma ya kwanza
View attachment 2369592
Kama wewe ni "Christianescovick" soma Math.5:43 - 48.
Mmesikia kwamba ilisemwa: 'Mpende jirani yako, na kumchukia adui yako.' Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu ...
Ukraine pamoja na kudhulumiwa anaonesha huruma na Upendo kwa Mrussi ambaye ni adui yake.
Hakika Ukraine atabarikiwa kwa hilo. Ushindi ni lazima. Heko/Slava Ukraine.
 
Huu mjadala wa hawa wakimbizi wa urusi unafurahisha sana.

wafaransa na wajerumani wanadai kuwazuia hao vijana wasiingie mataifa ya ulaya ni kinyume cha mira na desturi ya watu wa ulaya.

Norway na Finland wanadai hawa vijana walikuwa wanaunga mkono uvamizi wa Taifa lao muda wote na kwamba hii mambo ya kukimbia ni uoga tu wa kuuwawa ila wanaunga mkono vita.

nikawa naona hawa Finland ni kama wanazungumzia mpaka hawa warusi wa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…