Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Wakuu, hili daraja kulipuliwa na aibu kwa Urusi iliyodai inalilinda hili Daraja kwa Mitambo maalum. Halafu lilipo ni mbali na Frontline ya Ukaine ilipo. Hadi wikii iishe, lote litakuwa chini. Urusi watawaambia nini wafuasi wao?
View attachment 2380601
Urussi watawaambia wafuasi wao kwamba daraja lipo vizuri ila mafundi na wahandisi wanalifanyia ukarabati mkubwa ili liweze kupitisha vifaru na ndege - Nyie Tulieni.
 
Warusi sasa hivi hawana tofauti na nguruwe pori, maana wanashinda kwenye mahandaki.
Ngoja chakula kiishe. Watatoka tu kufuata au kutafuta kingine.N a hapo ndio itakuwa kuilia na kusaga meno.
 
Mzee wa mikwara Putin alisema ikitokea nchi yeyote ikagusa Daraja lake la Crimea basi atatandika nuclear.

Leo anasema itakuwa ni kitendo Cha kigaidi tu na sio Ukraine waliotandika sababu hawana uwezo.

Kapewa zawadi yake ya birthday ya kutimiza miaka 70 Duniani.

Asanteni.
Happy birthday Putin
 
Warusi wameanza kuikimbia Crimea, Watapita wapi? Kila siku tunawaambia Ukraine sio kwao walikuwa hawaelewi
View attachment 2380604
Sasa wameelewa ila wamechelewa kidogo. Pale darajani cjui watatumia chopa au waogelee kama hakuna mamba. Vinginevyo wasubiri maji yagande kuwa barafu halafu watajipitia kiulaini wakitembea kwa miguu. Kiburi chao kitaisha.
 
Uungwana ni ku surrender. Angalau inakupa possibility ya 50% survival. Failure to comply the order, is to threaten your life by 100%.

Uungwana ni vitendo, wakikaza fuvu watageuka kuwa mizoga. Aliyewapa order ya kuja kuua wa Ukraine hakuna hata mtoto wake aliyeenda kwenye mobilized troops. To surrender is the very best option for them.
Kabisa Naumga mkono hoja. Hakuna sababu ya kuumia kwa ajili ya mijitu ambayo kwanza haina hata shukrani. Wenyewe walianzisha vita halafu wanawasukumia huko watoto wa wenzao eti wao ndo wakafe. Hatua ya kwanza ni kujisalimisha tu- mambo mengine baadaye
 
20221008_125239.jpg
 
Hicho ndo walikuwa wanakitafuta. Warusi wanadai siyo makombora la Ukraine bali ni bomu limetegwa. Swali la kujiuliza daraja kubwa kiasi kile kwa ulaya nzima halina ulinzi mpaka mtu akatege bomu?
Mhhh! Mfa maji haachi kutapatapa.
 
Wanajitetea. Hata hivyo plan ilikuwa ni kulilipua, tutege bomu, turushe kombora au nyambizi. Leongo moja kukata mawasiliano na tumefanikiwa. Wataka kutupangia tubomoe kwa kutumia Sururu au?
Watulie tu; dawa inaingia taratibu.
 
Hebu toa maelezo ya mlipuko huo tafadhari. Umetunyima uhondo. Wengine tunapata furaha sana tunapoona maghala ya silaha za warusi yamelipuliwa. Kulipuliwa Crimea Bridge imetupa furaha kubwa sana leo.
Kwa kweli leo, Hiiii; tumejawa na furaha tele.
 
Hivi mnakumbuka hiki kikosi cha airborne assault brigade? Wao huwa hawaogopi Warusi. Wana Spika zao Frontline, wanawatandika huku wamewawekea Muziki wa nyimbo za kishujaa za wanajeshi wa Ukraine. Sema saa nyingine wanawatega Warusi, Wanaweka Spika juu ya handaki Warusi wanajua wapo hapo kimbe wamehama mapema. Ile wanajifanya kwenda kuwateka Urusi wanatokewa kwa nyuma wanalizwa. Walishazoea, Wana Spika nyingi Frontline.
 
Back
Top Bottom