Tatizo wanadhani napost picha kushindanisha kati ya Urusi na Ukraine. Mimi napost mafanikio ya Frontline ya Ukriane. Ingependeza mtu akija kusema nimedanganya aseme ukweli aniumbue. Lakini sio kunitukana. Kosa langu kuongea ukweli au? Tunakosa mijadala yenye tija sababu mtu haji na hoja. Hii ni vita tuitumie kujifunza silaha mpya na mbinu mpya za kijeshi. Mfano leo Ukraine imeachia Wanajeshi wa Urusi 218, aje mtu aseme walikuwa wafungwa 10. Wenzetu Africa hasa Ghana na Nigeria wanabishana kwa hoja, ila Tanzania anayejua matusi na udhalilishaji ndo anaonekana mwenye point. Tanzania muna safari ndefu kufikia uhuru wa kujieleza. Pro Urusi wa huko Tanzania wanaona matusi ndo dili. Nasikitika sana.. Ndo maana siwajibu sababu hawajengi hoja